Ijumaa, 10 Shawwal 1445 | 2024/04/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Usimamishaji Khilafah ni Faradhi juu ya Kila Muislamu Kote Ulimwenguni, Ima Awe Anadhulumiwa Moja kwa Moja na Serikali Dhalimu au La

Tangu kuanguka nguvu ya ukomunisti na uhuru wa Kyrgyzstan, nchi hii inajaribu kuunda hisia kwamba Kyrgyzstan ni dola ya kisekula ambayo haishawishiwi tena na fikra ya upagani na inamdhamini kila mmoja haki yake ya kuamini. Lakini kiuhalisia, inaonekana tofauti. Katika miaka ya hivi karibuni idadi ya misikiti, taasisi za elimu za Kiislamu na madrassa zimeongezeka. Waislamu, ambao ni jumla ya asilimia 86 ya watu, wameanza kutekeleza Uislamu zaidi na zaidi katika maisha yao ya kila siku na Shariah pia imehusishwa katika maswala ya kisiasa. Jambo hili linaihofisha serikali ya kisekula ya Kyrgyzstan na, chini ya pingamizi la ugaidi na msimamo mkali, serikali inajaribu kufanya kila linalowezekana kuzuia kuenea kwa Uisilamu kama njia ya maisha.

Kuanzia katika usimamizi wa nyenzo za masomo katika taasisi za Waislamu, pamoja na shule jumla za dola na hata kukataza uvaaji wa hijab shuleni na kuwazuia wanaume kufuga ndevu, serikali inaingilia utekelezaji wa Uislamu. Bila shaka, serikali hii ya kisekula ya kikatili iliipiga marufuku kazi tukufu ya Hizb ut Tahrir mnamo mwaka wa 2004. Tangu wakati huo, ukamataji wa kikatili wa wanachama au mashabiki wa chama hiki umekuwa ukifanyika ili kuwahofisha wanachama na kuwazuia kueneza njia ya maisha ya Kiislamu. Hata wanawake wanakamatwa na kufungwa gerezani bila ya sababu yoyote, ili tu kuutisha Ummah.

Mnamo Juni mwaka huu, wanawake 8 wa Kiislamu walikamatwa na wawili wao wangali gerezani bila ya sababu yoyote. Arunova Erkingul na Baktybek kyzy Mahabat wako jela kwa kumiliki nyenzo za Kiislamu. Serikali hii ya kikatili haijali kuhusu umri wa wanawake, watoto wao, wazazi wao wakongwe, na afya zao au za familia zao. Wanajaribu kufanya kila kitu ndani ya uwezo wao kueneza mawazo ya kisekula na kuwaweka watu mbali na Uislamu.

Tangu kuvunjika Khilafah, Ummah umejipata katika hali hii mbaya, ambapo wake zao, watoto wao, wazazi wao wanavumilia mateso ambayo hayawezi kuvumilika. Wanakamatwa, kuteswa, kubakwa, kunyimwa chakula, kulipuliwa mabomu na kupigwa marufuku kutekeleza njia yao ya maisha. Lakini habari njema ni kuwa wanajitolea mhanga kwa ajili ya Uislamu na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na inshaAllah watapokea malipo yasio na idadi. Lakini jambo la kutisha juu yake ni je tumefanya nini kama Waislamu kwa ajili ya Uislamu? Je, sisi pia tunastahiki kutarajia malipo yayo hayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) wakati hatufanyi lolote kwa ajili ya Dini yetu na tumeshughulishwa na maisha yetu, huku wakati huo huo kaka zetu na dada zetu wakiendelea kuvumilia mateso kama hayo kwa ajili ya Uislamu? Je, si aibu kumuomba Mwenyezi Mungu (swt) pepo ya daraja ya juu kabisa, ilhali hatujajitolea kwa kiwango cha juu kabisa kwa ajili ya Uislamu? Tunazisababishia nafsi zetu matatizo yasiyo na maana na kuyaona kama mitihani kwetu na tunashughulika nayo kila siku, tukisahau suluhisho halisi la Ummah na dori halisi ya Muislamu katika hii Dunia. Nukta sio kwamba kila mmoja awekwe gerezani au akumbwe na mateso, bali inahusu kutambua ushirika wake ndani ya Ummah wa Kiislamu, kufanya kazi na Ummah kwa ajili ya ukombozi wake wa kweli na kutumia wakati ndani ya Dunia hii kwa ajili ya Dini ya Mwenyezi Mungu (swt).

Nafi’a ameripoti akisema: “Abdullah ibn Umar aliniambia kwamba amemsikia Mtume (saw) akisema:

«مَنْ خَلَعَ يَدًا مِنْ طَاعَةٍ لَقِيَ اللَّهَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا حُجَّةَ لَهُ وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً»

‘Yeyote mwenye kuondoa mkono katika utiifu atakutana na Mwenyezi Mungu (swt) Siku ya Kiyama hali ya kuwa hana hoja kwake, na yeyote anaye kufa na hana Bay'ah (utiifu) shingoni mwake (kwa Khalifah) amekufa kifo cha Kijahiliya (zama za ujinga).’” [Muslim]

Usimamishaji Khilafah ni faradhi juu ya kila Muislamu kote ulimwenguni, ima awe anadhulumiwa moja kwa moja na serikali dhalimu au la. Kupuuza faradhi hii ya haraka ni mojawapo ya madhambi makubwa ambayo kwayo Mwenyezi Mungu (swt) anaadhibu vikali. Hivyo tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) asahilishe mitihani ya dada zetu waliokamatwa nchini Kyrgyzstan ili washiriki katika kazi hii tukufu ya Kusimamisha Tena Khilafah kwa Njia ya Utume ili wapokee malipo bora zaidi miongoni mwa wanadamu.

Ameen Allahuma Ameen.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Amanah Abed
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

مسلمات_قرغيزستان#

#KırgızistanlıMüslümanKadınlaraÖzgürlük

#FreeMuslimahsKyrgyzstan

#WaacheniHuruWanawakeWaKiislamuKyrgyzstan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 31 Agosti 2020 14:40

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu