Jumatatu, 07 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mkutano wa Khiyana pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kiyahudi
(Imetafsiriwa)

Habari zilizuka kuhusu mkutano uliochukua takriban saa mbili kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya Najla El Mangoush na Waziri wa Mambo ya Nje wa umbile la Kiyahudi jijini Roma. Suala hilo lilipofichuka, Waziri Mkuu Abdul Hamid Dbeibah alitoa amri ya kumsimamisha kazi Najla El Mangoush katika Wizara ya Mambo ya Nje. Kufuatia kuenea kwa habari hii, watu walikusanyika kupinga mkutano huu wa kisaliti na adui wa Kiyahudi. Walilaani mkutano huu, ambao ulionekana kama aina ya uhalalishaji mahusiano na umbile linaliokalia kimabavu Palestina, ikionekana kama kitendo cha kisaliti cha kuisalimisha Palestina kwa kuikabidhi hadharani kwa Mayahudi. Inafaa kufahamu kwamba kujisalimisha huku kumekuwa kukiendelea kwa miongo kadhaa, na hatuwezi kusahau hija ya Jerusalem mwaka 1993, ambayo ilifanyika wakati wa utawala wa Gaddafi katika karne iliyopita. Ilikuwa ni hatua ya kwanza ya utawala huo kuvunja kizuizi cha kisaikolojia ndani ya Umma wa Kiislamu kuhusiana na mkaliaji wa kimabavu wa Palestina.

Inafahamika wazi kwamba nchi za kikafiri zikiongozwa na Marekani na pamoja nazo, Uingereza, ndizo zinazotumia zana zao za ndani katika maeneo ya mashariki na magharibi mwa nchi. Wanasukuma mambo haya yanayokinzana kuelekea kukaribiana na umbile nyakuzi la Kiyahudi huko Palestina. Ukafiri ni mila moja, na utiiifu wao unapelekea kwenye udhalilifu na fedheha hapa duniani. Hakika uhalifu wao ni mkubwa, na mwenye kuutenda atapata adhabu hapa duniani na kesho Akhera. Anasema Mwenye Nguvu na Mwenye Uwezo:

[سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ]

“Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya.” [Al-An'am:124].

Sisi katika Hizb ut Tahrir/Libya, huku tukilaani vikali kitendo hiki cha uhalalishaji mahusiano na tabia hii, ambayo kidini (Shari') imeharamishwa na kuchukuliwa kuwa moja ya madhambi makubwa ya kukubaliwa na kuridhika nayo, tunayaona haya yote kuwa ni hatari sana, hususan kuisalimisha waziwazi ardhi takatifu kwa adui mnyakuzi, Mayahudi. Hili ni jaribio la kuficha hukmu ya Sharia ambayo kila Muislamu anaijua, ambayo ni kwamba Palestina ni ardhi ya Kiislamu iliyobarikiwa, kama inavyoonyeshwa na maandiko ya Wahyi wa Mwenyezi Mungu ambayo yamekuja kutoka juu ya mbingu saba. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ]

“SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.” [Al-Isra:1].

Kuikomboa kutoka kwa adui mnyakuzi ni wajibu kwa Waislamu wote, hasa wale wenye nguvu katika ardhi za Kiislamu. Faradhi juu yao hata ni kubwa zaidi.

Enyi Waislamu nchini Libya na kwengineko, yale ambayo nchi yetu inayashuhudia yanalazimu utimizo wa haraka wa wajibu huu wa Shari’: kusimamisha tena maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume katika ardhi za Waislamu. Kupitia hili, mnaweza kufanya kazi kuelekea kuzikomboa ardhi na watu kutoka kwa utawala wa makafiri nchini Palestina na ardhi nyinginezo za Kiislamu. Nyinyi, enyi Waislamu, hamna budi ila kujiunga na safu za wale wanaofanya kazi pamoja na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida iliyokaribia, kwa mapenzi ya Mola Mtukufu, ili kuukomboa Umma kutoka mikononi mwa watawala hao vibaraka wanaoungwa mkono na Magharibi.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَقُلِ اعْمَلُوا فَسَيَرَى اللَّهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُ وَالْمُؤْمِنُونَ وَسَتُرَدُّونَ إِلَى عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ]

“Na sema: Tendeni vitendo. Na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini wataviona vitendo vyenu. Na mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhaahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda.” [At-Tawba:105].

H. 15 Safar 1445
M. : Alhamisi, 31 Agosti 2023

Hizb-ut-Tahrir
Libya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu