- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa
Amiri wa Hizb ut Tahrir
Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Katika Ukurasa Wake wa Facebook
Jibu la Swali
Kuamiliana na Dola zilizo za Kivita Kivitendo
Kwa: Abu Muhammad Salim
(Imetafsirirwa)
Swali:
As-Salamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh
Abu Muhammad Salim
Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu uwe uko katika afya njema, na Mwenyezi Mungu akupe ushindi mkubwa. Namuomba Mwenyezi Mungu aifungue milango yote ya kheri mikononi mwako.
Swali hili nalielekeza kwa Sheikh wetu na kipenzi chetu, Amiri wa Hizb ut Tahrir, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, likisema:
Ndugu mmoja aliniuliza kuhusu kufanya kazi katika kiwanda cha kutengeneza makontena katika makaazi ya Barkan. Hivi majuzi, sehemu ya kiwanda hiki iligeuzwa kwa manufaa ya jeshi la ‘Israel’, na kinatengeneza matrela ya kusafirisha majenereta ya umeme na vitu vyengine vinavyohusiana na jeshi. Je, inajuzu kufanya kazi katika sehemu hii inayotengeneza matrela kwa ajili ya jeshi?
Mwenyezi Mungu akubariki na akulipe malipo bora zaidi.
Mwenyezi Mungu akuhifadhi, akupe ushindi, akulinde, akupe nguvu, na alete ushindi na tamkini kupitia mikono yako.
Ikiwezekana, jibu la haraka litathaminiwa—Mwenyezi Mungu akulipe kheri.
Jibu:
Wa Alaikum Assalam wa Rahmatullahi wa Barakatuh,
Kuhusu kiwanda kilichotajwa (ambacho hivi majuzi kilikuwa na sehemu iliyogeuzwa kwa manufaa ya jeshi la ‘Israel’ na kutengeneza matrela ya kusafirisha majenereta ya umeme na vitu vyengine vinavyohusiana na jeshi), ni mali ya umbile la Kiyahudi, ambayo ni dola ya kivita kivitendo. Jibu linategemea hali mbili:
1. Waislamu wanaoishi chini ya uvamizi.
2. Waislamu walio nje ya uvamizi.
Hali ya kwanza:
Waislamu walio chini ya uvamizi wa Kiyahudi ni kama Waislamu waliobaki Makka baada ya dola kuasisiwa mjini Madina. Inajuzu kwa watu wa Palestina walio chini ya uvamizi wa Mayahudi kujishughulisha na ununuzi, uuzaji n.k, isipokuwa katika kazi inayomtia nguvu adui. Kadhalika, kwa Muislamu ambaye ana uraia wa Marekani kwa mfano, hukmu yake ni sawa na ya Waislamu wa Makka ambao hawakuhama, hivyo inajuzu kwao kuamiliana na Dar al-Harb (dola ya kivita) wanayoishi ndani yake, isipokuwa katika mambo ambayo yanawatia nguvu makafiri dhidi ya Waislamu, kwa msingi wa kufikia uhakiki wa kisheria (tahqiq al-manat).
Hali ya pili:
Hapo awali tumejibu maswali sawia na haya katika majibu mengi, ikiwemo:
Jibu la Swali mnamo tarehe 31/03/2009:
1. Kufanya kazi moja kwa moja na dola za kivita kivitendo hairuhusiwi, na pia hairuhusiwi kufanya kazi na kampuni za dola hizo, kwa sababu uhusiano pamoja na wapiganaji halisi ni uhusiano wa kivita, sio wa amani wa kibiashara.
2. Kufanya kazi na taasisi zinazo amiliana na dola za kivita kivitendo unachunguzwa kama ifuatavyo:
a. Ikiwa mradi ambao taasisi hiyo inafanyia kazi ni wa dola zilizo kwenye vita kivitendo, hairuhusiwi kufanya kazi na taasisi hiyo kwenye mradi huo.
b. Iwapo mradi si wa dola za kivita, bali ni wa watu wenyeji, kama vile kujenga shule au kujenga barabara, basi dhambi ni juu ya taasisi hiyo inayo amiliana na dola za kivita, lakini kazi hiyo inaruhusiwa maadamu mradi huo sio wa dola zilizo za kivita kivitendo.
Jibu la Swali mnamo tarehe 24/07/2011:
"... Kuingia mkataba wa moja kwa moja na makampuni na mashirika ya dola zinazokalia kwa mabavu ardhi za Waislamu (zile ambazo ziko vitani kivitendo) hairuhusiwi, kwa sababu ni aina ya muamala na dola ambazo ni za kivita kivitendo. Ama kuhusu kuingia mkataba na serikali ya kieneo au shirika la kieneo lisilofungamana na dola inayokalia kwa mabavu lakini kuwa na uhusiano nalo, yafuatayo yanazingatiwa:
1. Ikiwa uhusiano unahusisha miradi ya kijeshi na dola inayokalia kimabavu, hairuhusiwi.
2. Ikiwa uhusiano unahusisha miradi ya kibiashara ambayo haina madhara kwa nchi, inaruhusiwa, lakini ni bora kuepukwa kutokana na shaka ya kuleta madhara.
3. Ikiwa mfanyikazi ameajiriwa na dola ya kieneo, lakini mkataba wake ni wa moja kwa moja na dola vamizi, hairuhusiwi.
4. Ikiwa mfanyikazi ameajiriwa na dola ya kieneo na mkataba wake uko na dola hiyo ya kieneo, basi inaruhusiwa, hata kama dola hiyo ya kieneo inapokea msaada wa kifedha kutoka kwa dola vamizi.
5. Ikiwa mfanyikazi ameajiriwa na dola ya kieneo, mkataba wake uko pamoja na dola ya ndani, lakini anapokea mshahara wake moja kwa moja kutoka kwa dola vamizi, hapo hairuhusiwi.
Dalili ya hili ni hukmu za kuamiliana na dola ambazo ziko katika vita kivitendo."
Nataraji hili linatosheleza, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi na ni Mwingi wa hekima.
Ndugu Yenu,
Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah
12 Muharram 1447 H
Sawia na 07/07/2025 M
Link ya jibu kutoka ukurasa wa Amiri wa Facebook.