بسم الله الرحمن الرحيم
Kwa Wote Waliojadili, Kutia saini, Kunyamaza, na Kutoa Baraka
Nyinyi na Kuchora kwenu Mipaka na Mayahudi muko chini ya Miguu ya Watu wa Lebanon na Umma wa Kiislamu
(Imetafsiriwa)
Baada ya makubaliano ya kuchora mipaka na Mayahudi, wavamizi wa Palestina, ilikuwa ni habari tu na uchambuzi uliosambazwa na wanasiasa, na baada ya kuwa soko la maneno yaliyochakaa, kiburi, uzalendo na utaifa, na baada ya mipaka ya bahari na nchi kavu ambayo wakoloni wameiunda imebaki kuwa mada ya toa au pokea ndani ya Lebanon. Hata hivyo, leo hii, makubaliano hayo yamekuwa uhalisia wa aibu kwa wale wanasiasa, vyama na mashirika ambayo yalidai kwa miaka mingi kwamba vita na mapambano yao na Mayahudi ni mapambano ya kihakika! Madai haya yote yaliporomoka! Hivyo basi, tunasema, kwa maneno mafupi, kwa wale wote ambao Ummah unawajua na makosa yao:
Watawala wa Misri, Jordan, Palestina na Morocco wamekutangulieni katika fedheha hii, na hivi karibuni watawala wa Ghuba na Sudan wameungana nao! Matokeo ya hilo yalikuwa nini?
Watawala wa Misri wamehalalisha (mahusiano na umbile la Kiyahudi), lakini watu wa Misri kamwe hawajayahalalisha, na hata kutoka kwao alitoka yule aliyempiga risasi mhaini, ambapo iliufanya Ummah umtukuze Mwenyezi Mungu na kufurahi, na bado anamchukulia aliyefanya kitendo hiki kuwa shujaa wa mashujaa wake. Watawala wa Jordan wamehalalisha mahusiano, lakini watu wa Jordan kamwe hawajayahalisha, na miongoni mwao walikuwapo waliowapiga risasi wanajeshi wa Kiyahudi kwenye mipaka, kwa hivyo Ummah ulikuwa ulijifakhiri naye na ulifurahishwa naye na bado unamwona kuwa shujaa wa mashujaa wake. Viongozi wa lile linaloitwa Shirika la Ukombozi wamehalalisha mahusiano, lakini Waislamu nchini Palestina wangali wanawatesa Mayahudi na wale wafuasi wao, na Umma unaendelea kukua na kufurahia kila kitendo dhidi ya Mayahudi. Watawala wa Morocco wamehalalisha, lakini hisia za watu wa Morocco bado zimejaa chuki kwa Mayahudi, wavamizi. Badala yake, waliipindua serikali ya Haki na Maendeleo nchini Morocco, ambayo inachukuliwa kuwa na "mielekeo ya Kiislamu" katika uchaguzi uliofanyika mnamo tarehe 8/9/2021 wakati ilipogusia kuhalalisha mahusiano na Mayahudi. Hii ni baadhi ya hali ya Ummah kwa walio kutangulieni kwa aibu na fedheha pamoja na Mayahudi, msimamo wa heshima na madhubuti na utabakia, Mwenyezi Mungu akipenda, na hii ndiyo hali ya Waislamu katika Ghuba ya Arabu na Sudan, ambayo ni moto chini ya jivu la dhulma ya watawala vibaraka inayosubiri kulipuka na kuinuka katika nyuso za watawala ili kuiteketeza na kumteketeza kila msaliti wa masuala yake yanayotokana na imani yake.
Basi jueni, enyi mlioketi na kuchora mipaka nchini Lebanon, wanasiasa na vyama, mliojadiliana, mkatia saini, walinyamaza na kutoa baraka, na wakaisifia aibu hii kama makubaliano ya kihistoria! Na kwa hakika mulimpa mali ya watu wa Palestina mvamizi wao! Mulividanganya vitongoji vyenu kwamba uchoraji mipaka hiyo ni kwa faida ya mafuta na gesi ya Lebanon, baada ya kurekebisha sheria ya mafuta ili kumwaga pesa zake kwenye mifukoni mwa kampuni za kibinafsi ambazo nyinyi na wapambe wenu mnazisimamia, na kwenye mifuko ya Amerika na Magharibi! Jueni kwamba watu watiifu na watukufu wa Lebanon kwa jumla, na Waislamu hasa, wanazingatia makubaliano yenu chini ya miguu yao, na hawataacha fursa yoyote bila ya kuonyesha kutoridhika kwao nanyi kwa kila njia na mbinu zinazopatikana.
Ummah unajua kwamba aliyesimamia makubaliano hayo, ziara zake na kiburi chake tangu mwanzo hadi mwisho, ni Marekani, ubalozi wake na balozi wake, ili kuweka mikono yao juu ya mali ya Lebanon, na hata juu ya utajiri wa mashariki mwa Mediterania. Pindi Marekani ilipopata na hilo, iliruhusu walafi miongoni mwa Wazungu kwenda na kuanza uchimbaji!
Na neno kwa watoto wa vyama na mashirika na jamaa zao waliojitolea mhanga katika kupigana na mvamizi, kwani ni suala la Uislamu, na hamu ya kutaka kufa shahidi. Jihadharini musije mukawa miongoni mwa walio radhiwa na kufuatwa, musije mukaachiliwa au kuachwa, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«إِنَّهُ سَيَكُونُ عَلَيْكُمْ أَئِمَّةٌ تَعْرِفُونَ وَتُنْكِرُونَ، فَمَنْ أَنْكَرَ فَقَدْ بَرِئَ، وَمَنْ كَرِهَ فَقَدْ سَلِمَ، وَلَكِنْ مَنْ رَضِيَ وَتَابَعَ...»
“Hakika watakujieni Maimamu (watawala) mnaowapenda (wanayoyafanya) na baadhi ya (wanayoyafanya) mnayo yachukia. Basi mwenye kukataa basi hana hatia, na mwenye kuchukia basi yuko salama. Lakini anayefurahishwa na kufuata...” Washutumuni viongozi wenu waliotii kwa maslahi ya wafuasi na wafadhili, na kumwaga damu ya watoto wenu.
Umma nchini Lebanon na kwingineko uko katika hali ya matumaini, hasa kwa mabadiliko ya kimataifa yanayotokea, kuwashambulia watawala, wakiongozwa na wafanyikazi miongoni mwa watoto wake pamoja na watu wenye nguvu na ulinzi kwa ajili ya kusimamisha dola ya uadilifu na uongofu, Khilafah kwa njia ya Utume, itakayowafanya Mayahudi na kila aliye halalisha mashusiano nao waonje mateso. Na itasafisha uchafu wote wa watawala, vyama na mashirika ambayo yameudanganya Umma kwa miaka mingi.
(وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَن يَكُونَ قَرِيباً)
“Watakutikisia vichwa vyao, na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!” [Al-Isra: 51]
H. 24 Rabi' I 1444
M. : Alhamisi, 20 Oktoba 2022
Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Lebanon