Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 21 Rabi' I 1447 | Na: HTS 1447 / 31 |
M. Jumamosi, 13 Septemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kama sehemu ya kampeni iliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan kukwamisha mpango wa kutenganisha Darfur, Hizb ilifanya Visimamo katika miji kadhaa ya Sudan
(Imetafsiriwa)
Kama sehemu ya kampeni iliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayat Sudan kukwamisha mpango wa Marekani wa kuichana nchi hii kwa kuitenganisha Darfur na Sudan, hizb ilifanya kisimamo katika Msikiti wa Al-Aqit mjini Gadharef mnamo siku ya Alhamisi, Septemba 11, 2025 baada ya swala ya Ijumaa Septemba 12, 2025, miji kadhaa mikubwa ya Sudan ilifanyika visimamo, pamoja na misikiti mikuu ya Sudan yote. Shawak, Singa, Rabak, Madani, Abbasiya, Taqli, Khartoum (Kalakila na Dukhainat), na misikiti miwili mjini Omdurman.
Wakati wa visimamo hivyo, mashababu waliinua mabango mengi yaliyoandikwa:
1- Tibueni mpango wa Amerika kutenganisha Darfur
2- Tibueni mpango wa mipaka ya damu na kuzuia kujitenga kwa Darfur
3- Kadhia ya umoja wa dola ni kadhia nyeti, na lazima hatua za uhai au kifo zichukuliwe kuhusiana nayo.
4- Simamisheni Khilafah ili kung'oa athari za Magharibi kafiri kutoka nchi yenu
5- Hakika Imamu ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujihami kwake
6- Ikamateni mikoni ya vibaraka na wasaliti na kuzuieni kujitenga kwa Darfur
7- Hamasisheni nguvu za wenye ikhlasi ili kutibua mpango wa kutenganisha Darfur
8- Vikosi vya jeshi katika serikali lazima viungane pamoja
9- Waunganisha wanamgambo wote ndani ya jeshi moja na mukomeshe kuleta machafuko na kuisambaratisha nchi.
10- Ikamateni mikono ya vibaraka na wasaliti na musiiache Darfur kama mulivyoiacha Sudan Kusini hapo awali.
11- Zuieni kujitenga kwa Darfur kabla ya kujiunga na Sudan Kusini
12- Enyi watu wa Sudan! Nyinyi mnao uwezo wa kutibua njama ya kuitenga Darfur, basi simameni mbele ya Mwenyezi Mungu, kwa utiifu.
13- Watu wa El Fasher wanauawa kwa vita na njaa, basi fanyeni haraka kuwaokoa.
14- Kuanzishwa kwa serikali sambamba, ni mpango wa Marekani wa kutenganisha Darfur, basi zuieni kutekelezwa kwake.
15- Amerika inaharakisha mpango wake wa kutenganisha eneo la Darfur, na hakuna wokovu isipokuwa kwa kuufanya umoja wa dola kuwa suala la nyeti.
Waumini pia walihutubiwa baada ya kutoka misikitini kwa wito wenye kichwa: “Enyi watu wa Sudan, msiiruhusu Marekani kuichana nchi yenu na kutenganisha Darfur.” Wito huo ulisikika katika kila msikiti na mshababu wa Hizb ut Tahrir. Katika mji mkuu wa utawala, Port Sudan, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan alihutubia umati wa watu, akielezea kwamba mataifa yana maswala nyeti maishani mwao, yaani maswala ambayo ni lazima kuchukua hatua moja: uhai au kifo katika yake. Aqida ya Kiislamu imefafanua masuala yetu nyeti, ikiwemo umoja wa dola na umoja wa umma. Pindi tulipoweka suala hili kwenye daraja ya chini kabisa, Amerika iliweza kutenganisha Sudan Kusini. Sasa inatafuta kuasisi dola mpya kwa kuzingatia mipaka ya umwagaji damu, na inatayarisha hatua ya kujitenga kwa Darfur kwa kutumia mazingira sawa na kusini.
Wito huo uliwataka watu wa Sudan kuamka ili kukwamisha mpango wa Marekani katika kumtii Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Wahudhuriaji katika visimamo vyote hivyo, vilivyofanywa katika miji mbalimbali ya Sudan, walijibu kwa takbir na tahlil, wakisifu mwitikio wa Hizb ut Tahrir kwa masuala haya na onyo lake la mara kwa mara kwa umma juu ya hatari zinazowazunguka.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Wilayah Sudan
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
-
Click to open image! Click to open image!
https://hizb-uttahrir.info/sw/index.php/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari/sudan/4958.html?print=1&tmpl=component#sigProId0aa942fbbd
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |