Jumanne, 06 Jumada al-thani 1442 | 2021/01/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kufikia Kwenye Mzizi wa Tatizo la Ufaransa

Kuchapishwa tena kwa gazeti la tashtiti la Kifaransa la Charlie Hebdo lenye msururu wa katuni za mabishano zinazomchora Mtume Muhammad (saw) kunakoashiria mwanzo wa mashtaka juu ya shambulizi katika afisi zake mwaka 2015, kwa mara nyengine tena limevuta mawazo ya mivutano baina ya Ufaransa na Uislamu. Picha zimeripua machafuko mengine, yaliyopelekea kifo cha mwalimu wa Kifaransa wa shule ya msingi  mwezi Oktoba 2020. Raisi wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa lawama moja kwa moja juu ya Uislamu akieleza kuwa “Uislamu uko katika mgogoro kote ulimwenguni.” Ufaransa, kwa muda mrefu imekuwa na mahusiano mabaya na Uislamu na wafuasi wake. Hata hivyo, hivi sasa inakabiliana na matatizo magumu zaidi ya yale ya wahamiaji wake wapatao milioni 6.5.

Mwaka 1789, Ufaransa ilisimamisha dola imara katikati ya Ulaya kupitia Mapinduzi ya Ufaransa. Wafaransa walimuuwa Mfalme wao na kuwa watu wa mwanzo kuukumbatia uhuru wa mtu binafsi na usekula katika Ulaya ikiwa ndio maadili ya kujengea mfumo wake wa siasa-jamii. Wafaransa waliongoza mabadiliko Ulaya na kuwa vinara wa mfumo mpya; hii ndio sababu wanafikra wengi na wanafalsafa wa zama zile walikuwa ni Wafaransa, kama Voltaire. Wafaransa tokea wakati huo wamekuwa na heshima kubwa katika kipindi hichi cha historia kikitajwa kuwa ni sehemu msingi ya utambulisho wa Wafaransa. Kisha baadaye, walielekeza mawazo yao Ulaya na nje yake. Matumizi ya nguvu za kijeshi ya Ufaransa yalishinda kwa ufanisi wa kikatili, huku ikieneza matumizi yake ya ushawishi kupitia thaqafa yake ya kiliberali ya kisekula.

Koloni muhimu kwa Ufaransa lilikuwa eneo la Afrika Kaskazini la Algeria. Wafaransa waliivamia Algeria mwaka 1830 na mara moja waliitawala. Mkakati wao muhimu ulikuwa ni kuifanya iwe ni sehemu ya Ufaransa ili itawaliwe kama nchi moja. Walijaribu kufanya haya kwa kuwapeleka Algeria mamia ya maelfu ya Wazungu waliojulikana kama pied-noirs (walowezi). Lakini Ufaransa ilijitahidi kuidhibiti na kuichukuwa Algeria. Ndani ya miongo mitatu ya mwanzo (1830-1860) ya uvamizi, hadi Waalgeria milioni moja kati ya milioni tatu waliuliwa na Wafaransa kutokana na vita, mauwaji ya watu wasiokuwa na hatia, maradhi na ukame. Uvamizi jumla wa Ufaransa nchini Algeria ulitumia rasilimali nyingi na kulikuwa na sababu moja kwa hilo, ambayo aliielezea Charles-Andre Julien katika jarida la Mambo ya Kigeni mwaka 1940: “Kukamatwa kwa Algiers mwaka 1830 kuliashiria safari muhimu katika sera ya Ufaransa ya kujipanua, kwa kuwa Afrika Kaskazini ilikuwa sio kama makoloni ya zamani yaliomilikiwa na Ufaransa katika Bahari ya Caribbean na Bahari ya Hindi. Ufaransa mara moja ilitambua kuwa Afrika Kaskazini haikuwa ikizalisha bidhaa za kitropiki na kuwa wakaazi wenyeji hawakuwezekana ima kuangamizwa kuweka njia kwa wakoloni wa Kizungu wala kuwatia utumwani kuwafanyisha kazi kwa maslahi yao. Pia waligundua kuwa Uislamu uliwapatia wenyeji maadili ya kidini na kithaqafa ambayo yaliwafanya kujihami kwa ushupavu. Ufaransa haikujiandaa kiuzoefu kufahamu na kuwatawala Waislamu.”

Katikati ya karne ya 20 uzani wa nguvu za kilimwengu ulibadilika. Wakati Ufaransa na Uingereza zikiwa ndio dola zenye nguvu zaidi, Vita vya Pili vya Dunia (WW2) vilibadilisha kila kitu. Wanazi waliidhalilisha jamhuri ya Ufaransa kwa kuiteka katika kipindi cha siku 44 tu. Ufaransa ilikuwa na wakati mgumu baada ya WW2 ikijaribu kurejesha nafasi yake katika medani ya ulimwengu. Wakati karne ya 20 ikipita, nafasi ya Ufaransa na ushawishi katika dunia umekuwa ukiendelea kushuka. Kuanguka kwa ushawishi wa Ufaransa duniani kote ni jambo ambalo Wafaransa wamejifunza kuwa nalo.

Kufifia kwa ushawishi wa Ufaransa ulimwenguni kumekuwa na athari mbaya kwa jamii ya Ufaransa. Uchunguzi wa mfululizo wa Wafaransa umeendelea kuonyesha kuwa watu wamekata tamaa na hali mpya jinsi ilivyo. Mwanzoni mwa karne mpya, Gazeti la Time liliandika kuwa utamaduni wa Ufaransa ‘unakufa’. Ufaransa iliokuwa maarufu wakati mmoja kwa kile kinachoitwa joie de vivre (kufurahia maisha), inataabika kutokana na maisha ya huzuni; Profesa Claudia Senik, profesa wa Chuo Kikuu maarufu cha Sorbonne ameitaja Ufaransa hivi sasa kwamba imekuwa yenye utamaduni dhaifu. Uchunguzi wake juu ya udhaifu wa Ufaransa, kabla ya miaka ya 70 (1970s), ameona kwamba: “Inahusiana na namna Wafaransa wanavyoiangalia dunia na nafasi yake humo. Wana matarajio makubwa kuhusu ubora wa maisha, uhuru na maadili mengi yanayosukumwa na Mapinduzi ya Ufaransa na hii imeweka kigezo cha kiwango cha juu cha furaha” Senik amesema. “Wanaangalia nyuma katika zama za ustawi wakati Ufaransa ilipokuwa ikiweka kanuni za mchezo, na hivi sasa tumekuwa kijinchi chengine kidogo ambacho kinalazimishwa kukubali na kujifunga na kanuni.”

Wakati Ufaransa wanaamini kuwa wana maadili bora zaidi, maadili haya yameshindwa kutatua wingi wa matatizo yanayoikabili nchi. Kwa upande wa kiuchumi, muundo wa kijamii ya kidemokrasia ya Ufaransa, ambapo serikali ina jukumu kubwa katika uchumi, inaficha hali mbaya sana ya kutokuwepo kwa usawa. Walio matajiri zaidi ambao ni asilimia 10 wanamiliki asilimia 55 ya utajiri wa nchi na usawa wa kipato ni mbaya zaidi. Mfumo wa usalama wa kijamii wa Ufaransa kwa muda mrefu umekuwa ni suluhisho kwa hili, lakini hivi sasa imekuwa ni sababu ya deni la taifa kulizidi pato la taifa (GDP). Ubinafsi katika Ufaransa kwa muda mrefu umekuzwa na kuwa ni maadili ya Ufaransa lakini imeipelekea Ufaransa kuwa na kiwango kikubwa zaidi cha utumiaji wa madawa yenye kuharibu tabia, na kuwa moja ya nchi yenye kiwango kikubwa zaidi ya vifo vya kujiua. Ufaransa hivi sasa inajikuta iko juu kati ya nchi za Ulaya zenye viwango vya juu vya watumiaji wa madawa ya kutuliza akili na ulevi katika Ulaya. Ufaransa imeonekana kwenye tafiti kuwa ni ya juu zaidi ya watu wasio na furaha ulimwenguni. Uhuru, usawa na udugu huenda ni kauli mbiu ya Ufaransa lakini imefanya machache kushughulikia suala la kutokuwepo usawa, mgawanyiko na matumizi mabaya ya madaraka nchini Ufaransa.

Ufaransa kwa kawaida iko juu kwenye uchunguzi wa viwango vya huzuni na kukosa matumaini ya baadaye. Maandamano ya kundi la vizibao vya Manjano ambayo yameisimamisha Ufaransa yameonyesha kuwa matatizo ya nchi hayatokani na Waislamu wachache bali ni kushindwa kwa tabaka la kisiasa na mifumo, ambayo ni tatizo kubwa kote katika ulimwengu ulioendelea. Uhuru umenasibishwa na matatizo ya kijamii kama kuvunjika kwa familia, mfadhaiko na upweke. Usekula umetenganisha kanisa na serikali, lakini fedha na siasa vimetia sumu nidhamu za kisiasa kote katika nchi za Magharibi – nidhamu zilizoshindwa kuwasaidia wanaadamu. Wanasiasa wa Kifaransa daima wamekuwa wakipindisha mijadala kuhusiana na mambo haya kwa kuwalaumu wahamiaji na Waislamu na ndio sababu hivi leo misuli ya uliberali unaolazimishwa na dola unashabihi zama mpya ngumu za uhafidhina zikiwakabili wahamiaji wake wachache wapatao milioni 6.5 – wahamiaji waliokuja Ufaransa kusaka maisha bora, lakini wakawasili katika wakati ambao Wafaransa wenyewe wamepoteza matumaini katika maadili yao, serikali na taifa.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Adnan Khan

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Waislamu wa Sri Lanka, Hakuna wa Kuwalilia!!

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu