Muungano na Amerika hauruhusiwi kwa Pakistan, wala Muungano na India hauruhusiwi kwa Afghanistan
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Waziri wa Ulinzi wa Pakistan Khawaja Asif mnamo Jumatatu (20 Oktoba 2025) alitupilia mbali madai ya Afghanistan kwamba Islamabad inatenda kwa niaba ya Marekani ili kuunda mabadiliko ya serikali jijini Kabul, akielezea madai hayo kama “upuuzi mtupu”. Islamabad imesema kwa muda mrefu kwamba India, hasimu wake wa muda mrefu, inafanya kazi pamoja na Afghanistan kusaidia Tehreek-e-Taliban Pakistan (TTP), ambayo inajulikana kama Taliban ya Pakistan, na wanamgambo wengine dhidi ya Pakistan. New Delhi inakanusha madai hayo.



