Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Gaza iko Ukingoni mwa Kuzidishwa Mauaji na Ukandamizaji Mkali ikiwa Umma wa Kiislamu hautasonga mbele Kuinusuru
(Imetafsiriwa)

Gaza Hashim inaingia katika hatua mpya ya mauaji na uharibifu baada ya wizara ya usalama ya umbile halifu kuamua asubuhi ya Ijumaa hii, 08/08/2025, kupanua operesheni zake ili kuweka udhibiti wake juu ya Mji wa Gaza kikamilifu, na uamuzi huu ulikuja kwa siri kutoka kwa Amerika kwa ulimi wa Trump, Rubio, na wengine kutoka kwa wakaazi wa (ikulu ya) Jumba Jeusi.

Uamuzi mpya wa uvamizi huo hauna maana nyengine isipokuwa mauaji zaidi, njaa zaidi, na uhamishaji zaidi, hadi utakapoondoa uwezekano wowote wa uhai mjini Gaza, ikiwa kutabakia uwezekano wowote ndani yake, na kuwaacha watu wa Gaza na chaguzi mbili pekee hakuna ya tatu: kifo au kuhama, na wako karibu na chaguo la kifo.

Na kwa upande mwengine wa Palestina iliyotekwa nyara, umbile halifu linaamua kwa maneno na vitendo kulazimisha ubwana wake juu ya Ukingo wa Magharibi, kwa hivyo linaua, kukamata, kubomoa nyumba, kunyang'anya ardhi, kupanua makaazi yake kwa upanuzi mbaya, na kubadilisha miji na vijiji – kwa kuweka milango ya kuingilia – kwenye maeneo yaliyotengwa na Amerika na kuwa mithili ya hifadhi za wenyeji wa Amerika nchini Amerika na ghetto za ukoloni wa Kimagharibi barani Afrika.

Enyi Waislamu:

Haikuwa kwa wale ambao wameghadhibishwa na Mwenyezi Mungu (swt) kufanya uhalifu wao isipokuwa kwa kamba kutoka Amerika, dola za Magharibi, na washirika wao na vibaraka kutoka kwa watawala wa Waislamu. Kauli hizo wanazozitoa kuhusu huruma zao na watu wa Gaza au miito hiyo dhaifu ya kuruhusu kuingia kwa misaada si chochote ila ni majaribio ya kuwapotosha watu na kuwapurukusha, kwani dola hizi ndizo zinazolipa umbile la Kiyahudi silaha, na wao ndio wanaotoa ulinzi kwa uhalifu wake. Vituo vya misaada ambavyo Amerika ilianzisha vimekuwa mitego ya kifo na mauaji, na kufanya tonge ya riziki ya watu kutumbukizwa katika damu na udhalilifu.

Na katika ukaidi huu inaonekana dori ya Mamlaka ya Palestina, ambayo haijaacha kuwabwagia jukumu juu ya mujahidina kwa jinai za Mayahudi huko Gaza, na inataka kuwapokonya silaha kwa matumaini kwamba kwa fedheha na udhalilifu huu, inaweza kupata utambuzi wa dola kwenye karatasi, ambayo Amerika inaikanyaga kwa maneno yake na Mayahudi kuyasambaratisha maamuzi hayo. Na bado rais wa Mamlaka ya Palestina anaendelea kuwa na ndoto ya kutawala kitu cha Gaza, hata kama katika mfumo wa manispaa au mamlaka ya ndani ambayo iko karibu na mamluki wanaofanya kazi ili kutumikia malengo ya umbile la Kiyahudi.

Kadhia ya Palestina na Gaza haina shaka yoyote; sababu yake ni wazi na ufumbuzi wake ni dhahiri. Hata hivyo, Umma wa Kiislamu, chini ya kampeni ya uhadaifu, umeanza kuona kuingia kwa chakula kwa watu wa Gaza kuwa ni mafanikio, na kabla ya hapo, uliona kufikiwa kwa mapatano kama mafanikio, na kuona kusitishwa kwa uvamizi kuwa ni mafanikio pia. Pengine umbile hilo, ulimwengu, na watawala vibaraka wanataka kuufikisha Umma wa Kiislamu kwenye hitimisho kwamba kuhama na kusalimu amri ni chaguo bora zaidi kuliko kuangamizwa kwa watu wa Gaza, au kwamba maangamizi ya nusu yao ni bora kuliko maangamizi yao yote. Wakati wote Ummah unatambua katika ufahamu wake wa kina kwamba sababu ya maradhi hayo ni kuwepo kwa umbile nyakuzi na kuwepo kwa tawala zinazoilinda na kuzuia Ummah mzima usiinusuru Gaza, na unatambua kwamba suluhisho pekee ni kuikomboa Palestina yote, kutoka bahari yake hadi mto wake, na kwamba ni wajibu ni lazima kwa umma wa Kiislamu kupeleka majeshi makubwa ili kuwanusuru kuwanusuru kaka zao, na lazima uvuke na kuwakanyaga wale waliorithi kwake udanganyifu wa kutokuwa na uwezo na udhaifu wa azma, na wameipasua kwa mipaka iliyoifanya kuwa mazungumzo na kuivunja vipande vipande.

Enyi Umma wa Muhammad (saw), Umma bora kabisa uliotolewa kwa ajili ya wanadamu:

Kadhia ya Palestina leo imefikia kiwango ambacho hakijawahi kufika hapo kabla, kwani kunaswaliwa swala na ibada za Kiyahudi ndani ya Msikiti wa Al-Aqsa, watu wa Gaza wanachinjwa na kuwekwa njaa, na watu wa Ukingo wa Magharibi wanazingirwa kwenye mageto na wanakabiliwa na yale yaliyo mabaya zaidi kuliko yaliyotokea Gaza ikiwa Mwenyezi Mungu (swt) hatatufunika kwa Rehema na Ushindi. Kila hatua inayochukuliwa na Umma wa Kiislamu leo bila ya kuangusha viti vya utawala, kufungua mipaka, na kisha kukusanyika katika jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu ili kukomboa Al-Masra (mahali pa Isra), itaongeza mizigo ambayo Ummah unaibeba, juu ya mizigo ya damu, njaa, na mzingiro wa watu wa Gaza. Na isipo kuwa usukume harakati kubwa pamoja na wanazuoni wake, watu wake wa kawaida, wanafikra wake, wasomi wake na majeshi yake, kuelekea kuliunganisha neno lake chini ya bendera moja, bendera ya “La illaha illallah” (Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu) katika kivuli cha Khilafah kwa njia ya Utume na kusimamisha Dini na kutangaza jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt), mauaji na bughudha yataongezeka miongoni mwa watu wa Gaza hasa na katika Palestina kwa jumla, na mutaulizwa kuhusu mulichokuwa mukifanya.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ (38) إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache. (38) Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [Surah At-Tawbah:38–9]

H. 14 Safar 1447
M. : Ijumaa, 08 Agosti 2025

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.