Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wito kwa Waislamu kwa Jumla, na kwa Watu wa Ash-Sham Hasa
(Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake, na maswahaba zake, na wanaomfuata.

Mumejifunza kuhusu matukio yaliyoharakishwa huko Ash-Sham, na hatima ya Bashar, dhalimu wa Ash-Sham, ambaye amekuwa mtu wa kufukuzwa na mkimbizi tangu tarehe 8 Disemba 2024. Mumeona kile ambacho kimekuwa dhahiri juu ya udhalimu wake juu na chini, na jinai za aibu waliyotendwa wafungwa, hata hayawani ardhini hawajatenda chochote kama hayo. Kisha mukatazama jinsi watu walivyosherehekea kuangamia kwa dhalimu mijini, vijijini na mabarabarani, wakimshukuru Mwenyezi Mungu (swt) kwa kuwapa ushindi kwa kuondosha utawala wa dhalimu huyo.

Kisha mumeona na kusikia jinsi Amerika, ikifuatiwa na Uturuki, ilivyowakusanya watawala wa Kiarabu huko Aqaba kujadili jinsi serikali mpya ya Syria inapaswa kuwa: [Wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano ya Mawaziri wa Kiarabu walikutana leo, Jumamosi, katika mji wa Jordan wa Aqaba kuhusiana na matukio ya Syria... Uturuki... Marekani... Mwakilishi Mkuu wa Muungano wa Ulaya... na mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria.] Taarifa hiyo ilisomeka hivi: (Mikutano hiyo ilijadili njia za kuunga mkono mchakato wa kisiasa wa kina ukiongozwa na Syria “ili kufanikisha mchakato wa mpito kwa mujibu wa Azimio 2254 la Baraza la Usalama...”). Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Geir Pedersen alisema wakati wa mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken, kando ya mikutano ya Aqaba [“tunatarajia kuona dola ya Syria ikijitokeza, kama yenye uwakilishi kamili, isiyo ya kimadhehebu, inayojumuisha watu wote, ambayo inaweza kuleta pamoja sehemu zote za jamii ya Syria” (Al Jazeera, 14/12/2024)]. Baada ya hapo, gazeti rasmi la “Uturuki” lilisema [kwamba Erdogan anaweza kufanya ziara ya “kihistoria” jijini Damascus ndani ya wiki mbili zijazo. Alithibitisha wakati wa mazungumzo yake na waandishi wa habari kwamba nchi yake “itasaidia utawala mpya wa Syria katika kujenga muundo wa serikali”. Aliongeza kuwa anatumai kuwa kuundwa utawala mpya wa Syria unaoongozwa na al-Julani kutapelekea kiwango kipya cha uhusiano wa pande mbili. (Sky News Arabia, 20/12/2024)].

Kisha, wajumbe wa Marekani na Ulaya walikuja Syria katika mikutano na serikali mpya ili kupanga hali hiyo kwa namna ambayo wajumbe hao wanaitaka. Wa mwisho wao, mnamo Ijumaa 20/12/2024, alikuwa ujumbe wa Amerika. Mwishoni mwa mkutano huo, Idara ya Operesheni za Kijeshi nchini Syria ilitoa taarifa kuhusu nukta muhimu zaidi ambazo zilijumuishwa katika mkutano wa kiongozi wake, Ahmed Al-Sharaa pamoja na ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ambao ulisema: [Upande wa Marekani ulithibitisha dhamira yake ya kuunga mkono watu wa Syria na utawala mpya wa Syria, na kusimama nao katika kukabiliana na faili zinazosubiriwa na changamoto kubwa, kama vile eneo la kaskazini mashariki mwa Syria, na wajumbe walielezea kuunga mkono hatua zilizotangazwa na utawala mpya wa Syria... Taarifa hiyo iliongeza: “Kwa upande wake, wajumbe walitoa shukrani zao kwa juhudi za utawala mpya katika kuwaachilia huru wafungwa, akiwemo Raia wa Marekani Travis... Taarifa hiyo iliendelea: “Kwa upande mwengine, upande wa Syria ulitoa makaribisho yake kwa ujumbe huo... na kueleza kuwa watu wa Syria wanahitaji msaada mkubwa ili kufikia afueni na ustawi katika ngazi zote, ukitoa wito wa kuondolewa vikwazo vilivyowekwa dhidi yake, na kueleza kuwa watu wa Syria wanasimama kwenye masafa yale yale kutoka kwa nchi na pande zote katika kanda hii bila kuiweka Syria katika hali ya mgawanyiko” (Arabic RT - Arab World News, 20/12/2024)].

Kisha mumeona na kusikia jinsi jeshi la Mayahudi lilivyovamia vijiji vya Golan na Quneitra, na kufanya mashambulizi takriban 600 yakilenga maeneo ya jeshi la Syria, hasa vituo vya anga na mifumo ya ulinzi wa anga, katika operesheni kubwa zaidi ya kuharibu uwezo na zana za kijeshi katika historia ya kisasa, kama ilivyoelezwa kwenye tovuti ya Sky News Arabia tarehe 19/12/2024. Mashambulizi yake yaliendelea ndani ya eneo lisilo na wanajeshi hadi ikafika Mlima Hermon: [“Majeshi ya Israel yalikalia Mlima Hermon walipoingia kwenye eneo lisilo na jeshi kati ya Syria na Milima ya Golan iliyokaliwa kwa mabavu.” (Al Jazeera, 18/12/2024)]. Hivyo basi, baada ya umbile la Kiyahudi kufanya mamia ya mashambulizi dhidi ya vituo vya kijeshi, kiusalama na kisayansi nchini Syria, mbele ya macho ya watawala wapya wa Syria, watawala wa Waarabu na watawala wa nchi za Waislamu... kana kwamba jambo hilo haliwahusu! Kilicho kibaya zaidi na cha uchungu zaidi ni kwamba serikali mpya ya Syria inatangaza, pamoja na hayo yote, kwamba haikusudii kuwa na mgogoro na umbile la Kiyahudi, wala na Marekani na Ulaya, na kwamba wanaomba amani na kuondolewa kwa vikwazo juu yao, na kusaidiwa katika ujenzi na ujenzi upya... maombi ambayo ni zaidi ya udhalilifu na fedheha:

Asharq Al-Awsat ilichapishwa kwenye tovuti yake tarehe 15/12/2024: [...Ahmed Al-Sharaa alisema mnamo Jumamosi kwamba 'Israel' inatumia visingizio vidogo kuhalalisha mashambulizi yake dhidi ya Syria, lakini aliweka wazi kwamba yeye hana nia ya kuingia katika migogoro mipya, kwani nchi hiyo inaangazia kujijenga upya baada ya kumalizika kwa enzi ya Bashar Al-Assad... Alisisitiza kuwa masuluhisho ya kidiplomasia ndiyo njia pekee ya kuhakikisha usalama na utulivu “mbali na matukio yoyote ya kijeshi yasiyopigiwa hesabu”]. Al-Jazeera imenukuu gazeti la ‘New York Times’ [Al-Sharaa alizitaka serikali kama vile Marekani kuondoa kibandiko cha kigaidi kutoka kwa Hay'at Tahrir Al-Sham, na pia ametaka kuondolewa vikwazo vyote ili Wasyria waweze kuijenga upya nchi.” (Al-Jazeera, 17/12/2024).

Enyi Waislamu kwa jumla, na hasa watu wa Ash-Sham: Utawala mpya wa Syria, unaoongozwa na al-Julani, una uhusiano wa karibu na utawala wa Uturuki unaozunguka katika mzunguko wa Amerika. Ikiwa anadhani kwamba kwa kuifurahisha Marekani, atatabikisha utawala wa kisekula, ataipiga vita Khilafah na walinganiaji wake, na kufunga jela juu yao, ingawa alifungua jela nyengine na kuwaachia huru wote waliomo isipokuwa wanachama wa Hizb ut Tahrir wanaofanya kazi kurudisha utawala wa Mwenyezi Mungu duniani, Khilafah Rashida, na hilo ni ili kuifurahisha Marekani na Magharibi katika vita vyao dhidi ya Khilafah na watu wake. Akiwa anadhania kuwa hili litahifadhi kiti chake (cha utawala), basi amekosea isipokuwa ataendelea kuwatumikia, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitufahamisha kupotea kwa mwenye rai hii, kwani yeye (saw) amesema katika yale aliyoyapokea Ibn Hibban katika Sahih yake kutoka kwa al-Qasim kutoka kwa Aisha, Mama wa Waumini, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«مَنْ أَرْضَى اللهَ بِسَخَطِ النَّاسِ كَفَاهُ اللهُ، وَمَنْ أَسْخَطَ اللهَ بِرِضَا النَّاسِ وَكَلَهُ اللهُ إِلَى النَّاسِ»

“Yeyote anayetaka radhi za Mwenyezi Mungu kwa ghadhabu za watu, Mwenyezi Mungu atamtosheleza kwa watu. Na yeyote anayetaka radhi za watu kwa ghadhabu za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamkabidhi kwa watu.”

Yeyote anayeangalia hatima ya wafuasi wa wakoloni makafiri na wale wanaofuata nyayo zao ili kuwafurahisha ataona kwamba hali zao zinazungumza wazi juu ya hatima yao:

[إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَنْ كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ]

“Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.” [Qaf: 37].

Enyi Waislamu kwa jumla na hasa watu wa Ash-Sham: Mfumo pekee alioufanya Mwenyezi Mungu (swt) kuwa ni faradhi na Mtume wake (saw) na Makhalifa waongofu wakautabikisha, ni kuhukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, safi na ya wazi, pasi na dosari yoyote, na bila mfumo mwengine kuchanganywa ndani yake. Kwa hiyo wema hauchanganywi na uovu, na sehemu za Uislamu na sehemu za usekula hazitabikishwa (pamoja). Bali utawala ni kwa mfumo wa Khilafah Rashida bila ya mgawanyiko.

[وَأَنِ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَنْ يَفْتِنُوكَ عَنْ بَعْضِ مَا أَنْزَلَ اللهُ إِلَيْكَ فَإِنْ تَوَلَّوْا فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللهُ أَنْ يُصِيبَهُمْ بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ..]

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao …” [Al-Ma’idah: 49]

Mumejitolea muhanga, mumedhurika, wengi wenu wameuawa shahidi na wengi wamejeruhiwa. Mihanga hii lazima iwe ya kusimamisha utawala wa Mwenyezi Mungu (swt) duniani, Khilafah Rashida, na sio kubadilisha serikali moja ya kisekula kwa nyengine, hata kama jina na anwani vinatofautiana. Hivyo, mihanga yenu itakuwa nuru inayomulika Ash-Sham. Walakini, ikiwa mihanga hii itakuongozeni kubadilisha mfumo mmoja ulioundwa na mwanadamu na kuweka mfumo mwengine ulioundwa na mwanadamu, basi mutakuwa mithili ya yule anayefungua uzi wake uliosokotwa baada ya kuwa na nguvu:

[وَلَا تَكُونُوا كَالَّتِي نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِنْ بَعْدِ قُوَّةٍ أَنْكَاثاً..]

“Wala msiwe kama mwanamke anaye uzongoa uzi wake baada ya kwisha usokota ukawa mgumu.” [An-Nahl: 92]

Enyi Waislamu kwa jumla, na watu wa Ash-Sham hasa: Kiongozi wa Hizb ut Tahrir, asiyewadanganya watu wake, anakuonyeni juu ya mikono ya mashetani wa wanadamu wanaotaka damu yenu imwagike bure, ili msifikie wema msafi na dhahiri, kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, bali hukmu iliyotungwa na mwanadamu lakini yenye jina na maana tofauti. Badala ya kuwa Umma ambao makafiri wanauchukulia kwa uzito, mumerudi kuwa wafuasi wa makafiri wakoloni na vibaraka wao, na huu ni uhalifu, Mwenyezi Mungu aepushie mbali, ambao hatima yake ni udhalilifu duniani na adhabu kali kesho Akhera.

[سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ]

“Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya.” [Al-An’am: 124]

Jihadharini msiipoteze mihanga yenu, hasa kwa vile Ash-Sham lazima iwe ndio kitovu cha nyumba ya Uislamu, kama alivyotufahamisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika Hadithi ambayo At-Tabarani ameipokea katika Al-Mu'jam Al-Kabir kutoka kwa Salamah bin Nufayl, ambaye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «عُقْرُ دَارِ الْإِسْلَامِ بِالشَّامِ» “Kitovu cha nyumba ya Uislamu ni Ash-Sham.”

Kwa hivyo fanyeni kila muwezalo kuzuia masuluhisho mabovu ya kisiasa ya kisekula ambayo wakoloni makafiri na vibaraka wao wanataka. Msiruhusu mihanga yenu katika matukio haya ipotee bure na kubakia alama tu! Na iungeni mkono Hizb ut Tahrir, inayofanya kazi ya kusimamisha utawala wa Uislamu, Khilafah Rashida, na mtapata malipo makubwa na ushindi mkubwa, Mwenyezi Mungu akipenda. Kisha mutakuwa miongoni mwa wanaostahiki bishara njema:

[نَصْرٌ مِنَ اللهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ]

“Nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!” [As-Saf: 13]

H. 19 Jumada II 1446
M. : Jumamosi, 21 Disemba 2024

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu