Marekani ya Kibeberu Inatumia Wakala Wake Shirika la Excelerate Energy kutia Udhibiti juu ya Bandari na Bahari zetu za Kimkakati ili Kuendeleza Udhibiti wake wa Kisiasa
- Imepeperushwa katika Bangladesh
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Balozi wa zamani wa Marekani nchini Bangladesh Peter D Haas alifanya mkutano wa karibu saa moja na Waziri wa Mambo ya Nje Asad Alam Siam mnamo Alhamisi (4 Septemba). Ingawa hakuna upande uliofichua maelezo ya majadiliano hayo, vyanzo vya habari viliripoti kuwa mazungumzo hayo yalihusu uwezekano wa kuagiza LNG kutoka Marekani, pamoja na ushirikiano wa sasa na miradi ya mustakabali. Kwa sasa Haas anatumika kama Mshauri wa Kimkakati wa Excelerate Energy - shirika la kimataifa la Texas ambalo linaendesha kituo cha LNG kinachoelea huko Maheshkhali, Cox’s bazar.