Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  16 Muharram 1447 Na: 1447 / 01
M.  Ijumaa, 11 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mfuko wa Fedha wa Kimataifa: Chombo Mikononi mwa Makafari cha Kudhibiti Sera ya Ndani ya Nchi Inayokopa
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumatano, 9/7/2025, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ulionya kwamba uchumi wa Iraq unakabiliwa na changamoto kubwa. Bodi ya IMF, katika taarifa yake ya kuhitimisha mashauriano ya Kifungu cha IV na Iraq, ilisema kuna nafasi ya kuimarisha mapato yasiyo ya mafuta kupitia ongezeko la kodi na ushuru wa forodha.

Ilieleza kuwa, kwa upande wa mapato, pamoja na kuimarisha usimamizi wa kodi, kuna nafasi ya kuongeza ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa, kurekebisha ushuru wa mapato ya kibinafsi, ikiwemo kupunguza misamaha, na kutoza ushuru wa mauzo jumla katika muhula wa katikati.

Kuhusu matumizi, mageuzi ya kina ya mswada wa mishahara ya umma, kwa kupunguza ajira na kupitisha sheria ya kupunguza idadi ya wafanyikazi, yanapaswa kutekelezwa. Hatimaye, ni muhimu kurekebisha mfumo wa pensheni ya umma kwa kuongeza umri wa kustaafu na kupunguza viwango vya haki stahiki na ubadilishaji asilimia.

Haya ni maagizo ya IMF kwa serikali ya Iraq - uingiliaji wa wazi katika sera ya ndani ya nchi.

Enyi Waislamu na watu wa Iraq: Haifichiki tena kwa mtu yeyote jinsi mkanganyiko wa kiuchumi ulivyo ndani ya nchi yenu, na jinsi umasikini unavyoongezeka licha ya utajiri mkubwa iliyo nao. Sababu ni kushikamana kwa serikali yenu na Amerika na dola zengine zenye ulafi kupitia ala zao, na Amerika ikiwa na mkono wa juu katika ala hizi zinazowakilishwa na dolari na Benki ya Dunia na IMF. Amerika imetabanni msaada wa kifedha kama moja ya ala zake za kisiasa, kwa nje ili kusaidia nchi zenye uhitaji, lakini kiuhalisia ni ili kushawishi maamuzi ya kisiasa ya nchi. Ni jambo la aibu na pia la kusikitisha kwamba nchi kama Iraq, yenye utajiri mkubwa na rasilimali nyingi, inakimbilia kukopa - na kutoka kwa nani?! Kutoka kwa chombo kinachotaka kutawala maamuzi ya kisiasa ya nchi, haswa sera yake ya ndani!

Kilichotajwa hapo juu na Bodi ya IMF, kama vile kuongeza kodi na ushuru kwa watu, sio ushauri bali ni wizi wa juhudi za watu baada ya kuwa tayari wameshaiba utajiri wa nchi – ili Amerika na nchi za Ulaya ziishi kwa anasa kwa gharama ya mataifa ya Kiislamu, ambayo sasa yanaishi katika umaskini na mahitaji baada ya kuporwa – na hivyo shirika hili linapata pesa zake kwa riba maradufu. Pia ni kuingilia sera za ndani kiasi cha kudhibiti ajira na kustaafu!

Je, kuna rai au mamlaka iliyobaki kwa watawala hawa wa Ruwaibidha (watepetevu na duni)?! Sera yao ya kigeni imefungamana na mabwana zao makafiri, mfumo wao wa kisiasa na kiuchumi umelazimishwa juu yao, na hata sera zao za ndani haziachiwi wao. Umma wa Kiislamu unaishi katika udhalilifu na fedheha kiasi gani leo?!

Enyi Waislamu: Jueni kwa yakini kwamba mikono hii haiwezi kukatwa, mali zenu hazitarudi kwenu, na ushawishi wa makafiri hautatolewa katika ardhi zenu isipokuwa kwa dola ya Khilafah Rashida, ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na bishara njema ya Mtume wake Mtukufu (saw). Basi jitokezeni kufanya kazi nzito pamoja na Hizb ut Tahrir ya kusimamisha faradhi hii kubwa, ambayo ndani yake mna heshima yenu, udhalilifu kwa makafiri, na juu ya yote, radhi za Mola Mlezi wa walimwengu wote.

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُوْلَـٰٓئِكَ هُمُ الْفَـٰسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 55]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.