Mtu Anayehusika na Usalama wa Watu Anawezaje Kukimbia Akitafuta Usalama?!
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Sudan News ilinukuu Darfur 24 katika ripoti moja yenye kichwa: “Kujiondoa kwa Uratibu au Kuanguka?! Makamanda na Maafisa wa Jeshi na Vikosi vya Pamoja Waondoka Al Fasher Siku Mbili Kabla ya Kuanguka Kwake,” ikisema: “Vyanzo viwili kutoka Darfur Kaskazini viliifichulia Darfur 24 kwamba makamanda wa jeshi, pamoja na wanachama wa vikosi vya pamoja, gavana wa Darfur Kaskazini, Al-Hafiz Bakhit, na wanachama kadhaa wa serikali yake, waliondoka Al Fasher siku mbili kabla ya Vikosi vya Msaada wa Haraka kutangaza udhibiti wao kamili wa makao makuu ya Kikosi cha 6 cha Wanajeshi Wapiganaji.”



