Enyi Watu wa Jordan na Wanajeshi Wake: Jihadharini na Kundi la Kitengo cha Gilead, Vitisho vya Umbile la Kiyahudi kwa Nchi yenu, na Ushiriki na Utiifu wa Serikali!
- Imepeperushwa katika Jordan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Jana, 10 Septemba 2025, kamanda wa Kamandi Kuu ya jeshi la umbile la Kiyahudi alitangaza kuundwa kwa kitengo kipya cha kijeshi, kinachoitwa “Kitengo cha Gilead,” katika Bonde la Jordan, kitakacho kaa kwenye Bonde la Jordan. Kitengo hichi cha kikanda kina jukumu la kulinda mipaka ya mashariki ya Mayahudi katika Bonde la Jordan na Bahari ya Dead. Aliashiria kuwa kuanzishwa kwa kitengo hicho kunajiri ndani ya muundo wa kile alichoelezea kama “masomo ya kujifunza kutokana na kushindwa kugumu kwa Israel mnamo Oktoba 7, 2023.” Uundaji huu mpya unakuja baada ya vitisho vya viongozi wa umbile la Kiyahudi kupanuka hadi nchini Jordan na kwengineko chini ya mwavuli wa mradi wa “Israel Kubwa”, uliotangazwa na Netanyahu, uliobarikiwa na Trump, na kutangazwa wazi na Smotrich, Waziri wa Fedha wa umbile la Kiyahudi.