Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Msimamo wa Hizb ut Tahrir kwa Palestina katika Kongamano Lake "Kujiweka Mbali na Khiyana Kubwa" ni Msimamo Unaowakilisha Waislamu
Na: Ustatha Rola Ibrahim *

(Imetafsiriwa)

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir ilifanya kongamano kubwa mtandaoni kwa ushirikiano na Al-Waqiyah TV kuhusu khiyana kubwa iliyofanywa na Imarati na Bahrain chini ya anwani: "Kujiweka Mbali na Khiyana Kubwa" mnamo Jumamosi, 2 Safar al-Khair 1442 H sawia na 19/9/2020 M. Kongamano ambalo ripoti za kuitishwa kwake ziligonga kama radi kwenye vichwa vya wale wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Mara tu kongamano hili lilipoanza shughuli zake, uongozi wa Facebook ulizuia ukurasa wa Afisi Kuu ya Habari kutoka kwa umma. Kabla ya kufanyika, kongamano hili, sifa njema zote ni kwa Mwenyezi Mungu, lilisababisha mngurumo mkali.

lilivitikisa viti vya enzi vinavyougua; viti hivi vya enzi na mabwana wake wanaofuatilia vitendo vya chama hiki kitukufu, wanapaswa kujua ni wapi kiwango cha hisia za Ummah na ufahamu wake umefikia. Ama kwa waumini, nyoyo zao zilikuwa zikifurahi na kuburudika waliposikia msimamo wa chama juu ya usaliti wa usawazishaji mahusiano.

Kongamano hili kubwa lilikuwa na sifa mbili spesheli:

Ya kwanza: Vyombo vya habari vyenye busara, vilikuja kutangaza ujumbe mzito na wenye ikhlasi, juu ya kujiweka mbali na khiyana kubwa kuhusu suala la Palestina bila kuogopa lawama katika kazi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; neno la haki ndio silaha yake, silaha ambayo ni kali kuliko upanga mbele ya madhalimu.

Ya pili: ushiriki wa watu aina tofauti tofauti. Kongamano hili liliwakutanisha Waarabu na wasiokuwa Waarabu wenye rangi za ngozi na lugha tofauti tofauti, lakini kwa pamoja wanashuhudia ukweli, kwamba Ardhi Iliyobarikiwa ni mali ya Umma wa Kiislamu wote, sio mali ya Wapalestina au Waarabu peke yao na ni aya kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo haiwezi kuachwa au kuuzwa.

Miongoni mwa muhimu zaidi ya yale yaliyosemwa katika kongamano hili:

- Hotuba ya kwanza ilitolewa na Dkt. Mus'ab Abu Arqoub iliyopewa kichwa: "Palestina itakombolewa na Majeshi ya Waislamu," ambapo alisema: "Makubaliano yote, mikataba na usawazishaji mahusiano yako chini ya miguu ya Umma wa Kiislamu na hayana uzito. Usawazishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi pamoja na tawala hizo haimaanishi chochote, ni kama mtu anayeweka amani na yeye mwenyewe, na umbile la Kiyahudi na wasaliti hawa wamegundua hili. Wao ni kama mtu anayepeana mikono na bwana wake au kibaraka wa bwana wake, na Ummah umejiweka mbali nao”.

- Hotuba ya pili ilitolewa na Ustadh Ahmad Al-Qasas kutoka Lebanon yenye kichwa: "Kushindwa kwa Magharibi kuwashawishi Waislamu kuhusu Umbile la Kiyahudi" ambayo alisema:

"Magharibi ilifikiri katika karne ya ishirini kwamba Umma wa Kiislamu ulikuwa umeangamizwa, na kwamba ulikuwa umepata pigo baya ambalo halingewafanya warudi tena kwenye uhai, lakini ilishangaa baada ya hapo kwa sababu Uislamu umekuwa wa kwanza bali msukumo wa pekee wa Umma huu dhidi ya ukaliaji kimabavu, uvamizi wa kithaqafa na kifikra na njama zote zinazoandaliwa dhidi ya Umma huu”.                                       

- Hotuba ya tatu ilitolewa na Dkt. Ahmad Hassouna kutoka Jordan iliyopewa kichwa: "Ima Uongofu na Kukubaliwa au Kutelekeza na Kubadilishwa" ambapo alisema: "Mateso ambayo Ummah wa Kiislamu unapitia ni matokeo yasiyo epukika ya kuiacha kwa watawala ambao wanatawala kinyume na yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu. Hakuna shaka kwamba mapungufu katika kushikamana kwa Ummah na Shariah ni sababu ya adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ugumu wa maisha, ambayo ni dhahiri.

 (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ)

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7].

- Hotuba ya nne ilitolewa na Sheikh Nasir Ridha kutoka Sudan kwa anwani: "Jihadharini Msije Mkalipa Ushuru wa Jizya wa Usawazishaji Mahusiano, Enyi Watu wa Sudan." Ndani yake alisema: "Hapana tatu za Khartoum ambazo zilizinduliwa mnamo Septemba 1969 ni Khartoum hiyo hiyo mnamo Septemba 2020 inayokataa uhusiano wowote na umbile la Kiyahudi, isipokuwa uhusiano wa vita na mapigano. Na vijana wa Ummah nchini Sudan, kufuatia usambazaji wa Hizb ut Tahrir wa kipeperushi chake kilichokemea vitendo hivi vya hila na mikataba hii ya kufedhehesha iliyotiwa saini na watawala wa Imarati na Bahrain, waliwasiliana na chama hiki ili kusajili majina yao kujiunga na jeshi linalosonga ili kulitokomeza umbile la Kiyahudi, vivyo hivyo watu wa Sudan ”.

- Hotuba ya tano ilitolewa na Ustadh Sa'eed Fadl kutoka Misri Al-Kinana chini ya kichwa: "Umuhimu wa Misri Al-Kinana katika Suala la Palestina" ambapo alisema: "Umbile hili ovu ni kisu chenye sumu pembeni ya Ummah, na mwiba kooni mwake ambao ima Umma uutoe kwa kikohozi au utakufa; Ummah wa Uislamu hauajakidhiwa ufe na bila shaka utalitupa umbile hili. Umbile hili litaondolewa tu na Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, wakati wake umefika. Hivi karibuni tutatangaza na kuhamasisha majeshi ya Waislamu yanayoongozwa na jeshi la Misri kuikomboa Palestina yote, na Khilafah itaingia Al-Quds na itakuwa ni makao yake."

- Hotuba ya sita ilitolewa na Ustadh Abdullah Imamoglu kutoka Uturuki na kichwa: "Palestina sio Kadhia ya Waarabu, bali ni Kahida ya Uislamu." Ndani yake alisema: "Tunamuomba Mwenyezi Mungu awe shahidi wetu kwamba hatutakuwa miongoni mwa wale ambao wanakaa kimya juu ya mchezo huu wa usaliti, enyi Waislamu ambao nyoyo zao zinapuma kwa Al-Quds. Mnajua kwamba suala la Al-Quds sio jipya, kwani Msikiti wa Al-Aqsa na Al-Quds zimekuwa chini ya uvamizu kwa miaka sabini, na mnajua kuwa kadhia ya Palestina sio kadhia ya watu wa Palestina wala kadhia ya Waarabu peke yao, bali ni suala la Kiislamu, ni ardhi ya Isra na Mi'raj na hiyo imethibitishwa katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na ni Kibla cha kwanza cha Waislamu na amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu.”

Enyi Waislamu, je! Watawala wa Uturuki, ambao walikuwa kati ya wa kwanza kutambua uwepo wa umbile la Kiyahudi na ambao wanasema kuhusu umbile nyakuzi la Kiyahudi kwamba tunalihitaji katika Mashariki ya Kati, na kutumia kila fursa kuanzisha uhusiano wa karibu nalo, wanaweza wakuihami Palestina?!

- Hotuba ya saba ilitolewa na Sheikh Yusuf Makhraza kutoka Palestina yenye kichwa: "Wasifu wa Watawala wa Uovu" ambapo alisema: "Naapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwamba hakuna mungu mwingine ila Yeye, watawala wa Waislamu wako katika msimamo mmoja, wote wameshasawazishwa mahusiano na wote ni wapenzi wa Mayahudi, wakidai kuwa wao ni wenye ikhlasi. Naapa kwa Mwenyezi Mungu wao hawana ikhlasi, lakini badala yake wao ni mikia, hujifanya mbele ya Umma na kudai kwamba

usawazishaji wao wa mahusiano sio sawa na wa wengine. Kile walichokifanya ni zaidi ya usawazishaji na baada ya usawazishaji, bali wako kwenye uhusiano wa kawaida na Mayahudi."

- Hotuba ya nane, ilitolewa na Mhandisi Osama Al-Thuwaini kutoka Kuwait kwa anwani: "Kulikataa Umbile la Kiyahudi ni Kukataa Sababu za Kuundwa Kwake na Udhamini Wake." Ndani yake, alisema: "Huu ni mwaliko kwa kila mtu anayeipenda Palestina na kwa kila mtu anayependa kuiona ikikombolewa na chini ya kivuli cha Waislamu na utawala wa Uislamu, mwaliko kwa kila mtu anayepinga usawazishaji wa mahusiano na umbile la Kiyahudi, kukataa kwake kuwa na ufanisi, uzalishaji na kuendelea, kukataa usawazishaji ni lazima kuwe ni kukataa maamuzi ya uhalali wa kimataifa na kukataa uratibu na nchi kuu za kikafiri, haswa Amerika, upitishaji wa tawala katika nchi za Waislamu ambazo hazina nguvu isipokuwa juu ya watoto wa Waislamu. Kukabiliana na mashoka haya matatu ya uovu kunawezekana tu kwa kheri tatu; sheria ya Uislamu, jihad na dola ya Khilafah. ”

- Hotuba ya tisa ilitolewa na Dada Umm Abdullah kutoka Lebanon iliyopewa kichwa: "Jibu la Wanawake Waliokombolewa kwa Khiyana Kubwa Dhidi ya Ardhi ya Masra (Eneo la Isra')", ambapo alisema: "Watawala wa nchi za Kiislamu wamelegeza msimamo kwa Hapana kwa ujumla wake na yaliyomo ndani yake, kiwango na kiwango, na mwishowe kuwa: ndio. Na suala hilo likageuka kuwa mradi wa Mamlaka ya Palestina. Au mradi wa dola ya kisekula ya kidemokrasia ya Palestina hadi watetezi wake wakafikia ngazi ya chini kabisa. Hatusikii tena juu ya Hapana isipokuwa: hapana kwa Khimar (mtandio wa kichwani), hapana kwa uangalizi, hapana kwa uvumilivu, hapana kwa ugaidi, hapana kwa jamii ya kiume, hapana kwa mamlaka ya baba juu ya binti zake, na kile tunachosikia juu ya sheria za CEDAW ambazo zinataka kuhujumu nidhamu ya kijamii katika Uislamu huko Palestina."

- Hotuba ya kumi, ilitolewa na Sheikh Issam Ameira kutoka Palestina, ilikuwa na kichwa: "Watu wa Palestina wako Imara juu ya Uaminifu." Ndani yake alisema: "Enyi Waislamu, Palestina sio mali ya watawala hawa wasaliti, wala Al-Quds wala Al-Aqsa sio yao. Badala yake hawana uhusiano wowote na Umma huu hata kidogo, hawatokamani nao, na wala si katika wao. Hawatatoka katika wale ambao Mwenyezi Mungu (swt) atawakirimu kwa ukombozi wake, na hawatapata heshima ya takbira pamoja na wakombozi, na pande za usawazishaji mahusiano zitakuwa na hasara.

- Hotuba ya kumi na moja, ilitolewa na Ustadh Mundhir Abdullah kutoka Denmark yenye kichwa: "Kuzorota kwa Utendaji wa Kisiasa wa Magharibi," ambapo alisema: "Magharibi kafiri inajaribu kurekebisha mfumo huo ambao uliasisiwa juu ya mabaki ya Ummah . Uchi wa dola ya kitaifa ulifunuliwa, watu waliiasi, viti vya enzi vya madhalimu vikaanguka, na ufalme wa kidhalimu, wa kulazimishwa ukatetemeka. Kwa hivyo, Magharibi ilirudi na majeshi yake na nguvu zake ili kuzuia kuanguka kwa mfumo wake fisidifu."

- Hotuba ya kumi na mbili, ilitolewa na Ustadh Ahmad bin Hussein kutoka Tunisia yenye kichwa: "Ushindi uko pamoja na Vijana." Ndani yake alisema akiwaambia watawala: "Wacha kwanza wajiuzulu kwa pamoja kutoka kwa shirika la kimataifa ambalo liliitambua dola ya Kiyahudi na kusema inapenda amani, na pili kufuta maamuzi yote yanayotokana nayo, na tatu kuvunja vyama vyote na kila mtu aliyelihurumia umbile hili, au mtu yeyote ambaye, kama ilivyo hali nchini Tunisia, anasita kupinga usawazishaji mahusiano. Nne, kuchukulia mipaka kuwa batili, na tano kuhamasisha vikosi na maafisa katika majeshi yao. Hapo tu ndipo Ummah atachunguza suala lao; ima utawasamehe au la, hapo tu ndipo Khilafah (Ukhalifa) inaweza kupunguza adhabu yao nzito na kupata alama nzuri katika rekodi yao nyeusi."

Ama hotuba ya kufunga, ilitolewa na Mkurugenzi wa Afisi ya Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, Mhandisi Salah Eddine Adada, kwa anwani: "Ujumbe wa Hizb ut Tahrir katika Hali hii ya Uchungu" ambapo alikusudia toleo la chama hiki ambalo lilituma ujumbe kwa Ummah wa Kiislamu chini ya kichwa: "Leo Hii Imarati Na Bahrain Zinatia Saini ya Mkataba Pamoja na Dola ya Kiyahudi, Mkataba wa Uhaini Mkuu kwa Palestina Ambayo Ndipo Alipofikia Mtume (saw) Katika Safari Ya Isra Na Miiraj Yake. … Wanafanya Hivyo Hata Bila ya Kumhofu Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Waumini!"

Tunamwomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba msimamo wa Hizb ut Tahrir kwa suala la Palestina na maswala moto ya kieneo na kimataifa yatakuwa msaada kwa watu wenye ikhlasi wa Ummah huu, kuelewa tatizo, sababu yake, suluhisho na jinsi ya kulitekeleza .

*Imeandikwa kwa Ajili ya Gazeti la Ar-Rayah – Toleo 306

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 07 Oktoba 2020 09:08

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu