بسم الله الرحمن الرحيم
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Tajikistan Yaomboleza kwa Huzuni Kubwa Mbebaji Dawah Ustadh Ismail Dadobov
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Tajikistan inaomboleza kwa masikitiko makubwa kuondokewa na mbebaji ulinganizi mwenye ikhlasi Ismail Dadobov, aliyeaga dunia kwenda kwenye rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu mnamo siku ya Ijumaa, 17 Muharram 1445 H, sawia na 4 Agosti 2023 M, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Ndugu yetu Ismail alizaliwa huko Khojand, Tajikistan, mwaka wa 1972. Ameacha watoto sita, macho yao yakibubujikwa na machozi.
Ndugu yetu Ismail alikuwa miongoni mwa wale walioonyesha kujitolea kusikoyumba katika Dawah ndani ya safu za Hizb ut Tahrir, akisimama dhidi ya dhulma ya madhalimu bila ya kuogopa lawama ya mwenye kulaumu isipokuwa Mwenyezi Mungu.
Aliwekwa kizuizini mara mbili na akatumia miaka kumi na minane ya maisha yake katika jela ya madhalimu. Ingawa dhulma ya jela iliathiri afya yake, haikuweza kuvunja azma yake katika kufuata Dawah!
Ismail alisimama kishujaa dhidi ya dhulma na alibaki imara kwenye haki. Pamoja na dhulma zote alizokumbana nazo gerezani na chuki za madhalimu, hazikumzuia kuendelea na Dawah yake. Kinyume chake, alipata nguvu na ujasiri wa kufanya kazi kuelekea kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Ndugu yetu aliendelea na Dawah yake katika safu za Hizb baada ya kutoka jela mwaka wa 2019. Alifanya kazi bila kuchoka kwa ajili ya kusimamisha Khilafa Rashidah kwa njia ya Utume hadi alipofariki.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amfinike kwa rehema zake Pana na ampe makaazi katika mabustani yake makubwa pamoja na Manabii, watu wa kweli, mashahidi na watu wema, na hao ndio maswahaba watukufu. Pia tunamuomba awape subira, faraja, na maliwazo mema familia yake na wapendwa wake. Tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa familia yake. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amsamehe ndugu yetu Ismail na amkubalie mema yake.
Licha ya uzito wa kumpoteza ndugu yetu, tunasema tu yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu.
[إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea..” [Al-Baqara: 156]
H. 18 Muharram 1445
M. : Jumamosi, 05 Agosti 2023
Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Tajikistan