Ijumaa, 24 Safar 1448 | 2026/08/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Amali za Kuhuisha Ibada za Dhu al-Hijjah za Mwaka 1447 H

Katika kuhuisha ibada za Dhul-Hijjah na kwa heshima ya Sunnah tukufu ya Mtume, Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan iliandaa maandamano ya takbira na tahlil mnamo Jumatatu, ya kwanza ya Dhul-Hijjah 1447 H. Maandamano yalianza kwenye lango la afisi ya hizb mjini Port Sudan, yakipita kwenye njia kuu, na kufikia Soko Kuu, ambapo yalifikia kilele chake katika ua wa Hoteli ya Al-Haramain, mahali pa mikutano ya kisiasa ya mji huo. Wakati wa maandamano hayo, umati mkubwa wa watu ulijiunga, wakipiga takbira na tahlil pamoja na ndugu zao, wakionyesha furaha yao kwa amali ya hizb na kusifu amali hii ya kipekee nchini, kwa mujibu wa maelezo yao.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Amali kwa Mnasaba wa Idd al-Adha Iliyobarikiwa 1447 H

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan iliandaa amali katika afisi yake ya Khartoum kusherehekea Idd al-Adha kwa mwaka 1447 H (2026 M). Wakati wa amali hiyo, Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, alitoa hotuba na kujibu maswali kutoka kwa waliohudhuria.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan: Amali na Shughuli Wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan 1447 H

Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan iliongeza shughuli zake za umma wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, ikihimiza jamii ya Waislamu kufanya kazi nayo ili kuanzisha jengo kuu la Uislamu: Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo ilivunjwa miaka 105 iliyopita. Iliendesha hotuba za kisiasa, mihadhara, na visimamo katika viwanja vya misikiti, masoko, na maeneo mengine ya umma, pamoja na programu zake za kawaida katika afisi zake katika miji mbalimbali ya Sudan.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Amali kwa Mnasaba wa Idd ul-Fitr Iliyobarikiwa 1447 H

Katika siku ya tatu ya Idd al-Fitr Iliyobarikiwa, sawia na Jumamosi, 12 Machi 2026 M, mashababu wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan walikusanyika katika afisi ya hizb katikati mwa jiji la Khartoum ili kupeana salamu za Idd. Mkutano huo ulijumuisha mashababu kutoka kote Khartoum, Omdurman, Jabal Awliya, Kalakila, Nile Mashariki, na maeneo mengine. Walitoa pongezi zao kwa Idd iliyobarikiwa na kuelezea furaha yao ya kuonana baada ya miaka mingi ya vita.

Soma zaidi...

Kama sehemu ya kampeni iliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan kukwamisha mpango wa kutenganisha Darfur, Hizb ilifanya Visimamo katika miji kadhaa ya Sudan

Kama sehemu ya kampeni iliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan kukwamisha mpango wa Marekani wa kuichana nchi hii kwa kuitenganisha Darfur na Sudan, hizb ilifanya kisimamo katika Msikiti wa Al-Aqit mjini Gadharef mnamo siku ya Alhamisi, Septemba 11, 2025 baada ya swala ya Ijumaa Septemba 12, 2025, miji kadhaa mikubwa ya Sudan ilifanyika visimamo, pamoja na misikiti mikuu ya Sudan yote. Shawak, Singa, Rabak, Madani, Abbasiya, Taqli, Khartoum (Kalakila na Dukhainat), na misikiti miwili mjini Omdurman.

Soma zaidi...

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Sudan Wilayah – Mji wa Kosti, Jimbo la White Nile Wakutana na Dkt. Muhammad al-Haitham, Katibu Mkuu wa chama cha National Unionist Party katika Jimbo la White Nile

Mnamo Ijumaa, 12 Septemba 2025, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Sudan ulimtembelea Dkt. Muhammad al-Haitham, Katibu Mkuu wa chama cha National Unionist Party, katika Uwanja wa Azraq Taiba huko Kosti.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Kisimamo cha Port Sudan cha Kutibua Mpango wa Kujitenga kwa Darfur!

Kujibu kwa takbira, tahlil, na uungaji mkono, pamoja na vyombo vya habari na uhamasishaji wa kisiasa, kisimamo kilifanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan kutibua mpango wa kujitenga kwa Darfur kilifanyika mbele ya Msikiti Mkuu mjini Port Sudan. Waumini walikusanyika baada ya swala ya Ijumaa, 20 Rabi' al-Awwal 1447 H - 12 Septemba 2025 M, kwenye Msikiti Mkuu mjini Port Sudan kwa ajili ya kisimamo hicho ikiwa ni sehemu ya kampeni ya hizb kutibua mpango wa kujitenga kwa Darfur.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu