Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 15 Rabi' I 1447 | Na: H 1447 / 008 |
M. Jumapili, 07 Septemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wahanga wa Vita Wanaoteseka Zaidi ni Watoto wa Gaza wenye Ulemavu
(Imetafsiriwa)
Vita vya maafa dhidi ya Gaza, vilivyoanza mnamo Oktoba 7, 2023, vimeathiri kila nyanja ya maisha huko: watu, miti, mawe, na rasilimali, hasa wanawake na watoto. Vifo na uharibifu vimeenea kila mahali. Kulingana na Wizara ya Afya mjini Gaza, vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 63,000, kujeruhiwa kwa wengine 160,000, na mamia ya maelfu ya watu kuyahama makaazi yao, huku kukiwa na janga kubwa la kibinadamu linalojumuisha uhaba wa chakula, dawa, na maji safi ya kunywa.
Ripoti ya hivi punde ya kamati ya Umoja wa Mataifa iliripoti kuwa watu 157,114 walijeruhiwa kati ya Oktoba 7, 2023, na Agosti 21 mwaka huu, 25% kati yao wako katika hatari ya ulemavu wa maisha. Ilitangaza kuwa takriban watoto 40,500 wamepata majeraha yanayohusiana na vita katika muda wa miaka miwili tangu kuzuka kwa vita hivyo, na kwamba zaidi ya nusu yao wanakabiliwa na ulemavu. Takriban watoto 21,000 mjini Gaza wamepata ulemavu!!
Kamati hiyo ilisema kuwa watu wenye ulemavu wa kusikia au kuona mara nyingi hawakujua maagizo ya kuhamishwa kutoka kwa vikosi vilivyovamia, na hivyo kuwafanya wasiweze kukimbia. Baadhi waliuawa shahidi bila hata kujua kuhusu amri za kuhamishwa.
Baadhi yao walilazimika kutoroka katika mazingira yasiyo salama na yasiyofaa, kama vile kutambaa kwenye mchanga au matope bila msaada. Pia wanakabiliwa na upunguzwaji mkubwa wa misaada ya kibinadamu, na kuwaacha wengi bila chakula, maji safi, au vyoo, na kutegemea wengine kwa ajili ya kuishi, hasa kwa vile hawawezi kuvipata.
Watoto walikuwa na hisa kubwa ya ulemavu huu, na kuwa walengwa wa uvamizi katika vita vyake vya maangamizi vinavyoendelea. Kila shambulizi la anga linaweza kumaanisha kukatwa mguu wa mtoto, kupooza kwa maisha yake yote, au umbo ambalo hubadilika sura zake na kuacha kovu la kudumu, na kuwaacha wakikabili tazamio la kupoteza maisha yao yote ya baadaye mara moja. Katika kambi na makaazi ya watu waliohamishwa, wanakosa huduma ya matibabu, vifaa vya usaidizi, au hata chakula cha kutosha. Huku hospitali nyingi zikiharibiwa na dawa na vifaa vya matibabu vikiwa haba, watoto wenye ulemavu ndio walio katika hatari kubwa ya kupuuzwa. Wengi wao wanahitaji vikao vya mara kwa mara vya matibabu ya viungo, dawa za kudumu, na viungo vya bandia. Walakini, kukatwa kikamilifu kwa huduma za matibabu kumegeuza mahitaji haya kuwa ndoto isiyoweza kufikiwa. Kisaikolojia, watoto wanakabiliwa na hofu ya mashambulizi ya anga, njaa, na ukosefu wa matumaini, na kufanya maisha yao ya kila siku kuwa msururu wa mateso yasokwisha.
Yote haya na mengine mengi yanatokea mbele ya macho na masikio ya dunia nzima, pamoja na taasisi na vyama vyake vinavyodai kuwa vya kibinadamu na vinavyosimamia haki za binadamu. Wanachofanya hakiendi zaidi ya maandamano rasmi hapa, au kuwasilisha ripoti huko, au kujaribu kuleta misaada isiyokidhi njaa! Na watawala wa Kiislamu wanajishughulisha na kuhifadhi viti vyao (vya utawala) juu ya maiti na damu za Waislamu na mateso yao, haswa mjini Gaza, kwa kughafilika na kupuuza yale aliyoyasema (saw): «مَا مِنْ امْرِئٍ يَخْذُلُ امْرَأً مُسْلِمًا فِي مَوْضِعٍ تُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ وَيُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ إِلَّا خَذَلَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ وَمَا مِنْ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِمًا فِي مَوْضِعٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ إِلَّا نَصَرَهُ اللَّهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ نُصْرَتَهُ» “Hakuna (Muislamu) atakayemwacha Muislamu mwengine katika mahali ambapo utukufu wake unakiukwa na heshima yake inavunjwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamwacha katika mahali ambapo angependa nusra yake. Na hakuna Muislamu ambaye atamnusuru Muislamu mwengine mahali ambapo heshima yake inavunjwa na utukufu wake unakiukwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamnusuru mahali ambapo angependa nusra yake.” Siku ya malipo kutoka kwao iko karibu, Mwenyezi Mungu akipenda.
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |