Afisi ya Habari
Uholanzi
H. 1 Rabi' I 1447 | Na: 01 / 1447 |
M. Jumapili, 24 Agosti 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
“Israel” kama Mradi wa Kikoloni – na Uholanzi kama Nguzo Yake
(Imetafsiriwa)
Kuondolewa kwa Mkataba wa Kijamii wa Nieuw (BMT) kutoka kwa serikali kuliwasilishwa haraka kwenye vyombo vya habari kama hatua ya kikanuni. Kana kwamba upande huo hatimaye ulivunja sera kwa sababu ya mateso ya kutisha ya Wapalestina mjini Gaza. Lakini hiyo ni dhana potofu. Kuondoka kwao sio dhihirisho la chukizo la kimaadili, bali ni hesabu za kisiasa. Haitoi BMT nje ya mradi wa kikoloni unaoitwa “Israel”, lakini inaonyesha jinsi wao pia wamenaswa kwa kina ndani yake.
“Israel” tangu kuanzishwa kwake, imekuwa mradi wa kikoloni, uliopandwa katikati ya moyo wa ulimwengu wa Kiislamu. Iliasisiwa na inadumishwa ili kuigawanya kanda hiyo, kuidhoofisha, na kutumika kama kituo cha maslahi ya Magharibi. Uholanzi imekuwa sehemu ya hili kwa miongo kadhaa. Iwe VVD, BBB, au NSC: zote zinatambua na kuunga mkono “Israel” kama dola, na hivyo mradi wa kikoloni ambao umewakandamiza watu wa Palestina kwa zaidi ya karne moja.
Tofauti kati ya baraza la mawaziri la sasa na NSC ni vipodozi tu. Muungano huo unaunga mkono waziwazi sera za Netanyahu za mauaji ya halaiki, huku NSC ilizikubali kimya kimya tangu kuanzishwa kwake. Tatizo lao kamwe halikuwa kwa uvamizi, mauaji ya kijamii, au uhalisia wenyewe wa kikoloni, bali kwa njia isiyokubalika ambayo Netanyahu alitekeleza sera zake. Kuondoka kwao kwa hiyo hakuchochewi na mshikamano na Gaza, lakini kwa hesabu tatu: shinikizo la kimataifa sasa ambapo Umoja wa Mataifa unazungumza waziwazi juu ya mauaji ya halaiki, shinikizo la ndani baada ya maandamano makubwa jijini The Hague, na hofu ya uchaguzi ya kuishia upande usiofaa wa historia.
Kwa watu wa Palestina, hakuna kinachobadilika. Mateso yamekuwa yakiendelea kwa karibu miaka miwili. Makumi ya maelfu ya watu wameuawa, watoto wanakufa njaa, na miji yote imegeuzwa kuwa vifusi. NSC ilisimama, ikatazama na kukaa kimya. Wakati walipogeuka sio wakati dhulma ilipoanza, lakini wakati ilipokuwa vigumu kuendelea kisiasa.
Yote haya yanaonyesha kwamba Uholanzi sio tu mshirika wa kubahatisha wa “Israel,” bali ni nguzo changamfu ya mradi mpana wa kikoloni wa Magharibi. “Israel” sio dola ya kawaida iliyopotea njia; ni mradi ambao tangu mwanzo ulijumuisha mantiki ya kikoloni. Na maadamu vyama vya Uholanzi vinatambua na kuunga mkono mradi huo, vinashiriki katika kuendelea kwake.
Hivyo basi ukombozi wa Gaza kamwe hautakuja kutoka kwa kile kinachoitwa huruma ya viongozi wa Magharibi. Sio kutoka The Hague, sio kutoka Brussels, sio kutoka Washington. Serikali hizi si waamuzi wasioegemea upande wowote, bali ni wasanifu na walinzi wa muundo wa kikoloni ambalo “Israel” inawakilisha katika ulimwengu wa Kiislamu.
Ukombozi wa kweli utakuja pale Waislamu wenyewe watakapoukataa mradi huu na kuungana. Umma unaporegesha umoja wake na kuasisi mamlaka yake ya kisiasa ambayo hayaiisujudii Magharibi, bali yanatenda kwa mujibu wa Uislamu. Hapo pekee ndipo Palestina itakombolewa – na kwa hayo, wanadamu wengine wote wataachiliwa huru kutokana na nira ya ubepari na udhibiti wa kikoloni.
Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Uholanzi
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uholanzi |
Address & Website Tel: 0031 (0) 611860521 www.hizb-ut-tahrir.nl |
Fax: 0031 (0) 611860521 E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl |