Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  16 Jumada I 1442 Na: 05 / 1442
M.  Alhamisi, 31 Disemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Amri Mpya ya Flemish ya Utambuzi wa Jumuiya za Kidini Maeneo ya Misikiti chini ya Mamlaka ya Serikali

(Imetafsiriwa)

Serikali ya Flemish ilipendekeza amri mpya kwamba kwa upande mmoja ni jaribio la kuifurahisha jamii ya Waislamu kwa kuitambua "rasmi" misikiti na kwa upande mwengine, kutekeleza udhibiti na "ufuatiliaji" ndani ya nyumba za ibada. Ingawa amri hiyo inazungumza kwa lafdhi za kijumla, ni wazi inalenga misikiti pekee.

Ule unaoitwa utambuzi "rasmi" wa misikiti umefungwa kwa masharti makali. Kulingana na amri hiyo, jamii za kidini nchini kama misikiti na bodi zao haziruhusiwi kupokea fedha kutoka ng'ambo. Zinatakiwa pia kutia saini taarifa ambayo inasema kuwa yaliyomo katika swala ya Ijumaa lazima yakubaliane na mipaka ambayo serikali ya kisekula inayapinga.

Kwa kuongezea, amri hiyo inachora mstari mbali zaidi kwa kuiambatanisha misikiti na “moslim executieve” (chombo kinachowakilisha huduma za ibada za Kiislamu na jamii ya Waislamu nchini Ubelgiji). Wakati wote chombo hicho cha utekelezaji kimekuwa hakina sifa nzuri kwa Waislamu. Nusu ya wanachama waliochaguliwa walikataliwa baada ya "ukaguzi wa asili" na serikali ya Flemish. Kwa hivyo, ni chombo ambacho wanachama wake wanakubaliwa na serikali ya Flemish na sio na Waislamu.

Kwa kufanya hivyo, serikali ya Flemish hailazimishi tu ni nani anawakilisha jamii ya kidini ya Waislamu, inaidhibiti misikiti kupitia hiyo. Waziri wa Sheria Vincent van Quickenborne ambaye ni mtetezi wa ushirikiano pamoja na chombo hicho cha utekelezaji cha Waislamu alikisifu kama ifuatavyo. "Ni matarajio yangu, pamoja na mawaziri wa nchi wanachama, kuutambua Uislamu endelevu katika nchi yetu ambao unakata uhusiano wote nje ya nchi na kutoa nafasi kwa vijana wengi ambao wanataka kutekeleza imani yao kwa njia ambayo inawiana na jamii yetu.”

Uislamu unaonekana kama tatizo, kwa hivyo misikiti ambayo ni kielelezo cha Uislamu lazima ilindwe. Wanataka kufikia hili kwa "kuitambua" kwanza ili iwe rahisi kuishawishi kuamuru "Uislamu" unaokubaliana nao.

Ni wazi kwamba kitendo, amri hiyo inalenga nyumba za ibada za Kiislamu na sio jamii zengine za kidini. Mbali na ukweli kwamba ni jaribio la kijanja la kuwapotosha Waislamu, pia ni la kibaguzi zaidi.

Ushauri wetu kwa Waislamu wenye ikhlasi ni kama ufuatavyo: kataeni amri hii ambayo lengo lake ni kuidhibiti jamii ya Waislamu. Pia inafungua mlango wa kuitia hatiani misikiti ambayo haitaki kutambuliwa ili kuishinikiza.

Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: Uhuru, Usawa, Udugu na Unafiki »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu