Mauaji na Njaa ya Watoto wa Gaza Havitakwisha Kupitia Mipango ya Wale Waliohusika na Mauaji ya Halaiki Bali Kupitia Uhamasishaji wa Majeshi ya Waislamu Pekee
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika kipindi cha miaka 2 iliyopita, watu wa Gaza wamekuwa wakikabiliwa na mashambulizi ya mabomu, mzingiro wa kikatili na jinai za kutisha zaidi za umbile la mauaji la Kiyahudi, ambapo wanawake na watoto wamekuwa wahanga wakuu. 65,000 wameuwawa, wakiwemo zaidi ya watoto 20,000 – sawa na watoto 30 wanaouawa kila siku. Watoto wamepigwa risasi kimakusudi na wavamizi wa Kiyahudi au mashambulizi ya droni barabarani, au hata wanapotafuta chakula kwenye vituo vya misaada ambavyo vimekuwa ‘mitego ya kifo’ kwa wanaokabiliwa na njaa. Kulingana na ‘Save the Children’, watoto waliuawa au kujeruhiwa katika zaidi ya nusu ya mashambulizi mabaya katika maeneo ya usambazaji wa chakula mjini Gaza ndani ya wiki nne baada ya Wakfu wa Kibinadamu wa Gaza kuanza shughuli zake.