Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kadri Wakati Unavyosonga Mbele, Thaqafa ya Kimagharibi Unarudi Nyuma

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 9 Oktoba, Gazeti la ‘the Guardian’ liliripoti kwamba mkuu wa shirika la kutoa misaada la Waislamu wa Uingereza Shaista Gohir, alikuwa na 'wasiwasi mkubwa' huku uhalifu wa chuki dhidi ya Uislamu ukiongezeka kwa theluthi moja kulingana na takwimu za hivi punde za serikali. Alisisitiza kuwa hata takwimu hizi zinazosumbua pengine ni ‘sio halisi’ kwani matukio mengi hayaripotiwi.

Shaista Gohir anaongoza shirika la kutoa misaada lenye makao yake jijini Birmingham, ambalo ndilo shirika pekee la kitaifa la kutoa misaada la wanawake wa Kiislamu nchini Uingereza. Aliongeza kuwa, "Tuna wasiwasi mkubwa, wa kina. Sikumbuki wakati katika harakati zangu zote ambapo Waislamu wengi kwa pamoja wana wasiwasi mkubwa na hofu na msongo wa mawazo. Nimesikitishwa sana na serikali, wako kimya,"

Yeye pia ni mshirika wa benchi na wakuu wa Mtandao wa Wanawake wa Kiislamu. Amewakosoa mawaziri kwa kuwa "kimya" na kutaka jibu la hadharani la serikali kwa data hizo.

Takwimu za Wizara ya Mambo ya Ndani zilionyesha kwamba uhalifu wa chuki uliorekodiwa nchini Uingereza na Wales ulikuwa ukiongezeka kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu, ikiwemo ongezeko la uhalifu wa ubaguzi wa rangi na kidini. Nchini Uingereza na Wales, ambapo watu milioni 3.9 wanajitambulisha kuwa Waislamu, uhalifu wa chuki dhidi ya Uislamu uliongezeka kutoka makosa 2,690 hadi 3,199 katika miezi 12 hadi Machi 2025.

Katika mwaka unaoishia Machi 2025, kulikuwa na uhalifu wa chuki 137,550 uliorekodiwa na polisi nchini Uingereza na Wales. Uhalifu wa chuki za rangi uliongezeka kwa asilimia 6 kutoka mwaka uliopita, na uhalifu wa chuki unaochochewa na dini ulikuwa juu kwa 3% kutoka 6,973 hadi 7,164 - idadi kubwa zaidi ya mwaka katika rekodi.

Misikiti na vituo vya jamii kote Uingereza viliripoti msururu wa mashambulizi dhidi ya waumini na mali mnamo Julai 2024 baada ya uvumi uliochochewa na mitandao ya kijamii kudai kwamba mshambuliaji wa Southport alikuwa Muislamu. Baadaye iliibuka kuwa Axel Rudakubana, ambaye aliwaua wasichana watatu wachanga, alizaliwa katika familia ya Kikristo na alikuwa na fasihi yenye chuki dhidi ya Uislamu.

Kwa vile mamilioni ya Waislamu duniani kote bado wanaziona nchi za Magharibi kama ngome ya uhuru na matumaini, udanganyifu unaochangiwa na vyombo vya habari vya ukoloni, hii ni ishara ya kuamka kutoka kwa "ndoto" ya kiliberali. Ukweli ni kwamba wale wanaoishi chini ya "mapendeleo" ya Magharibi wanajaribu kuishi katika jinamizi la mienendo ya kijamii ambayo ni eneo la vita kwa wanawake wa Kiislamu.

Tunachopaswa kutambua ni kwamba hakuna fursa ya kazi, malipo ya fedha au jukwaa la elimu litaruhusu wanawake wa Kiislamu kufanya kazi katika viwango vya juu ikiwa hawana usalama na amani, ambayo ni hitaji la msingi la binadamu.

Lazima tukumbuke kwamba sheria na kanuni za siasa huria ni nyumba ya karata ambayo haimlindi mtu yeyote. Hakika Mwenyezi Mungu (swt) ndiye mlinzi wa Waumini.

[هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ يَعْلَمُ مَا يَلِجُ فِي الْأَرْضِ وَمَا يَخْرُجُ مِنْهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ السَّمَاء وَمَا يَعْرُجُ فِيهَا وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ]

“Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita; kisha akakaa vyema juu ya enzi. Anayajua yanayo ingia katika ardhi na yanayo toka humo, na yanayo teremka kutoka mbinguni, na yanayo panda humo. Naye yu pamoja nanyi popote mlipo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona mnayo yatenda.” [Surah Hadid: 4]

Lakini hii inaweza tu kufanywa chini ya mamlaka sahihi ya Kiislamu ya Dola ya Khilafah chini ya sera zilizotabanniwa na Maswahaba watukufu (ra).

Hatuwezi kuwa na masuluhisho nusu; hatuwezi kuwa na uwiano wa kivipande na Waislamu. Ni lazima tu tujitolee kwa ajenda safi na kamilifu iliyo wazi katika Quran na Sunnah.

Tunachokiona katika ripoti ya ‘the Guardian’ ni upanuzi tu wa mashambulizi ya kimataifa dhidi ya Uislamu ambayo yanahofiwa kuwa suluhisho la pekee halisi la ukandamizaji unaokabiliwa na nguvu za Iblis (shetani) na maadui wa haki.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohamed
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.