Alhamisi, 07 Safar 1442 | 2020/09/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Lukashenko na Udikteta wa Ulimwengu wa Kiislamu:
Sura Mbili za Wapiganaji wa Uimla

Habari:

Muuangano wa Ulaya umeweka vikwazo dhidi ya maafisa 20 nchini Belarus. (Chanzo: euronews)

Maoni:

Leo vyombo vyote vya habari vinaangazia yanayojiri nchini Belarus, ambako dhalimu mwengine hakufaulu kuwazuia watu wake mwenyewe. Habari kutoka Belarus zinatupa fursa ya kuelezea kuhusu matukio sawia na haya katika ulimwengu wa Kiislamu, ambayo mizani yake inazidi habari za Belarus kwa mara nyingi mno. Katika maoni yangu nataka kuelezea kuhusu sura mbili za wale wanaoitwa "wapiganaji wa uimla", nazo ni kuhusu watawala wa ulimwengu wa Kimagharibi, wanaozungumza kuhusu uimla wa Lukashenko, lakini hawazungumzii kuhusu uhalifu wa vibaraka wao katika ulimwengu wa Kiislamu.

Ukweli ni, wale wanaoitwa watetezi wa haki za kibinadamu na wapiganaji wa uimla hawajali lolote kuhusu mtu wa kawaida, hawajali kuhusu raia wa Belarus wanaokufa leo katika viwanja vya miji ya Belarus. Hawajali kuhusu raia wa kawaida wa Ukraine waliokufa katika Uwanja wa Uhuru jijini Kiev mnamo 2014. Wanachojali pekee ni namna ya kulinda ushawishi wao wa kisiasa katika nchi nyenginezo.

Kwa kuwa Yanukovich nchini Ukraine, Lukashenko nchini Belarus na Putin nchini Urusi wanajumuisha nguvu za kisiasa dhidi ya Magharibi, Magharibi leo inazungumzia kuhusu watu wasio na hatia wanaopigwa na kuuwawa nchini Belarus, Ukraine na Urusi. Lakini "marafiki hawa wa waliodhulumiwa" hawazungumzii kuhusu Waislamu wanaopigwa na kuuwawa katika nchi za Waislamu kwa miongo mingi. Wakati wa maandamano ya 2014 nchini Ukraine watu 107 walikufa. Maarufu walijulikana kama "mia wa mbinguni". Ni "mia wa mbinguni" wangapi walioko katika Ummah wa Kiislamu? Kuna maelfu ya Waislamu wanaokufa katika maandamano makubwa ya miongo mingi dhidi ya uimla.  

Lakini hakuna yeyote anayejitolea kuwatangazia katika vyombo vya habari. Na endapo mtu atasubutu kufanya hivi mara moja anakashifiwa kwa hili na kufutwa kazi kutoka kwa wadhifa wake kama ilivyokuwa kwa Craig Murray, balozi wa zamani wa Uingereza nchini Uzbekistan. Mrithi wa dhalimu Islam Karimov Shavkat Mirziyoyev leo kwa mara nyengine tena ameangika mikono huku maelfu ya Waislamu wakiendelea kuteseka gerezani kwa kusema tu "Mola Wangu ni Mwenyezi Mungu" pekee. Raisi wa Misri Abdel Fatah as-Sisi aliyewauwa maelfu ya watu katika Uwanja wa Tahrir jijini Cairo mnamo 2013 ni D. "Dikteta Mpendwa" wa Trump. Kwa maana nyengine, Trump ana madikteta wengi kwa kuwakandamiza Waislamu, huku furauni mpya Sisi akiwa ni mpendwa wake.

Sababu ya hili ni kuwa "wapiganaji wa uimla" hawajali kuhusu kumaliza mateso ya watu bali wanajali kuhusu kulinda maslahi yao ya kisiasa na kiuchumi. Hivyo basi inapokuwa ni kwa manufaa yao kuwa na watu kama tulivyoona nyuma nchini Ukraine na Belarus na Urusi leo, Magharibi itazungumza sana kuhusu uimla na watawala wa kiimla, kwa kuwa watu katika nchi hizi wanaona badali katika maadili ya Kimagharibi.

Lakini pindi ikiwa hakuna faida kama tunavyoona katika ulimwengu wa Kiislamu, Magharibi itanyamaza kimya kuhusu watawala wa kiimla na fauka ya hayo itawasaidia. Katika ulimwengu wa Kiislamu, watu huanzisha uasi kwa lengo la kuondoa kamama ya Kimagharibi inayoashiriwa na watawala wa kiimla. Waislamu wanataka kuasisi nidhamu kwa mujibu wa matarajio yao ambayo ni muundo wa utawala wa Kiislamu ambao Waislamu waliufurahia kwa karne nyingi.

Hii ndiyo sababu pekee ya uimla katika ulimwengu wa Kiislamu kwa miongo mingi, ambao ungekuwa umetoweka lau kama haungesaidiwa kisiasa, kiuchumi na kupitia vyombo vya habari na jeshi vya wale wanaoitwa "wapiganaji wa uimla". Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Quran:

(وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لاَ تُفْسِدُواْ فِي الأَرْضِ قَالُواْ إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ)

"Na wanapo ambiwa: Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji." [2:11].

Maneno haya yana thamani iliyoje katika kuelezea uhalisia wa leo wa ulimwengu wa Kiislamu. Baada ya Waislamu wote kuwaambia viongozi wa Kimagharibi wanaowasaida madikteta katika ulimwengu wa Kiislamu yafuatayo: "Msiwe upande wa watawala wa kiimla na msifanye uharibifu katika ardhi" majibu wanayoyasikia ni: "Sisi tunalowatakieni nyinyi ni kheri, sisi ni wawekaji amani tu katika nchi yenu". Lakini hili si lolote ila ni unafiki tu.

Licha ya juhudi zote na usaidizi kwa watawala wa kiimla kutoka kwa Magharibi leo Ummah wa Kiislamu katika sehemu zake zote unataka kuepukana na watawala hawa Ruwayabidhah. Pasi na shaka leo Waislamu wako kwenye kizingiti cha mabadiliko ya kweli ya kihistoria katika ulimwengu wa Kiislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari Hizb ut Tahrir na
Fazil Amzaev
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 06 Septemba 2020 14:19

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu