- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Uislamu ni Ujumbe kwa Wanadamu Wote!
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mnamo tarehe 7 Agosti, Kituo cha Hadhara ya Kiislamu nchini Uzbekistan chini ya Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Uzbekistan kilichapisha ujumbe kwenye ukurasa wake wa tovuti kwamba: “Nakala ya barua ya Mtume wetu iliyotumwa kwa Mfalme wa Roma itawekwa hadharani kwenye Kituo cha Hadhara ya Kiislamu.
Risala za kidiplomasia zilizotumwa na Mtume Muhammad (saw) katika mchakato wa kueneza Uislamu na kuwalingania wanadamu kwenye tawhid zina thamani spesheli ya kihistoria. Yeye (saw) alituma barua kwa viongozi wa dola zinazoongoza duniani, akiziweka ithbati kwa muhuri wake.
Ufichuzi wa Kituo cha Hadhara ya Kiislamu utawasilisha ujenzi upya uliothibitishwa kisayansi wa mojawapo ya nyaraka za kipekee za kiroho na za kihistoria za barua iliyotumwa kwa Mfalme Irakli (Heraclius).
Pia imepangwa kuonyesha nakala za barua zilizotumwa kwa watawala wa Ethiopia, Misri, Bahrain, Oman na Shah wa Fursi. Barua hizi sio tu uthibitisho wa roho ya amani na kidiplomasia ya Uislamu, bali pia ni ushuhuda wa wazi wa hekima ya kisiasa na ubinadamu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)”.
Maoni:
Baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kumpa nusra kipenzi chetu Mtume Muhammad (saw) na kuwafungulia Waislamu Madina al-Munawwara, yeye (saw) alianza kutabikisha Uislamu katika maisha na kueneza ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa wanadamu wote, kwani Uislamu ni dini ya ulimwengu na Mtume Muhammad (saw) alitumwa kwa watu wote. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]
“Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui.” [34:28]
[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]
“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [9:33]
Baada ya Dola ya Kiislamu mjini Madina kumakinishwa, kazi iliyofuata ya Mtume (saw) ilikuwa ni kuanzisha mahusiano ya kigeni na dola jirani. Mahusiano ya kigeni yalimaanisha mahusiano ya dola ya Kiislamu na makafiri waliokuwa wakiishi nje ya mipaka yake na kuufikisha kwao Uislamu. Mwanzoni, eneo la dola lilifungika Madina tu, na sera ya kigeni ilijumuisha mahusiano na makabila yaliyo karibu na mipaka yake. Wakati dola ya Uislamu ilipoenea katika Hijaz yote, duara la sera ya kigeni lilijumuisha mahusiano na watu walioishi nje ya mipaka yake. Na pindi dola ya Uislamu ilipoenea kwenye Bara nzima yl Arabu, mahusiano ya sera ya kigeni yalianza kujumuisha dola kuu za wakati huo, kama vile Fursi na Byzantium.
Mtume (saw) alianza kutuma wajumbe wake nje ya Bara Arabu baada ya utaratibu wa ndani kuregeshwa na dola kuwa na nguvu za kutosha kwa ajili ya sera ya kigeni. Mtume (saw) alipokinaika kwamba Maswahaba zake watukufu (ra) walikuwa tayari kutekeleza kazi hii, akaanza kutuma risala kwa nchi jirani na himaya za dunia za wakati huo. Hivi ndivyo Waislamu walivyoeneza Uislamu kwa kutimiza amri ya Mwenyezi Mungu!
Leo hii, watawala mafisadi na wasio na thamani ambao wamejinyakulia madaraka katika ardhi za Waislamu kwa kujidai kuwa wao ndio viongozi wa Uislamu, wanaonyesha na kujifakharisha juu ya mafanikio ya Waislamu huko nyuma, kuwa ni tunu za kihistoria na kiroho, bila ya kuhusisha amri za Shariah kwao wenyewe na mfumo wao wa utawala. Wanazitumia hisia za Waislamu kwa kuwalaza usingizi na kuzikandamiza hasira zao, ambazo hukimbilia uhuru na kujitahidi kutabikisha Shariah katika maisha yao.
Kwa nini wanafanya hivi? Hiii ni kwa sababu mfumo wao wa serikali, na wao wenyewe hawana uhusiano wowote na Uislamu na Waislamu. Mtawala wa Kiislamu huwachunga watu wake kwa msingi wa Uislamu, kuwalinda watu wake na kulinda ardhi dhidi ya kushambuliwa na wakoloni makafiri. Mfumo wa utawala wa Kiislamu ni Khilafah, unaoeneza ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu mzima kupitia Dawah na Jihad!
Na kwa hivyo, ni wajibu juu yetu Waislamu kuzifagia tawala zote hizi vikaragosi, kuhuisha utawala wa Kiislamu kupitia njia ya kipenzi chetu Mtume Muhammad (saw), kumuweka mtawala muadilifu na kwa mara nyengine tena kuanza kueneza Uislamu duniani kote kwa njia ya Dawah na Jihad! Tunamuomba Mwenyezi Mungu atusaidie!
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir