Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 566
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Sudan kwa sasa iko katikati ya vita vya kipumbavu ambavyo vimesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya raia na kuzua mgogoro mkubwa zaidi duniani wa njaa na kuhama makaazi. Wananchi wa Sudan wamekumbwa na mizozo mbalimbali pamoja na umaskini mkubwa, udikteta, migawanyiko ya kikabila na kitabaka na matatizo mengine mengi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa miongo kadhaa chini ya uongozi, tawala na mifumo mtawalia.
Hizb ut Tahrir/Wilayat Bangladesh yaandaa kongamano la kisiasa lenye kichwa: “Bangladesh 2.0: Utegemezi au Ukombozi?”
Hizb ut Tahrir /Wilayah Jordan: Kalima katika Kikao cha Tanzia ya Ustadh Baker (Abu Usama) Mwenyezi Mungu Amrehemu
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia itafanya mkutano na waandishi wa habari wenye kichwa: “Hizb ut Tahrir inatoa Wito kwa Serikali na Upinzani Kuzungumza kwa Sauti Moja”
Tunajua kwamba mkakati wa Marekani wa kuasisi umbile la Kiyahudi katika moyo wa nchi za Kiislamu, kwa sehemu kubwa, umeegemezwa kwenye suluhisho la dola mbili. Hata hivyo, chini ya Trump, mkakati huu umeanza kuatelekezwa, au angalau kunyamaziwa, jambo ambalo limezua maswali. Kwa mfano, Trump alisema, "Unapotazama ramani, ramani ya Mashariki ya Kati, 'Israel' ni sehemu ndogo sana ikilinganishwa na ardhi hizi kubwa mno. Kwa hakika nilisema: 'Je, kuna njia yoyote ya kupata zaidi? Ni ndogo..." (Sky News, 19/8/2024). Je, hii inamaanisha kuwa mradi wa suluhisho la dola mbili wa Amerika umekufa na kukamilika, au bado ungali hai?