Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
H. 12 Rabi' II 1447 | Na: H 1447 / 13 |
M. Jumamosi, 04 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Suluhisho la Dola Mbili ni Kejeli ya Karne isiyo na Aibu
[اللَّهُ يَسْتَهْزِئُ بِهِمْ وَيَمُدُّهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ]
“Mwenyezi Mungu atawadhihaki wao na atawawacha katika upotofu wao wakitangatanga ovyo.” [Surah Al-Baqara: 15]
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh inashutumu vikali kile Prof. Yunus alisema kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, “Ni kwa msingi wa mipaka ya kabla ya 1967 tu, na Israel na Palestina wakiishi bega kwa bega kwa amani, haki inaweza kutendeka”. Wakati watu wa Palestina wanaangamizwa mbele ya macho yetu na Mayahudi kunyakua 78% ya Palestina kinyume cha sheria, ni vipi haki inaweza kutendeka kwa kuruhusu ‘Israel’ kuishi bega kwa bega na Palestina! Kwa nini tunaita makundi machache ndani ya umbile haramu la Kiyahudi kuwa ni dola (Palestina), lakini haina hata jeshi lake?
Kejeli hii inatukumbusha istihzai ya tangazo la Yasser Arafat la kuanzishwa kwa Dola ya Palestina mnamo tarehe 15 Novemba 1988 nchini Algeria. Ilikuwa dola kwenye karatasi, lakini matunda ghafi ya mazungumzo ya Oslo yalikuwa mamlaka ndogo chini ya visu vya Mayahudi. Licha ya hayo yote, utambuzi huu ulikaribishwa na watawala ruwaibidha (wajinga wasio na maana) wa Waislamu, pamoja na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Ligi ya Nchi za Kiarabu. Jambo la kushangaza ni kwamba, ilikaribishwa pia na mashirika ya Kipalestina, ambayo yanaona kuwa ni matunda ya uthabiti wao, kana kwamba Palestina imekombolewa na umbile la Kiyahudi kung'olewa! [قَاتَلَهُمُ اللَّهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ] “Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa?!” [At-Tawbah: 30].
Suluhisho lililobuniwa na Marekani la Dola Mbili linalenga kuhalalisha uhusiano kati ya umbile haramu la Kiyahudi na nchi za Kiislamu. Bila ya kuungwa mkono na watawala wasaliti wa nchi za Kiislamu, umbile hili halingedumu hata siku moja, pamoja na mabilioni ya dolari za misaada ya kijeshi inayopokea kutoka kwa ulimwengu wa Magharibi:
[لَنْ يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ]
“Maadui hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa.” [Aal-i Imran: 111]. Marekani, hasa, ilianza kutia ushawishi juu ya Suluhisho la Dola Mbili katika miaka ya 1990 na kulitumia kuendeleza malengo yake ya kijiografia na kisiasa kwa kuimarisha wakala wake – ‘Israel’. Marekani inahakikisha kwamba Ummah wa Kiislamu unabaki umegawanyika kwa kuiweka ‘Israel’ kuwa na nguvu za kijeshi na daima kutofautiana na majirani zake. Wakati huo huo, Marekani inaweka usawa kuzuia nguvu za ‘Israel’ kuzua mzozo ambao unaweza kuvuruga mfumo mzima. Mfumo huu wa ukaguzi na usawa ni pazia la utawala wa Marekani katika Mashariki ya Kati. Marekani si mpatanishi wa haki anayeweza kusawazisha; bali, ni meneja wa mfumo wa ikolojia ambamo kwao ‘Israel’ inatawala Waarabu, Marekani inadhibiti ‘Israel’ kwa kiasi fulani, na wakati mwengine, kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kupitia Iran, na kila mtu bado anaitegemea Washington.
Enyi Waislamu, Uingereza, Canada, Australia na Ureno zililitambua hiyo inayoitwa “Dola ya Palestina,” na kufuatiwa na nchi kadhaa katika mkutano wa ngazi ya juu wa kimataifa wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika kuanzia tarehe 22-30 Septemba 2025, na kusimamiwa na Ufaransa na Saudi Arabia. Ni wazi kwamba mkuu wa zamani wa ukafiri, Uingereza, na nchi nyingine za ukafiri ziliitambua ile inayoitwa Dola ya Palestina ili kuficha sura yao mbaya, ya ghilba kutoka kwa wanadamu wote kwa jumla na kwa watu wao hasa. Ripoti kadhaa za habari zinazoonyesha uungwaji mkono wa kijeshi kwa ‘Israeli’ zinathibitisha hili, kwa mfano, kulingana na shirika la habari la Anadolu, vyombo vya habari vya nchi hiyo viliripoti kwamba “Uingereza ilituma risasi zaidi ya laki moja kwa Israel ndani ya mwezi mmoja (Agosti iliyopita) katikati ya mauaji ya Gaza. Shehena nyingine mwezi Agosti zilijumuisha vifaru, bastola na bunduki, pamoja na aina mbalimbali za vilipuzi” (Manabzamin, 1 Oktoba 2025). Kupitia Azimio la udanganyifu la Balfour la mwaka 1917, Uingereza ya kibeberu yenye ujanja ilikabidhi sehemu za Khilafah Uthmani (Palestina) kwa Wazayuni. Kufuatia Vita vya pili vya Dunia, Marekani ilichukua udhibiti wa ME na ikawa nguvu kuu wakati Uingereza ilipofilisika. Tangu wakati huo, ulimwengu wa Magharibi unaoongozwa na Marekani umekuwa ukifanyia kazi mtego huu wa udanganyifu, ambao huilipa ‘Israel’ haki za kudumu za uporaji. Kama sehemu ya juhudi hizi, sasa wanapanga kuunda chombo cha kimataifa kinachoitwa “Mamlaka ya Mpito ya Kimataifa ya Gaza (GITA)”, ambacho kitakuwa na mamlaka ya kuwa “mamlaka kuu ya kisiasa na kisheria” ya Gaza kwa muda wa miaka mitano, na kitakachoongozwa na Tony Blair, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza ambaye alicheza dori ya kusaidia katika uvamizi wa 2003 wa Marekani nchini Iraq (“Ikulu ya White House inaunga mkono mpango ambao utamfanya Tony Blair kuongoza idara ya muda mfupi ya Ukanda wa Gaza”, The Guardian, 25 Septemba, 2025).
Enyi Waislamu, mauaji ya halaiki mjini Gaza sio tu janga la mbali, bali ni mstari wa mbele wa mapambano ya Umma wetu katika ardhi hiyo iliyobarikiwa. Ndugu na dada zetu nchini Palestina hawapiganii mamlaka ya muda mfupi au utajiri wa ulimwengu; wamesimama kama walinzi, wakiyatoa maisha yao wenyewe kwa ajili ya kila shubiri ya ardhi ambayo ni mali ya Waislamu, wakilinda utakatifu wa Ummah wetu dhidi ya mashambulizi ya makafiri wapiganaji. Nukta kuu ni kwamba Waislamu lazima wakumbuke kwamba suluhisho la Dola Mbili ina maana ya kutambua kudai kwa Mayahudi ardhi takatifu. Hii ni haramu katika Shariah. Maswahaba watukufu na mujahidina wema walimwaga damu zao hapo. Pia ni eneo la msikiti mtakatifu wa tatu, eneo la Hija kwa Waislamu duniani kote. Hapo ndipo ilipotokea Safari ya Usiku ya Mtume (saw). Kama ardhi ya Kiislamu, Palestina ni mahali ambapo Waislamu hawawezi kuacha hata shubiri yake moja.
Msiba mkubwa zaidi wa Ummah ni watawala wake, ambao huwafunga wana wetu mashujaa wa jeshi kwenye kambi. Badala ya kuwatuma kupigana chini ya bendera ya Uislamu ili kuwaokoa Waislamu na mauaji ya halaiki, kulinda Kibla cha kwanza, na kuikomboa ardhi yetu takatifu, wanawatuma kwa aibu kwenye misheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa chini ya uongozi wa makafiri wapiganaji. Tangu Khilafah ilipoondolewa karibu miaka mia moja iliyopita, Waislamu wamekosa Khalifa wa kujikusanya nyuma yake na kupigana. Kama Mtume (saw) alivyosema,
«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ عَنْهُ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam ni ngao watu hupigana vita nyuma yake na hujihami kwaye” (Imepokewa na Al-Bukhari na Muslim). Kwa hiyo, Waislamu duniani kote wanawalingania maafisa wa jeshi wenye ikhlasi kushikana mikono na kusimamisha tena Khilafah chini ya uongozi wa Hizb ut Tahrir. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ]
“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini” [At-Tawbah: 14].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |