‘Mkataba wa Mageuzi ya Julai: Udanganyifu Mkubwa’: Hizb ut Tahrir Yalaani Mkataba huo, na Kuhimiza Badali Msingi ya Kisiasa kwa Demokrasia Iliyofeli
- Imepeperushwa katika Bangladesh
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika kujibu hotuba ya hivi karibuni ya Mshauri Mkuu Profesa Yunus kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kitaifa wa Julai na kura ya maoni kuhusu mapendekezo ya mageuzi ya katiba katika Mkataba huo, Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh inatoa onyo kali kwamba mapendekezo ya mageuzi na mchakato wake wa utekelezaji si kitu zaidi ya hatua ya juu juu ambayo inashindwa kushughulikia sababu za msingi za mgogoro wa kisiasa wa Bangladesh. Inatoa udanganyifu wa mabadiliko ili kuhifadhi dhati ya mfumo wa kidemokrasia uliofeli.



