Jumapili, 03 Safar 1442 | 2020/09/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hairuhusiwi Kuchukuwa Fikra Kutoka Kwengine Kusikokuwa Uislamu

Kila fahamu isiyokuwa ya Uislamu haipaswi kuchukuliwa kwani zote ni fahamu za kijinga, japokuwa zinaonekana kuwa za kustaarabika na ziliotukuka, kama usekula, ambao huitwa fikra angavu miongoni mwa wanafikra wa Kimagharibi. Haijuzu kwa Waislamu kuvutiwa au kuheshimu fikra yoyote ya kigeni, ima iwe ni sehemu yake tu au yote kamili ambayo haipaswi kuchukuliwa hata kwa uzito wa chembe ndogo mno. Sababu ya kila balaa linaloukumba Ummah tokea ianze historia ya Uislamu ni kuchukua fikra za kigeni mbali na Uislamu, kama vile ukabila, falsafa za Kigiriki na Kihindi, utaifa wa Kiarabu na Kituruki, usekula na nyenginezo.

Watawala na wanachuoni katika Dola ya Kiislamu iliopita walitumia juhudi zao kuzifurusha fikra hizi fisidifu nje ya ardhi za Kiislamu na katika akili za Waislamu hadi kuvunjwa kwa Khilafah. Kuanzia hapo, Makafiri hawakuona ngao yoyote mbele ya Waislamu ya kuwahifadhi kutokana na uvamizi wa kithaqafa wa Kimagharibi. Na hivyo Waislamu wengi wamepagawishwa na fikra za Kimagharibi kiasi cha kuwa baadhi yao husema ‘Uislamu ni dini ya amani kama dini nyengine, inahakikisha uhuru wa kuabudu’ na hivyo wanapinga kuuliwa kwa wanaoritadi, huku wengine nao wakisema ‘adhabu katika Uislamu kama vile kukata mkono na kuchapwa mijeledi wazinifu zinahitaji marekebisho’, kana kwamba Uislamu haujitoshelezi na hivyo fikra nyengine ziongezwe na kana kwamba wanaadamu wako juu ya Mwenyezi Mungu (Mwenyezi Mungu atuepushe) katika kupangilia mambo ya watu.

Muislamu hachukui fikra yoyote mbali na Uislamu, ima iwe ni sehemu au yote kamili, kwa kuwa Uislamu unajitosheleza na ni mkamilifu na hivyo hatoshangazwa na fikra yoyote ya kigeni. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

   [الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإِسْلاَمَ دِينًا]

“Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema zangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndio Dini.”  [TMQ 5:3]

Zaidi ya hayo, Mwenyezi Mungu (swt) ameteremsha kitabu chake kuwa ni ufafanuzi kwa kila kitu na hakuwacha kitu chochote bila ya ufafanuzi ili kichukuliwe kutoka kwenye fikra nyengine kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyo sema,

[وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَى لِلْمُسْلِمِينَ]

“Na tumekuteremshia Kitabu hichi kinachobainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu” [TMQ 16:89]

Hivyo hivyo, Muislamu anapaswa kuuchukua Uislamu kwa ukamilifu na sio kivipande kwani Uislamu ni mkamilifu na mpana. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ ادْخُلُواْ فِي السِّلْمِ كَآفَّةً وَلاَ تَتَّبِعُواْ خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ]

“Enyi mlioamini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za Shetani, hakika yeye kwenu ni adui alie wazi” [TMQ 2:208]

Baada ya fikra ya kisekula kutawala dunia, watu walianza kufikiri kuwa wanaweza kupangilia mambo ya maisha yao pasi na haja ya Muumba wao na hivyo wakaitenganisha dini na maswala ya maisha. Hata hivyo, mkorogo ulioko leo katika maswala yao ya maisha, ima yawe ni ya kiuchumi au kijamii ni kutokana na upangiliaji wa mambo yao ya kimaisha kwa kutumia akili zao pungufu, ikiashiria kuwa hawawezi kuendesha mambo yao ya kimaisha bila muongozo kutoka kwa Muumba wao anaye simamia dunia na ulimwengu wote ambapo mtu hawezi kushuhudia fujo au tofauti kati yao, na ni rahisi Kwake (swt) kuyafanya hayo. Basi vipi wanadamu watataka kupangilia mambo yao kwa kutegemea akili zao wakati Mwenyezi Mungu (swt) anawaongoza kwayo kwa dini ya kweli. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,  

[أَفَغَيْرَ دِينِ اللّهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ]

“Je, wanataka dini isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila kilichomo mbinguni na katika ardhi kimesilimu kwa kumtii Yeye kikipenda kisipende, na kwake Yeye watarejeshwa? [TMQ 3:83]

Pia, kuchukua kichache kutoka katika fikra za kigeni ni kuivuruga dini tu kwa ujumla. Sababu kubwa ya kuuliwa kwa Uthman bin Affan (ra) ilikuwa ni kuichukua fikra ya kijinga ya kikabila baada ya Iman. Mtume (saw) aliasisi jamii ambayo ilijengwa juu ya Itikadi ya Kiislamu na yeye (saw) aliondosha fikra zote za kijinga ikiwemo ukabila kutoka kwenye mabongo ya Waislamu. Kwa hivyo ilikuwa Masahaba wote wa Mtume (saw) hawakutafautisha watu kutokana na makabila na rangi zao. Vile vile, Uthman (ra) aliwachagua magavana na viongozi kwa msingi wa uwezo wao katika kuchunga mambo ya watu wala hakutafautisha baina ya Banu Umayya, Banu Hashim na wengine katika kuwachagua magavana. Hata hivyo, kile kilicho sababisha mauwaji ya Uthman (ra), yaliofuatiwa na msururu wa fitna baada ya mauwaji hayo, ilikuwa ni baadhi ya watu kuchukua na kufadhilisha fikra ya kikabila dhidi ya Iman. Kama sio juhudi za watawala wa kikweli kama Ali bin abi Twalib (ra) kuzima fitna hazo baada ya mauwaji hayo, Uislamu ungekuwa umefungika pale ulipo ibukia na ufunguzi zaidi wa ardhi usingetokea.

Hivyo hivyo, wakati Uislamu ulipofika katika ardhi tofauti tofauti, ilikuwa ni jambo la kimaumbile kwa Uislamu kuwa na mvutano wa kifikra na fikra na dini nyenginezo. Hata hivyo, kilicho sababisha kuachana na njia ya sawa ya mvutano wa kifikra ilikuwa ni ushawishi wa fikra nyenginezo kama falsafa za Kigiriki juu ya baadhi ya Waislamu, ambazo hatimaye zilipelekea matatizo makubwa katika akili za Waislamu. Kama sio juhudi za wanachuoni wenye ikhlasi kama Imam Ghazzali kukabiliana na fikra hizi fisidifu, Uislamu ungelichanganywa na fikra nyenginezo. Pia, kasumba iliyo pitiliza ya utaifa na kutaka uhuru, kama utaifa wa Kiarabu na Uturuki, uliathiri pakubwa kuvunjwa kwa Khilafah katika karne iliopita. Hivi leo makafiri wengi hutamani Waislamu waritadi kupitia kuchukua fikra zisiokuwa za Uislamu na hivyo wanataka kuwachanganya Waislamu na fikra za kisekula. Kuna onyo kwa Ummah kutoka katika mtazamo wa sharia na historia la kutochukua fikra yoyote ya kigeni ili wasirudi kuwa makafiri baada ya kuamini kwao muongozo wa Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

 [وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الإِسْلاَمِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ * كَيْفَ يَهْدِي اللّهُ قَوْمًا كَفَرُواْ بَعْدَ إِيمَانِهِمْ وَشَهِدُواْ أَنَّ الرَّسُولَ حَقٌّ وَجَاءهُمُ الْبَيِّنَاتُ وَاللّهُ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ‏]

“Na anaye tafuta dini isiyokuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri. Mwenyezi Mungu atawaongoaje watu waliokufuru baada ya kuamini kwao, na wakashuhudia ya kuwa Mtume huyu ni wa haki, na zikawifikia hoja zilizo wazi? Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.” [TMQ 3: 85-86]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Muhammad Bin Farooq

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu