Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hakuna Wokovu kwa Watu wetu nchini Sudan
Wala Amani au Usalama isipokuwa chini ya Mfumo wa Uislamu

(Imetafsiriwa)

Katika yote historia, wingi wa makabila nchini Sudan kamwe haukuwa sababu ya mizozo na vita. Bali, kilichosababisha haya ni mapambano makali ya kisiasa na kijeshi baina ya dola za kikoloni na vibaraka wao, ambayo yaliharibu mazao na vizazi, hasa baada ya wao kuigawanya nchi na kupanda mbegu za fitina na mapigano ya kikabila na kimapendeleo, sawa kabisa na yale yanayotokea leo na kwa usahihi kabisa kama ilivyotokea katika siku za mwanzo za Ujahiliya. Tangu Uislamu utoweke na dola yake ivunjwe, watu waliregea katika hukmu za kijahilia, wakipigana kwa msingi wa ukabila, ambao Mtume (saw) aliuharamisha na kuonya vikali dhidi yake, kama alivyosema: «مَنْ قَاتَلَ تَحْتَ رَايَةٍ عِمِّيَّةٍ يَدْعُو إِلَى عَصَبِيَّةٍ أَوْ يَغْضَبُ لِعَصَبِيَّةٍ فَقِتْلَتُهُ جَاهِلِيَّةٌ»  “Mwenye kupigana chini ya bendera ya upofu, akilingania uasabiya (ukabila), au kughadhibika kwa ajili ya uasabiya, kisha akauwawa, kifo chake ni cha kijahiliya.”

Kwa hiyo, watu wa Sudan lazima watambue kwamba mazingira ya kisiasa yaliyopo, ambayo yanakosa utambuzi wa fikra ya kisiasa na yananasibishwa na makafiri wa Magharibi, ndiyo sababu ya migogoro na matatizo. Haya ni matokeo ya mgawanyiko wa kisiasa kwa msingi wa kikabila unaochukiza, kwani serikali mtawalia zimetumia makabila kama kichocheo cha mizozo yao. Zilifuata njia ya vyama katika ubaguzi wa kikabila. Kilichotokea na kinachoendelea huko Darfur ni mfano wa wazi kabisa wa hili, ambapo baadhi ya makabila yanaunga mkono mavuguvugu ya waasi yenye silaha, na hivyo kusababisha serikali kwa upande wake kuyapa silaha makabila yanayoiunga mkono na kuyatumia kupambana na waasi. Kwa mwelekeo huu, serikali mtawalia ziliamiliana na maeneo yote ya Sudan, na kusababisha hali ya taharuki na wasiwasi katika maeneo yote, hadi nchi nzima ikawa pipa la baruti tayari kulipuka wakati wowote. Wakati huo huo, wenye kupata hasara pekee katika vita na mapigano haya ya kikabila ni wananchi wenyewe. Wanaendelea kulipia gharama kubwa katika damu na maisha yao. Cha kusikitisha ni kwamba wao si chochote ila zana duni zinazotumiwa kuuana wao kwa wao!

Uislamu umeitukuza sana damu ya Muislamu, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

[وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِناً مُّتَعَمِّداً فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِداً فِيهَا وَغَضِبَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَاباً عَظِيماً]

“Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.” [An-Nisa:93]. Na Mtume (saw) akasema: «لَزَوَالُ الدُّنْيَا أَهْوَنُ عَلَى اللَّهِ مِنْ قَتْلِ مُؤْمِنٍ بِغَيْرِ حَقٍّ» “Kuangamia dunia nzima ni sahali mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kumuua muumini pasi na haki.” Na akasema (saw) pia: «إِذَا الْتَقَى الْمُسْلِمَانِ بِسَيْفَيْهِمَا فَالْقَاتِلُ وَالْمَقْتُولُ فِي النَّارِ» “Pindi Waislamu wawili wanapokutana kwa panga zao, muuaji na mwenye kuuliwa wote wako Motoni.”

Basi tuko wapi katika kumfuata Mtume (saw)? Na tuko wapi katika kukiregelea Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyesema:

[يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوباً وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ]

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.” [Al-Hujurat:13].

Hivyo, ni lazima tujitahidi kukomesha uvujaji damu yetu unaoendelea na kusitisha mpango wa makafir wa Magharibi kwa kufuata amri za Mwenyezi Mungu na Mtume Wake – yaani, kuhukumu kwa Uislamu. Hili tu ndilo litakalokomesha mapigano ya kikabila, kuweka hali shwari, na kumaliza uvurugaji wa maisha ya watu wasio na hatia kwa kurudi kwenye Uislamu na kufuta kila kitu kinachogongana nao.

Hata hivyo, Uislamu hauwezi kusimamishwa isipokuwa kwa mamlaka, maana yake kwa dola inayoutabikisha na kuubeba duniani kwa njia ya da’wah na jihad, ambayo ni Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Ndani yake, utawala ni jukumu, sio ngawira, kutekeleza wajibu wa uchungaji kuanzia afya, elimu, usalama, kuwezesha watu kulima na kutengeneza bidhaa, na kufungua njia za malisho ili msuguano usitokee kati ya wakulima na wafugaji. Kwa hivyo, inakata mikono ya wachochezi bila kusita na kukomesha madhihirisho yote ya mauaji, uchomaji moto, na uporaji kwa kutekeleza hudood (sheria za adhabu) kwa wale wanaovunja sheria.

Dola ya Khilafah pekee ndiyo yenye uwezo wa kuwayeyusha watu pamoja kama Ummah mmoja kwa msingi wa Uislamu mtukufu, si kwa msingi wa ubaguzi wa rangi, ukabila, au utaifa. Inatawala kwa sheria za Uislamu na mamlaka yake, mamlaka yale yaliyowaunganisha Waislamu na kuwafanya kuwa ndugu wenye upendo kwa Mwenyezi Mungu, kuwaunganisha Abu Bakr Muarabu, Bilal al-Habashi, Salman al-Faresi (Mfursi), Suhaib Mrumi, Hamza Mqurayshi, na Mu’adh Answari...

Hakika Uislamu huu mtukufu ndio pekee katika historia ya mwanadamu ulioyayusha watu, rangi na makabila kuwa Umma mmoja. Haukuishia Madinah bali ulienea katika Bara Arabu. Ukombozi wa Kiislamu ulieneza Uislamu: Waislamu walifungua Iraq, iliyokaliwa na Wakristo, Mazdakite, Majusi wa Kiarabu na Wafursi; uliifungua Fursi iliyokaliwa na wasio Waarabu, Mayahudi, Warumi; ulifungua ash-Sham mkoa wa Kirumi uliokaliwa na Wasyria, Waarmenia, Warumi, Waarabu; ulifungua Afrika Kaskazini ya Mabarbera; ulifungua Sindh, Khwarezm, Samarkand, na Andalusia – na kuwayeyusha watu hawa wote kuwa Ummah mmoja bila tofauti yoyote. Nuru ya Uislamu ilienea duniani kote kwa muda mfupi kwa sababu Uislamu unaamuru kuangalia mambo ya raia kwa ubinadamu, sio kwa ubaguzi wa rangi, madhehebu, au matabaka. Sheria za Uislamu zilitekelezwa kwa kila mtu, hivyo wote wakawa raia wa Dola ya Kiislamu, hakuna tofauti kati ya Muislamu na asiye Muislamu, na hakuna aliyemkosea mwengine. Yalipotokea, Uislamu uliyazuia na kuyaadhibu, kwani Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَى أَلَّا تَعْدِلُوا اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَى]

“Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu.” [Al-Ma’idah:8].

Watu wote ni sawa mbele ya mahakama, na mfumo wa utawala unaamuru umoja wa majimbo ya dola na kuhakikisha mahitaji ya kila mkoa bila kujali mapato yake kwa Hazina, na kuufanya mchanganyiko kutoepukika kati ya watu wote wa dola.

Hivyo, ni wajibu kwa kila Muislamu mwanamume na mwanamke kufanya kazi ya kusimamisha faradhi hii kubwa isiyokuwepo, jengo la Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

[إِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ]

“Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.” [Al-Anbiya:92]

#أزمة_السودان

#SudanCrisis

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Rana Mustafa

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.