Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  20 Rabi' I 1447 Na: HTS 1447 / 30
M.  Ijumaa, 12 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hotuba ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan - mbele ya Msikiti Mkuu jijini Port Sudan
Wito kwa Watu wa Sudan... Msiiruhusu Amerika Kuichana Nchi Yenu na Kuivua Darfur
(Imetafsiriwa)

Mwenyezi Mungu (swt) asema: [وَإِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ] “Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.” [Surat Al-Anbiyā’: 92]. Na Mtume (saw) asema, kama ilivyosimuliwa na as Muslim:

«فَمَنْ أَرَادَ أَنْ يُفَرِّقَ أَمْرَ هَذِهِ الْأُمَّةِ وَهِيَ جَمِيعٌ، فَاضْرِبُوهُ بِالسَّيْفِ كَائِناً مَنْ كَانَ»

“Hakika kutakuwa na mtelezo, na mwenye kutaka kugawanya mambo ya Ummah huu hali ya kuwa umeshikamana, muuweni kwa upanga, yeyote awaye.”

Enyi Waislamu: Mataifa katika maisha yao yana masuala nyeti, yaani, masuala ambayo mtu anakuwa na msimamo mmoja: yhai chini yao au kifo kwao. Itikadi ya Uislamu imetubainishia sisi Waislamu masuala yetu nyeti; yaani yale ambayo kipimo chake ni uhai au kifo. Miongoni mwa masuala hayo nyeti ni suala la umoja wa dola na umoja wa Ummah. Tulipoondoa suala hili kwenye kituo chake stahiki hapo awali, Amerika, kwa msaada wa baadhi ya watu wetu, iliweza kuichana nchi yetu na kuitenganisha Sudan Kusini, na sasa inaregea kukamilisha kile ilichoanza mwanzo kuchora, kwa mipaka ya damu, dola mpya katika mabaki ya nchi yetu; kwa kuivua Darfur, ambako matukio yanazidi kupamba moto katika kutumikia njama ya Amerika kwa usaidizi wa zana zake ndani na nje.

Amerika, iliyoitenga Sudan Kusini kwa visingizio vya madai ya amani, kupitia mikono ya watawala na waasi, na kwa baraka za wanasiasa na baadhi ya wanahabari na kimya cha wanazuoni, inataka leo kwa hali hiyo hiyo kuivua Darfur kutoka Sudan; kwa kuandaa jukwaa huko Darfur ambalo linadhibitiwa na Vikosi vya Msaada wa Haraka isipokuwa mji wa Al-Fashir, ambao vinajitahidi kuiangusha na imetangaza dola kwa kutangaza serikali sambamba huko Nyala, mji mkuu wa Darfur Kusini. Je, mutairuhusu kufanya hivyo katika nchi yenu?! Wallahi Atakuulizeni baada ya kukutakeni mufe bila ya kumzuia kafiri mkoloni kufikia lengo lake.

Enyi Watu wa Sudan: Simameni ili kutibua mpango huo, ng'oeni kundi la vibaraka na wanafiki, na rekebisheni mwenendo wa maisha yenu, kwani muumini hang’atwi mara mbili kutoka kwenye shimo moja. Tumeng’atwa kutoka kwenye shimo la Amerika kwa kuitenga kwake Sudan Kusini – je, tutairuhusu kuitenganisha Darfur?! Kutoka kwa Abu Huraira, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kwamba Mtume (saw) amesema:

«لَا يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ» “Muumini hatakiwi kung’atwa mara mbili (na kitu) kutoka kwenye shimo moja.”

Basi simameni, enyi Waislamu, kumtii Mwenyezi Mungu kwa kulifanya suala la umoja wa dola kuwa suala nyeti, ambalo kipimo chake ni uhai au kifo. Kutoka kwa ‘Urfaijah imepokewa kwamba alisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) akisema:

«مَنْ أَتَاكُمْ وَأَمْرُكُمْ جَمِيعٌ عَلَى رَجُلٍ وَاحِدٍ، يُرِيدُ أَنْ يَشُقَّ عَصَاكُمْ، أَوْ يُفَرِّقَ جَمَاعَتَكُمْ، فَاقْتُلُوهُ»

“Atakayekujieni na hali jambo lenu liko mikononi mwa mtu mmoja, na akakusudia kuvunja fimbo yenu au kugawanya mkusanyiko (jama’ah) wenu, basi mumuue.”

Je, tumtii kipenzi chetu Muhammad (saw), au tumtii Marekani mkoloni kafiri?! Hakika sisi tunamtii Mtume (saw) kwa kuitikia amri ya Mola wetu Mlezi Ametakasika aliyesema:

[وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَاحْذَرُوا فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا عَلَى رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ]

“Na mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume, na tahadharini. Na ikiwa mtageuka basi jueni ya kuwa juu ya Mtume wetu ni kufikisha ujumbe tu ulio wazi.” [Surat Al-Mā’idah: 92].

Na Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانْتَهُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ]

“Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Surat Al-Hashr: 7].

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.