Jumapili, 16 Rajab 1442 | 2021/02/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kizazi cha Wazee Hakiheshimiwi chini ya Miundo ya Urasilimali

Habari:

Mgonjwa wa akili ambaye alikufa kwa njaa baada ya marupurupu yake kusimamishwa aliachwa na serikali katika hatari ya "kuumia baya", Mahakama Kuu imesikia.

Mwili uliokuwa umechakaa wa Errol Graham ulipatikana mnamo Juni 2018 wakati polisi walipovunja gorofa yake ya Nottingham kumtoa.

Familia yake inaamini Idara ya Kazi na Pensheni (DWP) inayoshughulikia kesi ya mzee huyu mwenye umri wa miaka 57 ilikwenda kinyume cha sheria na kukiuka haki zake za kibinadamu.

Kesi yao inasikizwa katika Mahakama Kuu. (BBC, 12 Januari)

Maoni:

Ukweli kwamba aliachwa kwa muda mrefu bila kuangaliwa kufikia kiwango ambacho alikufa kwa njaa ni jambo la kawaida sana kwa wazee wengi. Katika jamii za Magharibi, kanuni ya ubinafsi inatawala juu ya majukumu ya pamoja tuliyo nayo kwa kila mmoja kama wanadamu. Wazee wanaonekana kama mzigo kwa jamii kwani Urasilimali unathamini manufaa ya kimada ambayo watu wanaweza kutoa. Ikiwa hawawezi kuchangia la maana, kusudi na thamani yao hupunguzwa. Hili linaonekana wazi kwa kuwa haja ya kumtembelea ilikuwa kwa sababu tu kulikuwa na hasara ya kimada kutoka kwa mwenye nyumba.

Katika Uislamu, wazee wanaonekana kuwa raia wa thamani wa jamii kutokana na mchango wao mkubwa katika historia ya maisha yao na kwa maarifa wanayoleta kwa kizazi kijacho. Thawabu kubwa huonyeshwa katika Uislamu kwa kuheshimu na kutunza mahitaji ya wazee. Ni haki yao, bila shaka, kuwa na pesa kwa maisha yao yote kwa ajili ya mahitaji yao. Nidhamu ya kiuchumi ya Uislamu inahakikisha kuwa ni aina ya fedha za umma na kamwe haiwezi kusimamishwa ghafla.

Qur'an inaeleza waziwazi:

 [وَقَضَى رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا]

“Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.” [Surat Al-Israa’: 23-24].

Kuwapeleka wazee kwenye nyumba za wazee wakati wanafamilia walioko wanataka uhuru wa kuishi maisha yao ni kawaida huko Magharibi. Kwa kweli, ni mojawapo ya fursa za biashara zenye faida kubwa. Kutupwa kwa maisha ya wanadamu kwa watu wageni kabisa ambao wanaowaona wazee kama akaunti wazi za benki ni jambo baya sana kwa mataifa ya sasa ya kidemokrasia na ni mtindo ambao hatuwezi kuuruhusu kukua katika nchi zetu za Kiislamu.

Inshallah kurudi kwa Khilafah kutahakikisha kuwa wazee, Waislamu na wasiokuwa Waislamu wanaangaliwa kwa hali nzuri zaidi, chini ya sheria pana za upangaji za haki za kibinadamu za Kiislamu, zilizoundwa na Mwenyezi Mungu (swt).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Imrana Mohammad

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu