Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  13 Rabi' II 1447 Na: HTS 1447 / 40
M.  Jumapili, 05 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Yaandaa Hotuba ya Kisiasa jijini Khartoum

(Imetafsiriwa)

Kama sehemu ya kampeni yake ya kukwamisha mpango wa kuichana Sudan kwa kutenganisha Darfur, Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa jijini Khartoum, katika eneo la Souq al-Dukhainat al-Awamirah, Jumamosi asubuhi, tarehe 4 Oktoba 2025.

Sheikh Abdul Fattah Ahmed, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alizungumza ndani yake, akianza na aya na Hadith zinazosisitiza umoja wa Umma wa Kiislamu na umoja wa Dola ya Kiislamu. Uislamu umesisitiza kuuwawa kwa anayetaka kuvunja umoja wa Ummah, kugawanya kundi lake, na kuusambaratisha umoja wake. Alisema kuwa adui kafiri anapokula njama dhidi ya umoja wa Umma na dola yake na kutaka kuuchana, hapo Waislamu lazima walifanye suala hili kuwa suala nyeti na kulichukulia hatua ya uhai au kifo.

Na sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan, kwa kuzingatia jukumu letu kwa Ummah, tunakufafanulieni mpango hatari ambao Marekani sasa inautekeleza ili kuitenganisha Darfur kutoka Sudan, kama ilivyotenganisha Kusini hapo awali.

Sheikh Ahmed alieleza uharamu wa mpango huu na kuwataka watu wa nchi hii kusimama kidete kuukabili, kwani wana uwezo wa kufanya hivyo, ili Darfur isiende jinsi Kusini ilivyokwenda. Aliwataka watu wenye ikhlasi wenye nguvu na ulinzi wauhifadhi umoja wa nchi, na kwamba Mwenyezi Mungu atawahoji kuhusu hilo. Aliwataka watu wa nchi kushikana mikono yao na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida ambayo itaukata mkono wa Marekani na Makafiri wa Magharibi kutokana na kuchezea mambo ya Ummah.

Umati ulikatiza hotuba ya Sheikh kwa shangwe za “Allahu Akbar” na “La ilaha illa Allah”, na kukariri kwamba Khilafah ndio suluhisho. Mmoja wa waliohudhuria alisema kuwa kazi hii ndiyo inayotakiwa, na lazima watu waizunguke.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.