Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ajenda na Genge la (LGBTQ) ni Matunda Mabovu ya Mfumo Muovu wa Kirasilimali

Januari 6 mwaka huu mwili wa Edwin Chiloba mwenye umri wa miaka 24 mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Eldoret, ulipatikana ndani ya sanduku ukiwa umeshindiliwa vitambara mdomoni na puani mwake. Kifo chake kimezuwa gumzo ndani na nje ya nchi haswa katika vyombo vya habari na katika mitandao ya kijamii kwa sababu Chiloba ni mtetezi wa LGBTQ+ (usago, ukhanithi…). Msemaji wa wizara ya kigeni ya Amerika Ned Price alitangaza tarehe 10 kuwa serikali ya Biden itatoa usaidizi kwa serikali ya Kenya kuchunguza mauaji hayo kwa kisingizio cha ukiukaji wa haki za kibanaadamu.

Ndani ya mwavuli wa haki za Kibinadamu, Wakoloni wamagharibi wanaeneza uchafu wa usago, ubasha na uhanithi LGBT (Lesbian Gay Bisexual Transgender). Marekani, nchi iliyohalalisha  ufuska wa ndoa za jinsia moja mwaka 1999, kulifanyika maandamano  mwaka 1965-66 ya jamii ya mashoga wakitaka kutobaguliwa kama raia wa daraja la pili na hii ni baada yao wao kuzusha rabsha na polisi huko Stonewall. Mwongo mmoja uliopita Baraza la kimataifa la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa likapitisha rasmi azimio lake la kutambua rasmi "haki" za LGBT. Nalo shirika la Amnesty International linashikilia msimamo huo sambamba na miungano ya mawakili katika mataifa mbalimbali duniani iko kifua mbele kutetea uovu huu.

Kufikia Novemba mwaka jana tayari Mataifa 30 yamehalalisha rasmi uovu huu unaongamiza vizazi. Bara la Afrika ambapo hadi sasa mataifa mengi yake hayajatambua ama kuhalalisha LGBT, ukiachilia mbali Afrika Kusini, lipo katika shinikizo la mataifa makubwa ya kibepari yanayotumia njia za kiuchumi, kisiasa na hata kijamii kulazimisha uchafu huu. Kwa masikitiko makubwa mashirika kama vile USAID na DANIDA yanayotumika kueneza maovu haya yamepewa ruhusa kufanya kazi katika nchini nyingi barani chini ya kisingizio cha kutoa misaada. Filamu za LGBT zinapeperushwa kama ile ya iliyopigwa marufuku nchini Kenya “I am Samuel’ iliyozinduliwa mwaka 2020.

Kukuza na kushajiishwa kwa hulka hii mbovu kunatokana na ufahamu wao wa kipotofu na mawazo yao ya kihuria/uhuru (liberal views) kwamba kukidhi matamanio ya kimwili ndiko kufaako kupewa kipaumbele zaidi hata kuliko kuendeleza kizazi. Kwa kile wakiitacho uhuru wa kibinafsi, jamii zao huruhusiwa kufanya kitendo chochote kile maadam kitafikia kwenye raha. Na ni kwa muktadha huu ndio tumefikishwa hapa ndoa za masago na mabasha! Ni wazi kuwa haki za LGBT zinalindwa na mfumo muovu wa Kimagharibi.

Enyi Waislamu: Tambueni kwamba wakoloni wa Kimagharibi wamekwisha angamiza kizazi chao na sasa wamo mbioni kuhujumu familia zenu kuzifanya kama wanyama bali zaidi ya wanyama! Kampeni ya LGBT inalenga mmomonyoko wa kimaadili na kukatisha mahusiano mazuri katika wanaume na wanawake. Kejeli nyingi mtafanyiwa na Wamagharibi kwa sababu ati nyinyi mnabeba msimamo wa kwamba ndoa pekee inayotambulika kisheria ni baina ya mwanamume na Mwanamke wala sio mashoga au masago! Hata hivyo, mtasimangwa na kukejeliwa na Wamagharibi na makundi yao kama harakati za wanawake (Feminists). Lengo la kejeli na masimango haya dhidi yenu ni nyinyi muanze kuyakubali machafu haya au kwa uchache mkubali na kutambua haki zao’. Na sio ajabu pia mkapachikwa majina ya ugaidi na misimamo mikali kwa sababu ya kupinga maovu haya.

Waenezaji uchafu huu hata wakiambiwa; “Acheni kuleta uharibifu katika jamii”, majibu yao ni kama alivyosema Mwenyezi Mungu (swt) “Laa bali sisi ni watengenezaji mambo!” Na wakiambiwa muogopeni Mwenyezi Mungu kwa kukomeka na madhambi haya kwa inadi wao wanaendelea kuhimiza watu kufanya machafu hayo. Wakoloni wanajua vyema kwamba nyinyi munachukizwa na machafu haya na kwa nini msichukizwe ilhali munatambua vyema Jinsi Mwenyezi Mungu (swt) alivyoangamiza watu wa Nabii Lut (as):

(فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا جَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهَا حِجَارَةً مِنْ سِجِّيلٍ مَنْضُودٍ)

“Basi ilipofika amri Yetu, Tukaifanya juu yake kuwa chini yake, na Tukawapigia mvua ya changarawe za udongo mgumu zipandanazo.” [11:82].

Enyi Wanaume wa Kiislamu: Nyinyi ndio wasimamizi wa familia zenu (wake zenu na watoto wenu) asema Mwenyezi Mungu (swt):

(ٱلرِّجَالُ قَوَّٰمُونَ عَلَى ٱلنِّسَآءِ بِمَا فَضَّلَ ٱللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَآ أَنفَقُوا۟ مِنْ أَمْوَٰلِهِمْ ۚ فَٱلصَّٰلِحَٰتُ قَٰنِتَٰتٌ حَٰفِظَٰتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ ٱللَّهُ)

“Wanaume ni Walinzi wa Wanawake kwa sababu Mwenyezi Mungu amewafadhili baadhi yao kuliko wengine, na kwa sababu ya Mali zao walizozitoa basi wanawake wema ni wale wenye kutii wanaohifadhi (hata) wasipokuwapo waume zao yale Aliyoyahifadhi Mwenyezi Mungu.” [4:34]

Usimamizi huu sio udikteta juu ya familia zenu bali ni usimamizi wa kimajukumu ili kuhakikisha kiwango cha juu cha kimaadili bali mshikamano thabiti baina ya wanafamalia. Usimamizi huu uko ndani ya Uislamu pekee wala haupatikani ndani ya mfumo batili wa Kimagharibi wa Kibepari uliomfanya mwanadamu afukuzane na matamanio yake kama mnyama hivyo kuhujumu mahusiano baina ya wanaume na wanawake. Natija ya mfumo huu ni kuziona familia zilizo paraganyika kukiwa hakuna huruma ya baba kwa mwanawe huku mwana kutomhurumia babake, mke kutoheshimu mumewe na mume kutoheshimu mkewe!

Enyi Waislamu: Tunawajibika kupaza sauti zetu katika kupinga matendo haya maovu, kufafanua umuhimu wa taasisi ya ndoa zetu, mahusiano baina ya wanaume na wanawake yote kwa mtazamo wa mfumo wetu wa Uislamu. Tuungane na Hizb ut Tahrir harakati ya Kiislamu inayofanya kazi ya kuhuisha maisha mema ya Kiislamu kupitia kusimamisha dola ya Khilafah kwa njia ya Utume katika mojawapo ya nchi za Waislamu. Dola hii ndio itakayolinda jamii kikamilifu dhidi ya maovu yote.

(يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱسْتَجِيبُواْ لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ)

“Enyi Mlioamini Muitikieni MwenyeziMungu na Mtume wake anapokutieni katika yale yatakayokupeni uhai mzuri wa duniani na Akhera.” [8:24].

H. 19 Rajab 1444
M. : Ijumaa, 10 Februari 2023

Hizb-ut-Tahrir
Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu