Jumanne, 09 Ramadan 1445 | 2024/03/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Wapalestina nchini Lebanon wako kati ya Shinikizo la Kimaisha na Hasara ya Kisiasa!!

(Imetafsiriwa)

Kwa zaidi ya miaka sabini, Wapalestina nchini Lebanon wanateseka kutokana na minyororo ya hali ngumu, na udhalilishaji katika matibabu na kushughulikiwa kwao! Na kupitia kutazama kwa umakini tatizo la Wapalestina nchini Lebanon, na wale wanao shawishi uwepo wao na maisha yao huko, yafuatayo yako wazi:

Kwanza: Mgogoro wa umbile la Lebanon: Umbile la Lebanon ambalo wakoloni wa Kifaransa waliliunda kuwa ni umbile la kimadhehebu, lina utata katika kuutazama uwepo wa Wapelestina, na mara kwa mara wasiwasi wao kuhusiana na mabadiliko ya idadi ya watu, ambapo Wapelestina wanahesabiwa katika mantiki ya kimadhehebu nchini Lebanon kama uwepo wa Wasunni. Mtazamo huu uliakisiwa katika kuamiliwa vibaya kwa maisha ya Wapalestina, kupitia kuzingirwa katika kambi na kuzuiwa kwa haki za kibinadamu, ya kufanya kazi na kumiliki, na kisha dola ya Lebanon ikakataa kabisa kuongeza athari yake ndani ya kambi chini ya visingizio vya uongo. Hawa msimamo huu rasmi wa Lebanon unazipa nguvu amri za Amerika, sambamba na mtazamo wake wa hivi karibuni wa uwepo kwa umbile la Kiyahudi katika ardhi ya Palestina, kisha hivi karibuni likaja tatizo la kisiasa na kiuchumi, ambalo kiuchumi limejitokeza katika watu wa Lebanon, na limekuwa na athari ya kuzidi kwa hali za maisha ya Wapalestina ndani yake.

Pili: Mgogoro wa UNRWA: Nchi kuu ambazo zinaunga mkono na ziko nyuma ya uwepo wa umbile la Kiyahudi katika ardhi ya Palestina, kupitia azimio la kigawanya nambari 181 lililotolewa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo 1947 M, ndizo zizo hizo zilizo asisi UNRWA Shirika la Msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina, kwa mujibu wa azimio nambari 302, lililotolewa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lenyewe mnamo 1949 “kwa lengo la kupeana misaada ya moja kwa moja na mipango ya ajira kwa wakimbizi wa Kipalestina”, mpaka suluhu ipatikane kwa hali yao: hata hivyo, kwa kukosekana suluhu hiyo, Baraza Kuu - limerudia mara kwa mara – kujadidiwa kwa mamlaka ya UNRWA, mara ya mwisho waliliongezea mamlaka ya kufanya kazi hadi Juni 30, 2023. Bila shaka katika kipindi cha miaka sabiini na mbili, UNRWA, ambayo iliundwa kushughulikia hali ya isiyo ya kawaida ya hifadhi, sasa imekuwa sehemu ya uhalisia (wa kimaumbile) wa maisha ya Wapelestina, na huku nchi kuu – haswa Amerika – zikidhamini suluhu ambazo zinaendeleza uwepo na makaazi ya Wayahudi, serikali katika ulimwengu wa Kiislamu zinasaidia katika dori ya kuwashinikiza wakimbizi kuondoka katika kambi na kuwafungulia mlango wa uhamiaji ili kusambaa pande zote za ulimwengu. Wakati huo huo, rasilimali za UNRWA zimekuwa haba, na kuna agizo kwa usimamizi wa UNRWA wasijishughulishe kidhati na mambo ya maisha ya Wapalestina, mara nyingine hata kwa kufadhili, na hili limedhihiri katika utendakazi wa watunzaji katika idara yake, licha ya kuwa na nguvu zote za kisheria, na mifano iko mingi, iliyo dhahiri zaidi ni:

- Uchelewa waziwazi katika kupeana msaada kwa wakimbizi katika janga la maambukizi ya Korona, licha ya ukweli kwamba UNRWA inazo fedha, na nguvu za kubadilisha mipango ya utendakazi katika uwepo wa hali hii ya dharura.

- Kufeli katika kuchukuwa tahadhari mwafaka za kiafya katika kukabili Korona, kama ilivyo shuhudiwa katika shutma kwa Waziri wa Afya wa Lebanon kwa utendakazi wake, na kashfa ya kupeana makaazi ya karantini katika shule mmoja ndani ya kambi ya Galilee, ambayo yamekosa viwango vya chini vya usalama wa kiafya.

- Pendekezo kwa serikali la kuzichukua fedha za UNRWA kutokana na mgogoro wa kifedha, na kutoitumia UNRWA mamlaka yake kimataifa katika kuchukua hatua yoyote muhimu kukomesha uporaji wa fedha hizi, kupitia benki za Lebanon na wanasiasa wafisadi. Imeripotiwa tangu Oktoba 2019, miradi ya UNRWA imesitishwa; miradi hii ambayo inaajiri maelfu ya wafanyikazi na waajiriwa wa Kipalestina, na ambayo soko linanufaika kwayo, ndani na nje ya kambi.

- Pendekezo kwa wanasiasa wa Lebanon kuiachia mamlaka ya jeshi na usalama faili ya kambi, ambao inaongeza ukiukaji dhidi ya wakimbizi katika vituo vya uangalizi, kwa ukosefu wa hatua yoyote ya kivitendo kwa kauli mbiu ya UNRWA “ulinzi” hadi hivi karibuni kambi zimekuwa milango, ambayo inafungwa wakati wa amri ya kutotoka nje katikati ya janga la Korona, kana kwamba watu ni wafungwa, ama mifugo waliofungiwa katika maboma yao usiku!!

- Kufeli kusitisha ukiukaji wa haki za kibinadamu dhidi ya wakimbizi, haswa haki ya kumiliki na kufanya kazi, ambayo iko na athari kubwa katika kupunguza shinikizo la idadi ya watu ndani ya kambi, na kuhakikisha maisha endelevu, mbali na mantiki ya msaada na kujikimu.

- UNRWA haipeani mpango wa maendeleo yoyote fanisi kwa wahisani na kwa wale wanao shughulikia mambo ya kisiasa na kiuchumi ndani ya Lebanon, kuzipangilia kambi katika hali nzuri na salama.

- Timu ya kiidara ya kimataifa ambayo kwa sasa inasimamia UNRWA inatekeleza kazi za kawaida pekeyake na haifanyi maamuzi yoyote ya kimikakati, kukabiliana na kuzorota kwa hali ya kibinadamu.

- Kusalimu amri kwa Shirika katika kutawaliwa na makundi, na kuruhusu makundi haya kuharibu mchakato wa kuajiri, ambako kumesababisha mantiki ya mapendeleo, yaliyo haribu utendakazi na kuwanyima ajira watu wengi waliohitimu. 

Tatu: Mgogoro wa makundi ya Kipalestina: ambao ulianza kwa kunyanyua kauli mbiu za ukombozi wa Palestina yote, na kumalizikia kwa uidhinishaji wa suluhisho la dola mbili, ambapo bila shaka, kivitendo iliachana na kile kilichoitwa "haki ya kurudi", ingawa ilihadaa kwa kubaki maneno tu. Wakimbizi wa Kipalestina nchini Lebanon wengi wao wametoka sehemu ya ardhi Iliyo Barikiwa ya Palestina, ambayo umbile la Kiyahudi limebuniwa, kinachoitwa ardhi ya 48, ambayo makundi haya yanatambua kama haki ya Wayahudi! Hivyo wapi watarudi?!!

Makundi haya sasa hayana maono kwa Wapalestina waliopo nchini Lebanon, wala hawapo na Wapalestina wanaobakia nchini Lebanon kwa kisingizio kuwa wanadai kuhifadhi haki ya kurudi, ambayo kivitendo na uhalisia inakataa kutambua uwepo wa umbile la Kiyahudi, wala hawapo kwa ajili ya utoaji makaazi mapya katika nchi ambazo Wapalestina wanaishi humo zaidi katika umri wao wote, wakati wameridhika na makaazi ya Wapelestina ndani ya Ulaya na Amerika!!

Hivyo basi, kwa nini makundi haya yameridhika, kisha, pamoja na udhalilishaji wote huu wa Wapalestina nchini Lebanon, udhalilishaji wa kuwanyima haki za kibinadamu na bila ya kuonyesha upinzani kwa serikali? Jibu ni, hawana mradi wala maono kwa suluhu ya watu hawa, isipokuwa wanatumia migongo yao, wakiinua njia yao kama kauli mbiu ili kujaza mifuko na matumbo, na kudumisha uhusiano wao na wanasiasa wa Lebanon, washirika katika njama na ufisadi. Hivyo muelekeo wa kisiasa wa mtoto wa Palestina, ambaye amekuwa akikimbia nyuma ya maazimio ya kimataifa na kila lililo rasmi, umepotea na hivyo hakufika popote.

Kutokana na haya, sisi katika Hizb ut Tahrir tunawaambia watu wetu waliopo Palestina kwa ujumla, na haswa walioko Lebanon: azimieni maono yenu kuelekea hatma yenu, kwani hatma yenu haitengani na hatma ya Waislamu wote, ambao wanataabika na dhulma za watawala vibaraka wa Magharibi na ambao dola ya inayo waunganisha ilivunjwa, ambao wamewahifadhi mayahudi katika kivuli chao, na nyuma yao ni Wakoloni, ambao hawangethubutu kubuni umbile lolote katika ardhi ya Palestina na kuwafukuza humo. Palestina kama Lebanon, Syria, na Misri, zote ni nchi za Waislamu pamoja na nchi yenu, hivyo msione aibu kuishi humo, kwani mko na thamani kubwa kuliko vibaraka, na kukombolewa kwa Palestina, Masra ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ni jukumu la kila Muislamu katika uso wa dunia hii, lakini kuishi katika ardhi ya Ash-Sham haswa, na kutua kwenu ndani yake, na kusubiri katika huzunu na tabu, yapo malipo makubwa, Mwenyezi Mungu akipenda, kwa sababu hili linagonga njama za makafiri ili kuwatoa katika Ash-Sham kuwaeka mbali na makaazi ya Waislamu, Bayt al-Maqdis na vitongoji vyake.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ]

 “Enyi mlio amini! Subirini na shindaneni kusubiri, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili mpate kufanikiwa.” [Al-i-Imran: 200]

H. 9 Ramadan 1441
M. : Jumamosi, 02 Mei 2020

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Lebanon

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu