Ijumaa, 01 Safar 1442 | 2020/09/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kufanya Hima Juu ya Sharia Huvunja Fikra ya Kuchelewesha Mambo

Tuko katikati ya mwezi mtukufu wa Ramadhan. Kama Waislamu, tunafahamu baraka na malipo yanayo ambatana na mwezi huu mtukufu.

«مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ»

“Anayefunga Ramadhan hali ya kuwa na imani na matumaini ya malipo (kwa Mwenyezi Mungu), hufutiwa dhambi zake zilizo tangulia.” (Imepokewa na Bukhari, Imani, na. 37)

«كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ يُضَاعَفُ الْحَسَنَةُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا إِلَى سَبْعمِائَة ضِعْفٍ قَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ إِلَّا الصَّوْمَ فَإِنَّهُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ يَدَعُ شَهْوَتَهُ وَطَعَامَهُ مِنْ أَجْلِي لِلصَّائِمِ فَرْحَتَانِ فَرْحَةٌ عِنْدَ فِطْرِهِ وَفَرْحَةٌ عِنْدَ لِقَاءِ رَبِّهِ وَلَخُلُوفُ فِيهِ أَطْيَبُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ رِيحِ الْمِسْكِ»

“Kila tendo la mwanaadamu huongezewa thawabu mara kumi yake hadi mara mia saba. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, ‘isipokuwa swaum, kwani hiyo ni yangu Nami Ndiye mlipaji, amewacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili yangu.’ Mfungaji anafuraha mbili, furaha ya wakati anapo futuru na furaha ya wakati anapo kutana na Mola wake, na harufu inayotoka mdomoni mwa mfungaji ni nzuri zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko harufu ya miski.” (Al-Bukhari)

Katika kutumainia kunufaika na malipo, tunafanya hima kutenda matendo yenye kulipwa. Tunapangilia ratiba zetu kuhakikisha kuwa tunasoma Quran, kusali na kutoa sadaka, yote hayo kwa matumaini ya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu (swt).

Kote katika ulimwengu wa Kiislamu, sote tumekuwa tukionyesha kuwajibika kukubwa kwa upande wa kupata malipo ya matendo ya kibinafsi. Hatuyaakhirishi kwa saa moja mbele au siku inayofuata. Lakini tunapaswa kukumbuka kuwa Uislamu ni zaidi ya matendo ya mtu mmoja mmoja. Unatupatia sisi nidhamu kamili ya sheria zinazo ongoza matendo ya kila mmoja wetu. Nidhamu ya sheria zinazo hitaji kutekelezwa kwa kiwango cha serikali.

Tunapo angalia, pote katika mazingira yetu, kile ambacho tunakikosa, ni kuwa tunakosa serikali ya Kiislamu ambayo hutawala kwa mujibu wa Sharia. Hivyo, inatuangukia sisi, kama Ummah wa Mtume Muhammad (saw), kufanya jitihada katika kuisimamisha tena Serikali ya Kiislamu.

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإِسْلاَمَ دِينًا

“Leo nimekukamilishieni Dini yenu na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndio Dini.”  (TMQ 5:4)

Mara baada ya aya hii kuteremshwa, Uislamu ukawa umekamilika na tukawa tunategemewa kuutekeleza katika kila nyanja ya maisha yetu.

Ni hapa ndipo tumekuwa tukisita sita kwenye matendo yahusianayo na mu’amalat – hukumu zenye kuhusika na mahusiano baina ya watu katika jamii. Ni hapa ndipo tunapo ruhusu wenyewe kupotea katika shughuli zetu za kawaida – (kwamba) nitafanya kesho. Tunapotea kwa kuamini kuwa hatuwezi kufanya chochote katika kuleta mabadiliko. Kuibadilisha jamii ni jambo lililo juu ya uwezo wetu – tutauachia uongozi na wanasiasa wasimamie. Viongozi hao hao ambao watatoka nje ya njia yao kwa kufanya kazi ndani ya mfumo usio wa Kiislamu na kunufaika kupitia mateso na matatizo ya wengine.

Mazingira ya ulimwengu yamezusha hali ya kutufanya tuwe nyumbani. Tumekuwa na fursa ya kupotea katika shughuli zetu za kawaida na kusitasita. Au tunaweza kutumia muda huu kuzingatia uhalisia tunaoishi nao. Hatupaswi tu kufikiria, lakini tunapaswa kutenda.

Tupo katika kipindi muhimu katika historia, ambapo dunia iko katika mabadiliko ambayo maambukizi yanayaleta na namna ambavyo mabadiliko haya yataiweka dunia.

Hii inatupa fursa ya kuzingatia namna tunavyo weza kuiunda dunia. Hivyo kwa nini hatuutumii mwezi huu kufanya kazi kuelekea katika mabadiliko ambayo tungependa kuyaona na kupata malipo ambayo Mwenyezi Mungu ametuahidi?

Tunahitaji kuwa na angazo hilo hilo la ibada juu ya matendo mengine – Uislamu ni zaidi ya ibada za mtu mmoja mmoja, ni itikadi ambayo inaongoza kwenye mazingira yetu ya kisiasa na ya kijamii na kiuchumi.

Kutoa sadaka ni tendo la thawabu, na ni moja ya jambo ambalo kila Muislamu hukimbilia kulikamilisha. Lakini kama Waislamu ambao wanafahamu kuwa majukumu yetu yanakwenda zaidi ya matendo ya kibinafsi, tuufanye muda huu kuwa ni fursa ya kuzizingatia dhurufu zilizo leta utafauti na ugumu ulioenea.

Usiiwache hadi siku inayofuata, usifanye chaguo la makusudi au lisilo la makusudi kuchelewesha matendo yetu.

Hatujui kama tutaishi kuiona siku inayofuata.

Kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyo sema katika Quran,

وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ

“Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho. Wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani.” (TMQ 31:34)

Na Mtume (saw) amesema katika hadith,

«كُنْ فِي الدُّنْيَا كَأَنَّكَ غَرِيبٌ أَوْ عَابِرُ سَبِيلٍ»

“Kuwa katika dunia kama kwamba ni mgeni au mpita njia”

Ibn Umar alikuwa akisema,

«إِذَا أَمْسَيْتَ فَلَا تَنْتَظِرْ الصَّبَاحَ وَإِذَا أَصْبَحْتَ فَلَا تَنْتَظِرْ الْمَسَاءَ وَخُذْ مِنْ صِحَّتِكَ لِمَرَضِكَ وَمِنْ حَيَاتِكَ لِمَوْتِكَ»

“Unapoingiliwa na jioni usiisubiri asubuhi, na unapopambazukiwa asubuhi usiisubiri jioni. Chukua siha yako kwa ajili ya maradhi yako, na uhai wako kwa ajili ya mauti yako.” (Al-Bukhari)

Kwa sasa, tunaishi katika dhurufu ambapo tuko majumbani kwa muda wa mwezi wote huu. Wakati hili halimaanishi kuwa tuko huru kutokana na majukumu yetu yote, inatupa fursa ya kuzingatia dunia ambayo tunaishi ndani yake. Inatupa fursa ya kuangalia dunia iliotuzunguka, tukijua kuwa tunaishi katika dunia ambayo ndugu zetu Waislamu wa kike na kiume wanateseka wakiwa chini ya tawala zisizo za Kiislamu wakiwa na hima ya kubadilisha dhurufu hizo.

Kujificha kutokana na ukweli huu na kufanya ucheleweshaji katika matendo yetu haitoondosha jukumu la kubadilisha uhalisia.

Abu Hurayra (ra) amepokea kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«بَادِرُوا بِالْأَعْمَالِ سَبْعًا هَلْ تَنْتَظِرُونَ إِلَّا فَقْرًا مُنْسِيًا أَوْ غِنًى مُطْغِيًا أَوْ مَرَضًا مُفْسِدًا أَوْ هَرَمًا مُفَنِّدًا أَوْ مَوْتًا مُجْهِزًا أَوْ الدَّجَّالَ فَشَرُّ غَائِبٍ يُنْتَظَرُ أَوْ السَّاعَةَ فَالسَّاعَةُ أَدْهَى وَأَمَرُّ»

“Kimbilieni kutenda matendo mema haraka iwezekanavyo, Je mnacho mnachokisubiri isipokuwa ufukara wenye kucheleweshwa au utajiri wa kijeuri au maradhi yenye kudhoofisha au udhaifu kutokana na uzee au mauti ya ghafla au Dajjal?. Au mnasubiri uovu usioonekana au Saa ya Kiama? Saa ya Kiama ni chungu na ya kutisha.” (At-Tirmidhi)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi ya Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fatima Musab
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

#FromAffliction2Success     #KutokaMatatizoHadiMafanikio     #MihnettenKurtuluşa             محن_ومنح#

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu