Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  27 Safar 1447 Na: 1447 / 03
M.  Alhamisi, 21 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Migogoro Inayosababishwa na Utawala Fisadi Haiwezi Kutatuliwa Kupitia Nao
(Imetafsiriwa)

Tangu Marekani ilipoikalia kwa mabavu Iraq mwaka 2003, na kwa miaka 22 sasa, imekuwa ikikumbwa na mzozo wa kifedha na umaskini na uchochole ulioenea. Licha ya mapato ya mafuta yanayofikia mamia ya mabilioni kila mwaka, wanasiasa na wataalamu wake hujitokeza kila mwaka kutoa tahadhari kuhusu mgogoro wa kifedha unaoweza kusababisha serikali kukosa uwezo wa kulipa mishahara ya wafanyikazi.

Mnamo Jumanne, Agosti 19, 2025, mtaalamu wa uchumi wa Iraq, Nabil Al-Marsoumi alisema katika chapisho kwenye ukurasa wake wa Facebook, “Akaunti rasmi za kifedha zilizotolewa na Wizara ya Fedha kwa nusu ya kwanza ya 2025 zinaonyesha kuwa jumla ya mishahara na fidia ilifikia takriban dinari trilioni 44.9, huku mafuta ghafi yalifikia dinari trilioni 45.2, ikimaanisha kuwa asilimia ya mapato ya mafuta inayolipia mishahara ilifikia dinari 99.2%.

Tarakimu hizi za kuogofya na mlingano huu wa kusikitisha unaonyesha waziwazi ufisadi wa mfumo wa uchumi wa serikali. Ni muhimu kutaja kwamba kiasi kikubwa cha fedha, alichodai kilitengewa mishahara na fidia, kwa hakika kinaingia kwa kiasi kikubwa kwenye mifuko ya wafisadi katika tawala tatu za urais na matawi yao, kupitia mishahara mikubwa, "wanaanga," "Rafha," na mipango ya kilaghai. Kwa hiyo, tunawaona wakipigania vyeo na kupanga njama wao kwa wao kwa kutumia njia ovu kabisa. Haya ndiyo tunayoshuhudia katika kila awamu ya uchaguzi.

Enyi Waislamu, Enyi Watu wa Iraq: Tatizo la Iraq na nchi nyengine za Kiislamu ni tatizo la mfumo, na tatizo la wasaliti wafisadi ambao makafiri wamewaweka juu ya shingo zenu baada ya kuivunja dola yenu na kuhujumu mamlaka yenu. Haliwezi kutibiwa na mbinu za viraka zilizojaribiwa na wale wanaojiita wataalamu wa kiuchumi. Ahmed Al-Tamimi, mtaalamu wa masuala ya uchumi, anadai kwamba “utabiri wa awali wa bajeti ijayo unaonyesha nakisi ya kifedha inayoendelea kutokana na sababu kadhaa zilizounganishwa, hasa kushuka kwa bei ya mafuta duniani, ambayo inawakilisha zaidi ya 90% ya mapato yote, pamoja na ongezeko la endelevu la matumizi ya uendeshaji serikali, hasa katika mishahara, pamoja na udhaifu wa wazi wa vyanzo mbalimbali.” Anafafanua kuwa “kukabiliana na nakisi hii kunahitaji ufumbuzi wa kivitendo, kuanzia kwa kurekebisha mfumo wa kodi na kupanua wigo wa kodi, kufanya kazi ya kukusanya kodi kutoka sekta zisizo rasmi, na kuimarisha mapato ya serikali kwa kuboresha ufanisi wa usimamizi wa uvukaji mipakani ili kukabiliana na magendo na rushwa, na kuongeza ukusanyaji wa huduma za serikali kama vile umeme, maji na manispaa kwa njia ya haki na iliyopangiliwa.”

Haya ni masuluhisho ikiwa fikra ni ya aina moja na utawala. Tiba ya kweli na yenye ufanisi ni kung'oa utawala huu mbovu na viongozi wake wafisadi na kusimamisha mfumo wa adilifu, wa kiwahyi. Mfumo wa Kiislamu, ambao Mola wa walimwengu ameuchagua kwa ajili ya wanadamu, unatabikishwa na watu waadilifu wanaomcha Mwenyezi Mungu Mtukufu na wanaozingatia maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، فَالْأَمِيرُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ...»

“Kila mmoja wenu ni mchungaji na kila mtu anajibika kwa kundi lake. Imam (khalifa) ni mchungaji wa watu na ataulizwa kuhusu raia wake (namna gani aliendesha mambo yao).”

Kwa izza hii na maisha haya ya heshima, Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake, inakulinganieni. Basi itikieni amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na fanyeni bidii kutimiza ahadi yake:

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” Na bishara njema ya Mtume wake (saw) kwamba itasimama baada ya kuondolewa utawala dhalimu:

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ. ثُمَّ سَكَتَ»

“Basi utakuwepo ni ufalme wa kidhalimu, na utakuwepo kwa muda anaoutaka Mwenyezi Mungu, kisha atauondoa atakapotaka kuuondoa, kisha itakuwa Khilafah kwa njia  ya utume, kisha akanyamaza.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.