Jumamosi, 10 Jumada al-thani 1442 | 2021/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 China Yatangaza Kambi za Mateso za Wauyghur

Habari:

Mnamo tarehe 7 Januari 2021, Twitter ya Ubalozi wa Jamhuri ya China (PRC) nchini Amerika ilichapisha chapisho lililotangaza kambi za kile kinachoitwa "kuwaelimisha upya" Waislamu wa Uyghur.

Chapisho hilo lilijumuisha link ya nakala muwafaka ya upigiaji upatu kutoka kwa vyombo rasmi vya habari vya Kichina lililokuwa na utangulizi ufuatao: "Utafiti unaonyesha kuwa katika mchakato wa kutokomeza msimamo mkali, akili za wanawake wa Uygur huko Xinjiang zilikombolewa na usawa wa kijinsia na afya ya uzazi zikaimarishwa, ikiwafanya wao kutokuwa tena mashini za utengenezaji watoto. Wanajiamini na kuwa huru zaidi".

Na maandishi ya makala haya yenyewe yanaelezea jinsi gani kwa sababu ya mabadiliko katika akili za Wauighur wa Kiislamu "kiwango cha uzazi huko Xinjiang kilipungua kutoka asilimia 1.6 mnamo 2017 hadi asilimia 1 mnamo 2018", na "ukuaji wa kawaida wa idadi ya watu ulipungua kutoka asilimia 1.1 hadi asilimia 0.6".

Maoni:

Wataalam wengi walishangaa juu ya chapisho kama hilo la kipuuzi; baadhi yao walidhani kwamba labda uchapishaji huo ulihusishwa na siku ya uthibitisho wa mwisho wa ushindi wa Biden katika uchaguzi wa urais nchini Amerika, na kwa hivyo kushindwa kwa Trump, ambaye kwa kipindi chake chote cha urais alizilaumu mamlaka za PRC na uwepo wa kambi za mateso kwa wa-Uighur.

Kumbuka kwamba Wauyghur wamefanyiwa ukandamizaji na shinikizo kali zaidi katika eneo la Mashariki mwa Turkestan lililochukuliwa na China kwa miongo kadhaa - Wachina wanawafunga mamilioni yao, kuwaozesha kwa lazima wasichana wa Uyghur kwa wanaume wa Kichina, na hata kuwapa makao wanaume wa Kichina katika familia za Uyghur.

Ama upande wa Amerika, kaulimbiu ya Uyghur imekuwa ikitumiwa nao (na muda mrefu kabla ya urais wa Trump) kwa madhumuni ya kuishinikiza China, kwa kutumia uhalifu ambao inaufanya katika XUAR ili kutia shinikizo la kimataifa juu yake, vile vile kwa ajili ya kulazimisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya China, ambayo inakuwa hoja nzito katika vita vya kibiashara. Na ni dhahiri kwa mtu yeyote kwamba Waamerika kamwe hawahisi huruma yoyote kwa Wauighur, ingawa wanaelezea "wasiwasi" wao usio na mwisho.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu