Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kukamatwa kwa Mamia ya Waandamanaji Wanaounga Mkono Palestina kwa Amani nchini Uingereza Yaonyesha Uhalisia wa Kinaya cha Demokrasia

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Jumamosi, tarehe 6 Septemba, karibu watu 900 walikamatwa katika maandamano ya kuunga mkono Palestina jijini London. Walikuwa wakipinga kuendelea kwa mauaji ya halaiki na njaa kwa raia wasio na hatia mjini Gaza, pamoja na kupigwa marufuku kwa kundi la Palestine Action ambalo serikali ya Uingereza iliharamisha kuwa shirika la kigaidi mwezi Julai. Waliokamatwa ni pamoja na maaskofu, makasisi, walimu, madaktari, wahudumu wengine wa afya, na vizazi vya wahanga wa mauaji ya Holocaust pamoja na waandamanaji walemavu. Wengi walikuwa wazee – katika miaka yao ya 60, 70 na hata 80 – na walijumuisha mzee mmoja kipofu mwenye umri wa miaka 62 aliye katika kiti cha magurudumu.

Mamia ya waandamanaji wa amani walifukuzwa na maafisa wa polisi kwa sababu tu ya kushikilia nembo inayosema – “Napinga mauaji ya halaiki. Naunga mkono Palestine Action”. Zaidi ya watu 700 walikamatwa katika maandamano ya awali kama hayo dhidi ya mauaji ya halaiki yanayoendelea Gaza kwa kuunga mkono shirika hilo.

Maoni:

Palestine Action ni shirika lenye makao yake nchini Uingereza ambalo limesema kuwa lengo lake ni “kukomesha ushiriki wa kimataifa katika “serikali ya mauaji ya halaiki na ubaguzi wa rangi ya Israel”, kama vile kusitisha usambazaji wa silaha kutoka Uingereza hadi kwa umbile la Kizayuni. Hii ni pamoja na kuvuruga operesheni ya watengenezaji silaha wanaohusishwa na uvamizi huo, kwa mfano, mkono wa Uingereza wa Elbit Systems, ambayo ni mtengezaji silaha  mkubwa wa umbile la Kizayuni. Baadhi ya wanachama wake wamechukua hatua ya moja kwa moja katika kujaribu kufikia malengo yake, ikiwemo kuingia ndani ya kambi ya anga ya RAF Brize Norton mnamo Juni na kuziharibu ndege 2 aina ya Voyager ambazo shirika hilo lilisema ni kulaani dhidi ya uuzaji silaha wa serikali kwa uvamizi huo. Iliripotiwa kuwa kambi hiyo ya anga ilitumiwa na ndege za kivita za ‘Israel’ zilizohusika katika ulipuaji wa Gaza. Kundi hilo lilipigwa marufuku kama shirika la kigaidi punde tu baada ya tukio hili, na kufanya uanachama au kuonyesha uungaji mkono wa umma kwa kundi hili ni kosa la jinai lenye adhabu ya miaka 14 gerezani.

Kufuatia marufuku hii, mamia ya waandamanaji wamekamatwa chini ya Sheria ya Ugaidi katika maandamano ya amani ya Palestina kwa kuonyesha uungaji mkono wowote au uhusiano na shirika hilo. Huko nyuma mwezi wa Mei 2024, ule unaoitwa uhakiki ‘huru’ wa serikali kuhusu ghasia za kisiasa na usumbufu ililinganisha kundi la Palestine Action na “makundi ya kigaidi” na kupendekeza amali zao zipigwe marufuku. Cha kushangaza ni, mwandishi wa uhakiki huo, John Woodcock, alikuwa mshauri alayelipwa kwa makundi ya ushawishi ambayo yanawakilisha watengenezaji silaha, pamoja na kuwa mwenyekiti wa zamani wa kundi la Labor Friends of Israel.

Ukweli kwamba serikali ya Uingereza haioni aibu katika kuwakamata mamia ya waandamanaji wa amani wanaoandamana dhidi ya mauaji ya halaiki na njaa ya watu huko Gaza, huku wakati huo huo ikishiriki katika mauaji haya ya halaiki kwa kuruhusu utengenezaji wa silaha na uuzaji wa silaha ili kulisaidia, unaonyesha kikamilifu ombwe la maadili, ukatili mkubwa na kinaya cha mfumo wake wa kidemokrasia. Mashirika mengine katika siku za nyuma yalichukua hatua za moja kwa moja kwa ajili yao, wakiwemo wapiganaji, wanaharakati wa hali ya hewa, na makundi ya haki za wanyama, hata hivyo, ukweli kwamba sheria za ugaidi zinatumiwa dhidi ya mashirika ambayo yanaunga mkono ukombozi wa Palestina, inabainisha kuwa marufuku hiyo inalenga hasa kuwanyamazisha wale wanaopinga uvamizi wa Kizayuni na kushiriki kwa serikali ya Uingereza katika mauaji haya ya halaiki. Kerry Moscogiuri wa shirika la kampeni ya kutetea haki za binadamu la Amnesty international Uingereza alisema: “Wakati serikali inapowakamata watu chini ya sheria za ugaidi kwa kukaa kwa amani katika maandamano, kuna kitu kinakwenda mrama sana hapa Uingereza.”

Mbali na waandamanaji wa wanaoiunga mkono Palestina kwa amani kukamatwa na kuwekwa kizuizini, wahadhiri wa vyuo vikuu, madaktari na wataalamu wengine nchini Uingereza wamesimamishwa kazi na wanafunzi kulazimishwa kuacha kozi zao kwa kukashifu uvamizi na uungaji mkono wa Wazayuni kwa ajili ya ukombozi wa Palestina. Ukosefu huu wa uadilifu umeakisiwa katika nchi nyingine za kidemokrasia, zikiwemo Amerika na Ujerumani.

Yote haya yanadhihirisha kinaya wazi cha ‘Uhuru wa kujieleza’ ndani ya dola kama hizo za kidemokrasia ambazo hutetea na kuhutubia ulimwengu kuhusu ukuu wa maadili yao ya kiliberali, lakini kiuhalisia, wako tayari kuyakanyaga na kuyatupilia mbali pale maslahi yao ya kisiasa na kiuchumi yanapotishiwa. Hii ni kwa sababu, chini ya mfumo wa kibepari, wa kisekula, wa kidemokrasia, manufaa ya kisiasa na kifedha daima yatatawala juu ya masuala mengine yote, ikiwemo kulinda utakatifu wa uhai wa mwanadamu. Ni wazi kwamba maadili na imani za nchi za kidemokrasia zinaweza kubadilika na kutupwa mithili ya dhamiri ya maadili ya serikali yanaziongoza! Mfumo wa kidemokrasia unatoa dhana kuwa mamlaka yanatolewa kwa watu, ilhali uhalisia ni kwamba yamewekwa imara mikononi mwa watawala au kipote cha matajiri ambao huunda sheria na sera kulingana na maslahi yao ya kibinafsi ya kisiasa na kiuchumi. Hata uhuru wa kusema hutolewa na kuchukuliwa kutoka kwa watu kulingana na kile kinachofaa kisiasa kwa serikali wakati huo. Zaidi ya hayo, uwajibikaji wa kweli kwa wale walio katika utawala ni ndoto tu – ambapo wale wanaohusika na kuupa silaha uvamizi wa mauaji ya halaiki wanaweza kuepuka athari zozote za kisiasa au mahakama!

Haya yote yanapaswa kutoa funzo la wazi kwetu sisi Waislamu, kwamba mfumo wa kidemokrasia uliobuniwa na mwanadamu, hata uwe na umbo aina gani hauwezi kamwe kuhakikisha haki kwa watu, wala hauna uti wa mgongo wa kimaadili wa kukomesha mauaji ya halaiki. Utoaji wa haki hautabiriki na unaweza kubadilika, na kuna mstari mwembamba kati ya demokrasia na ubabe, kama inavyoonekana nchini Amerika kwa sasa, na dola zengine mbalimbali za kidemokrasia. Kukomesha mauaji ya halaiki mjini Gaza na kuondoa uvamizi wa Kizayuni kunahitaji kusimamishwa kwa dola ambayo inajali kweli maisha ya mwanadamu, na inasimama kwa ajili ya ubinadamu na dhidi ya dhulma na ukandamizaji wa aina zote, bila kujali athari za kifedha. Inahitaji dola ambayo ni mlinzi wa Waislamu na Dini yetu na inayotumia jeshi lake kupigania kadhia yake. Dola hii ni Khilafah kwa njia ya Utume inayotawala kwa Qur’an na Sunnah pekee.

Kwa hivyo, ikiwa tunataka kuona mwisho wa mauaji ya Ummah wetu nchini Palestina, Kashmir, Sudan, Yemen na kwengineko, tunapaswa kufanya kazi kwa dharura kwa ajili ya kuregeshwa kwa dola hii, ikiwa ni pamoja na kuwataka walio katika majeshi ya Waislamu watoe Nusrah yao (msaada wa kimada) kwa ajili ya kuasisiwa kwake bila kuchelewa!

[وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَعْمَالُهُمْ كَسَرَابٍ بِقِيعَةٍ يَحْسَبُهُ الظَّمْآنُ مَاء حَتَّى إِذَا جَاءهُ لَمْ يَجِدْهُ شَيْئًا]

“Na walio kufuru vitendo vyao ni kama sarabi (mazigazi) uwandani. Mwenye kiu huyadhania ni maji. Hata akiyaendea hapati chochote.” [An-Nur: 39]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Asma Siddiq
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.