- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Marekani inatia Mikono yake Michafu katika Kila Mzozo; Sudan sio Tofauti
(Imetafsiriwa)
Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, Amerika imejidhihirisha kama mpangaji mkuu nyuma ya baadhi ya mizozo ya kunyama na ya ghasia zaidi kote duniani. Kutoka Urusi na Ukraine hadi India na Pakistan hadi China na Taiwan hadi Syria, Iraq, Afghanistan, Yemen, Kenya, Mali, Cameroon, na hii ni mifano michache tu! Hata hivyo, hakuna kilichoifichua Marekani zaidi ya uungaji mkono wake usio na haya na ushiriki wake katika mauaji ya halaiki yanayotokea Gaza dhidi ya watu wa Palestina. Kabla ya uvamizi, kuzingirwa kabisa, na kuangamizwa kwa Gaza, watu wengi hawakujua jinsi serikali ya Marekani ilivyokuwa chafu na jinsi wanavyoweza kuwatembeza wachezaji kama poni kwenye bao la chess. Pazia liliondolewa katika udanganyifu huu licha ya miongo mingi ya propaganda za Marekani ambazo zilikuuza wazo kwamba walihusika tu kukuuza demokrasia, kuondoa madikteta, kutekeleza sheria za kimataifa, au kulinda haki za binadamu, nk. Pamoja na mashambulizi ya ghasia dhidi ya watu wa Palestina, ilionekana wazi sana kwamba kwa kweli ni Amerika ambayo hutoa silaha na msaada wa kifedha kwa makundi na serikali zinazopigana (wakati mwengine pande zote zinazo zozana), Marekani ndiyo inayozitupilia mbali sheria za kimataifa kwenye tope, Marekani ndiyo inayoharibu, kutesa, kubaka na kuua, na Marekani, huku wakidai kuwa watetezi wa haki, kwa kweli ndiyo inayotekeleza vitendo vya unyanyasaji dhidi ya raia wasio na hatia kila siku ulimwenguni. Wao hawaungi mkono tu umbile la Kizayuni, bali madikteta, watawala haramu, wanamgambo, na makundi katika pembe nne za dunia. Kwa utambuzi huu, tunapaswa kuelewa kwamba vurugu na machafuko yanayotokea nchini Sudan hayana tofauti na wachezaji wa kimataifa na hayafanyiki ndani ya ombwe.
Serikali ya Sudan daima imekuwa mikononi mwa dola yenye nguvu ya kimataifa, kuanzia kwa Uingereza, ambayo iliandaa "uhuru" wao mwaka 1956, hata hivyo, punde tu ilibadilisha mkono kwa Marekani kufuatia kuinuka kwake kama dola kuu duniani. Kwa sababu nyingi ikiwemo rasilimali za thamani sana za Sudan na eneo la kimkakati la kisiasa la kijiografia, Mataifa ya Magharibi yanajaribu mara kwa mara kupata kipande chao cha mkate. Nchi kama vile Urusi, China, Uingereza na Ufaransa hujaribu kutia mguu kwa kutumia wakala wao wenyewe, kama vile Uingereza iliyo na UAE, au kwa kutumia mamluki kama vile Urusi kupitia kundi la Wagner, au kutumia ushawishi wa kiuchumi kama China. Hata hivyo, hakuna aliyeweza kumshinda bwana wa vibaraka, Marekani, katika mchezo wao wa ukoloni mamboleo. Marekani kwa upande mwingine inatumia mbinu mbalimbali ili kudumisha mshiko wake juu ya Sudan, kama vile, kuunga mkono makundi mbalimbali ya kijeshi huko na kufanya hila mbalimbali za kichinichini ili kuzuia serikali ya kiraia kuchukua madaraka nchini humo. Marekani pia hutumia washirika wake kama vile Saudi Arabia, UAE, Misri, na Uturuki kama "wachezaji wa kati," kuwaruhusu kuwa na dori katika eneo hilo, mradi tu ibakie ndani ya mipaka ya sera ya Marekani.
Vuguvugu la Anyanya, Kusini, lilikuwa ni kundi ambalo lilizaliwa kutokana na vita vya kwanza vya wenyewe kwa wenyewe na lilizalisha serikali ya Marekani na wamishonari wa Kikristo walioungwa mkono na Vuguvugu la Ukombozi la Sudan Kusini. Amerika iliweka msingi wake wa hatimaye kujitenga kwa Sudan Kusini na udhibiti wake kupitia uungaji mkono wake wa Vuguvugu la Ukombozi wa Watu wa Sudan, pamoja na uhusiano wa kihaini wa Omar al Bashir nao, na ushiriki wao katika kuongoza Mkataba wa Naivasha. Baada ya kuona mpango wake wa kutenganisha Sudan Kusini, Amerika ilielekeza macho yake katika eneo la Darfur, ambalo hapo awali lilikuwa linatumiwa na Uingereza kama njia ya kuweka mabaki yoyote ya udhibiti ambayo hapo awali ilikuwa nao kwa kuchochea vita huko. Walakini, kama kawaida, Marekani hutumia ushawishi wake, pesa, na vitisho kuzuia mipango yoyote inayoingilia mipango yake yenyewe. Leo, Amerika inadumisha mamlaka yake kupitia wanaume wa pande zote mbili wanaopigana uwanjani; Abdel Fattah al-Burhan, mtawala aliyeko tangu mapinduzi na mkuu wa Vikosi vya Wanajeshi wa Sudan, pamoja na, Mohammad Hamdan Dagalo (aka Hemedti), Jenerali wa Vikosi vya Msaada wa Haraka. Marekani inadhibiti SAF kupitia wakala wao, Saudi Arabia, ambaye hutuma fedha kwa SAF na RSF, kupitia kibaraka wao, Hemedti. Ingawa utiifu wa mtawala wao uko kwa Uingereza, UAE, imeendelea kuunga mkono RSF na kibaraka wa Marekani Hemedti kwa matumaini ya kupata ushawishi fulani juu yake na wafuasi wake ikiwa mpango wa Marekani utazaa matunda na Sudan itagawanyika tena. Ni aibu ilioje kwamba Burhan pamoja na Hemedti wanapigana kwa damu ya watu wa Sudan bila sababu nyingine isipokuwa kutumikia maslahi ya Marekani ya kutenganisha Darfur na Sudan, kama ilivyokuwa wakati ilipotenganisha Sudan Kusini!
Kwa watu wa Sudan, nataka kuwaachieni wito huu kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Sheikh Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah katika jibu lake la tarehe, 23 Dhul Qi’dah 1446 H sawia na 21 Mei 2025 M:
“Enyi watu wetu wa Sudan, tunakuombeni mrekebishe hali kabla ya majuto, kwani hakuna wakati wa kujuta, chukueni udhibiti wa pande mbili zinazopigana na muziunge mkono kwa uthabiti katika njia iliyo sawa. Inusuruni Hizb ut Tahrir katika kusimamisha Khilafah Rashida, kwani ndani yake kuna izza ya Uislamu na Waislamu na udhalilifu wa ukafiri na makafiri na radhi za Mwenyezi Mungu ni kubwa zaidi.
[إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَنْ كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ]
“Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.” [Qaf: 37]” MWISHO NUKUU.
Kwa uchambuzi wa kina zaidi kuhusu hali ya Sudan tangu zamani hadi sasa, ninakusihi uchukue muda wako kusoma makala hizi, na pia utafute katika tovuti hii kwa makala nyingi zilizoandikwa na Amiri wa Hizb ut Tahrir pamoja na Msemaji wa Hizb ut Tahrir Sudan.
Maregeleo:
https://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/q-and-a/93.html
https://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/q-and-a/970.html
https://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/press-releases/sudan/25587.html
https://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/press-releases/sudan/11056.html
https://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/qestions/political-questions/27753.html
https://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/press-releases/sudan/27267.html
#أزمة_السودان
#SudanCrisis
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Sarah Mohammed – Amerika