Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 14 Rabi' II 1447 | Na: HTS 1447 / 41 |
M. Jumatatu, 06 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Yatoa Hotuba ya Hadhara eneo la Nile Mashariki, Khartoum
(Imetafsiriwa)
Kama sehemu ya kampeni yake ya kutibua mpango wa kuigawanya Sudan kwa kutenganisha Darfur, Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya hadhara mnamo Jumamosi, tarehe 4 Oktoba 2025, katika Soko la 6 la Al-Wahda katika mtaa wa Nile Mashariki, Khartoum. Ustadh Omar Hassan, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alizungumzia kuhusu umoja wa Ummah kama suala nyeti. Alianza hotuba yake kwa maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):
[وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللهِ جَمِيعاً وَلَا تَفَرَّقُوا]
“Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane.” [Aal-i-Imran:103].
Akaeleza maana ya aya hiyo, kisha akasema kwamba Umma wa Kiislamu ulishikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu (swt) mpaka akaja mkoloni kafiri, akaivunja Khilafah, akazichana ardhi za Waislamu katika vidola vidogo, anaendelea kupanga njama dhidi ya Ummah na kugawanya kile kilichogawanyika na kutenganisha Sudan Kusini na kutayarisha dola zilizobaki kwa ajili ya kujitenga. Sasa, Amerika inatafuta kutenganisha eneo la Darfur. Alieleza kuwa Muungano wa Uasisi wa Sudan ni hatua moja tu katika njia ya kuisambaratisha nchi kwa kutenganisha Darfur.
Kisha akatoa wito kwa Ummah kubeba jukumu lake, kutimiza wajibu wake, na kujitahidi kwa dhati kuzuia kujitenga kwa Darfur, kama ilivyokuwa kwa Sudan Kusini. Hadhira iliitikia kwa shauku hotuba hiyo.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |