Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Al-Waqiyah TV: Khilafah Pekee Ndio Itakayoiletea Sudan Izza!

Sudan kwa sasa iko katikati ya vita vya kipumbavu ambavyo vimesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya raia na kuzua mgogoro mkubwa zaidi duniani wa njaa na kuhama makaazi. Wananchi wa Sudan wamekumbwa na mizozo mbalimbali pamoja na umaskini mkubwa, udikteta, migawanyiko ya kikabila na kitabaka na matatizo mengine mengi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa miongo kadhaa chini ya uongozi, tawala na mifumo mtawalia.

Mjadala huu unazungumzia jinsi dola ya Khilafah pekee, inayotawaliwa na mfumo na uongozi wa Kiislamu pekee inavyotoa masuluhisho ya wazi kwa matatizo haya. Utaangazia jinsi dola ya Khilafah inavyojumuisha kanuni, sheria, taasisi na taratibu za kujenga mustakbali thabiti wa kisiasa, adilifu, wa umoja, usalama na ustawi wa Sudan na ulimwengu wote wa Kiislamu.

Ni sehemu ya kampeni ya kimataifa iliyozinduliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir yenye kichwa, “Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti na Udanganyifu” ambayo inalenga kuleta mwanga wa kimataifa juu ya janga la kibinadamu linalozidi kuwatesa Waislamu wa Sudan kutokana na mzozo wa sasa unaoisibu nchi hiyo ambavyo vimepewa jina “Vita Vilivyosauliwa”.

Jumamosi, 28 Rabi-ul Awwal 1447 H - 20 Septemba 2025 M

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.