Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ramadhan Inamalizika Lakini Majanga Yanaendelea

Mwezi mtukufu wa Ramadhan unamalizika katika hali ile ile kama ulivyoanza kwa Ummah wa Kiislamu kukosa mtu wa kuwalinda maisha yao wala mali zao. Mwezi mtukufu ulianza huku Waislamu wakiwa wamegawanyika juu ya lini kuanza na kumalizika kufunga katika mandhari hiyo hiyo. Licha ya ari ya Ummah na matarajio yao ya kushuhudia umoja wao, hata katika suala la kuanza na kumalizika mwezi wa Ramadhan. Inasikitisha kuona hili lina salia kuwa vigumu kupatikana. Licha ya ukweli kwamba mwezi mtukufu wa Ramadhan ni mwezi wa Qur'an bado mahusiano kati ya Ramadhan na Qur'an yanabakia tu katika usomaji wa sura nyingi na kuhitimisha Msahafu pasi na hata chembe ndogo ya mazingatio ya mafundisho yake mema au utekelezaji kamili wa uongofu wake katika maisha yetu ya kila siku. Hii sasa ni takribani Ramadhan ya tisini na nne tangu Qur'an iache kutumika kama uongofu kwa wanadamu wote katika kutatua matatizo yao ya maisha ya kila siku.

Tunasherehekea Idd ul-Fitr kwa mavazi ya kuvutia, nguo mpya na kwa aina tofauti za vyakula tukitaraji kuwa kufunga kwetu, taraweh, kusoma Qur'an na Tahajjud zitakubaliwa mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Mbali na hayo, Waislamu katika maeneo mengine kama Palestina, na Syria hawana utulivu katika kutekeleza ibada yoyote. Hususan kaka na dada zetu mjini Gaza, Palestina. Huku Waislamu wengine wakiitafuta Lailat ul-Qadr, kaka na dada zetu kila mahali wanatafuta sehemu za kujificha kutokana na mvua nzito ya mabomu yanayo lipuliwa na Mzayuni muovu. Uovu, ukatili na unyama wa aina hii haujakabiliwa na upinzani wowote kutoka kwa ile inayoitwa dola kuu yenye nguvu, kana kwamba umwagaji huu wa damu tukufu, uangamizaji wa sehemu takatifu hauna uzito. Mtume (saw) asema: «لَزَوَالُ الدُّنْيَا أَهْوَنُ عَلَى اللَّهِ مِنْ قَتْلِ مُؤْمِنٍ بِغَيْرِ حَقٍّ»

"Kuangamia kwa dunia nzima ni sahali mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kumuua Muumini pasi na haki yoyote.". Mauaji haya yanayotekelezwa na Mzayuni yanachukiza ambapo vipande vya nyama za binadamu na vifua vya watoto, wazee na walemavu vimetapakaa kila mahali. Kosa lao nini? 

ENYI! WAISLAMU WETU WATUKUFU 

Wako wapi wanajeshi wenye nguvu wasio shindika katika biladi za Kiislamu kama Misri, Saudi Arabia, Pakistan, Iran na kwingineko? Je, hakuna yeyote kati yao anayeona aibu kuzembea kwake katika majukumu ya Kiislamu ambaye moyo wake waweza kutingishwa na hivyo kumpelekea kutekeleza jukumu lake la Kiislamu na hatimaye asifiwe katika maisha haya na akhera na kuyafanya maregeo kwa Mola wao kuwa ya furaha?!  

Wako wapi watawala katika maeneo haya, ni kitu gani kinachowazuia na kuwachelewesha katika kuharakisha kupeleka majeshi na kuwalinda kaka na dada zao wanyonge wanao dhulumiwa? Hakuna hata mshipa mmoja wa ghera na matarajio katika nyoyo zao baridi zenye kuona damu tukufu ya kaka na dada zao ikimwagwa na watu duni, wachafu walio laaniwa ambao mababu zao ni matumbili na masokwe?!

Mpaka lini watawala vibaraka katika biladi zetu za Kiislamu watapanga njama na kunyamaza kimya juu ya vitendo hivi viovu vya kinyama na vya dhulma vinavyo wakumba kaka na dada zao, huku kimya kimya wakijificha nyuma ya pazia za kuwaombea dua majeruhi, mayatima na wajane pasi na kuchukua hata hatua moja muhimu ya maana? Je, vibaraka hawa hawajui kuwa Mtume Mtukufu (saw) alikuwa akizinyoosha safu za wanajeshi na kuwatayarisha kwa mapambano na halafu ndio akimuomba Mwenyezi Mungu (swt) ushindi … kwa vitendo kama hivyo ndivyo watawala na watu wanapaswa kuvifanyiakazi, sio kuyazuia majeshi kutotoa msaada kwa watu wa Gaza na kuwaombea tu pekee! Mpaka lini Ummah hautazungumza dhidi ya watawala hao na kufanya kazi kuleta mabadiliko halisi yatakayo simamisha ngao ambayo itawalinda na kuwatetea kaka zetu na dada zetu mjini Gaza na ardhi nyingine za Waislamu.  

ENYI! WAISLAMU WETU WATUKUFU 

Tuna sherehekea Idd ul-Fitr huku eneo la Afrika Mashariki kukiwa na tishio la vita dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa kisingizio cha vita dhidi ya ugaidi huku uhalisia ukiwa Waislamu ndio walengwa pekee. Amerika inasonga mbele kupitia serikali vibaraka kuunda Vikosi Maalumu vya kupigana na Waislamu na Uislamu chini ya usimamizi wa Amerika na ufadhili kamili wa kifedha, kimafunzo na pasi na kuingiliwakati na serikali hizo. Vikosi Maalumu kama kitengo cha polisi wa kupambana na ugaidi (ATPU) cha Kenya na mfano wake nchini Tanzania vimekuwa ndio nembo ya uvunjaji sheria zao wenyewe ili kutekeleza unyama, mateso, kuingilia faragha, uvamizi wa usiku, kufukuzwa nchi kisiri, udhalilishaji wa wanawake wa Waislamu kama yaliyotokea mjini MWANZA hivi majuzi. Vikosi hivi Maalumu vinatekeleza vitendo vya kinyama katika hali ya jeuri na kiburi kikubwa mno, mbali na rundo la tuhma kuhusiana na mauaji ya wanaharakati wa Waislamu wasio na hatia na ulipuaji mabomu katika jaribio la kuhalalisha malengo ya kijeshi na kisiasa ya mfadhili wao. Kumekuweko na mauaji na ukamataji wa kiholela wa Waislamu katika miji tofauti nchini Kenya, Zanzibar, Arusha, Mwanza pamoja na udhalilishaji mkubwa mno wa hata wanawake na watoto. Waislamu katika nchi hizi huchukuliwa kama raia wa tabaka la pili wanaostahili kudhulumiwa licha ya mchango wao mkubwa na mababu zao nchini humu.

Eneo la Afrika Mashariki linakumbwa na mivutano ya kisiasa na vita kati ya Amerika na nchi za Ulaya zote zikipigania kuwa na ushawishi katika eneo hili. Hii ni kutokana na kugunduliwa kwa rasilimali asili nyingi katika eneo hili. Mafuta, Gesi, na rasilimali nyingine asili kama dhahabu, almasi, urani, nk. bila ya kutaja umuhimu wa kimikakati wa eneo hili ikiwemo Bahari Hindi kubwa ambayo ni muhimu kiuchumi na kiusalama. Juu ya hili, eneo hili linapakana na biladi muhimu za Kiislamu katika bara Arabu, Sudan, Somalia, nk. yote haya yanaongeza thamani ya eneo hili machoni mwa nchi za kirasilimali kufikia hadi kuwa tayari kusababisha ghasia, machafuko na vita vya wenyewe kwa wenyewe ili kufikia lengo lao yaani kutawala na kufyonza rasilimali asili kutoka eneo hili. 

Hilo daima hupelekea utovu wa usalama na hofu miongoni mwa wakaazi wake. Hofu na vitisho vimetanda juu ya Waislamu nchini Kenya kufuatia vifo visivyostahiki katika sehemu zilizo na Waislamu wengi katika maeneo ya Pwani na Kaskazini Mashariki. Vifo hivi vya kikatili vimesababisha machafuko, hofu na uoga miongoni mwa wakaazi wa eneo zima la Pwani kuanzia Mpeketoni, Poromoko, Hindi likipanuka hadi Witu.

Cha kushangaza zaidi, yote haya yanatokea na ilhali kuna kambi za kijeshi za Wanajeshi wa majini wa Kenya na Amerika, lakini wahalifu wakatekeleza uovu wao kwa zaidi ya saa kumi bila ya kusumbuliwa. Natija yake, utovu wa usalama umepenya sehemu nyingine kama Malindi na Mombasa huku ujambazi na mauaji yakiripotiwa kila siku. Swali ni je, ni kwani haya yote yamekuwa yakitokea hivi karibuni? Kwani ni zaidi ya mwaka sasa tangu matukio haya ya kinyama kuyakumba maeneo haya yaliyo na Waislamu wengi ambayo awali yalikuwa tulivu. Bila shaka, yeyote aliye na upeo mpana atahisi kuwa Uislamu na Waislamu ndio walengwa ili kuwaangamiza na pindi mauaji yoyote yanapofanywa inakuwa ni rahisi kubandika lawama juu yao.   

ENYI WAISLAMU WETU WATUKUFU!

Lolote linalotokea ulimwenguni na haswa ndani ya Afrika Mashariki, ni dhihirisho wazi la haja kubwa ya Ummah kuwa na mlinzi na msimamizi atakaye wachunga dhidi ya maovu haya. Msimamizi ambaye atayaunganisha majeshi yote ya Waislamu kwa pamoja dhidi ya maadui wao, huyu si mwengine ila ni Khalifah kama alivyoeleza Mtume (saw),

 «إنما الإمام جُنّة، يقاتل من ورائه ويتقى به» "Hakika Kiongozi (Imamu) ni ngao watu hupigana na hujilinda nyuma yake."

Licha ya maovu yote kufanywa dhidi yetu, kila usiku unapokucha unaashiria kukaribia kwa alfajiri ya ushindi. Huu pasi na shaka ni ukweli wa bishara njema ya Mtume ya kusimama tena kwa Khilafah ya Uongofu iliyo na nguvu na imara. Kinyume na Khilafah bandia iliyo tangazwa hivi majuzi ili kuwakanganya Waislamu, kuwalinda makafiri, kuuchafulia jina Uislamu, huku ikiwa haina alama halisi za dola kwa mujibu wa hukmu za Uislamu!  

Mwisho, Hizb ut Tahrir Afrika Mashariki inawalingania kwa ikhlasi Waislamu kubeba jukumu la kufanya kazi pamoja nao katika safari ya kusimamisha tena Khilafah ya Uongofu iliyo tabiriwa kwa wahyi na Mtume wetu Muhammad (saw).

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kupitia amali zetu njema tulizo zikusanya katika masiku haya ya mwezi huu mtukufu kwa lengo la kujikurubisha kwake (swt) ili aturuzuku ushindi wa haraka kupitia kusimama kwa Khilafah kwa njia ya Utume na kuturudishia ngao itakayo tulinda na kutuwezesha kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu kama anavyostahiki kuabudiwa bila ya uoga. Kwa heshima na taadhima, tunawatakieni nyote Idd Mubarak katika siku hii muhimu kama alivyoichagua Mwenyezi Mungu Mtukufu Muumba wa ardhi na mbingu.

www.hizb.info.com
www.hizb-eastafrica.com

H. 1 Shawwal 1435
M. : Jumatatu, 28 Julai 2014

Hizb-ut-Tahrir
Afrika Mashariki

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu