Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  16 Sha'aban 1444 Na: HTY- 1444 / 17
M.  Jumatano, 08 Machi 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ukambi Unawaua Watoto wa Yemen na Watawala wao hata Hawajali
(Imetafsiriwa)

Utafiti umetaja "kurudi kwa ukambi nchini Yemen" uliofanywa na mtafiti na mtaalamu wa ukambi, Dkt. Reem Al-Khashab, ambao matokeo yake yalichapishwa Machi mwaka jana, na kuthibitisha kusajiliwa kwa visa 5,000 vya ukambi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Utafiti huo ulionyesha kuwa idadi ya vifo kutokana na ukambi ilifikia 53 katika mwaka wa 2021, na kwamba 79% ya vifo ni kati ya watoto chini ya miaka mitano.

UNICEF pia ilithibitisha, katikati ya mwezi wa Disemba, vifo vya watoto 15 kutokana na ukambi nchini Yemen mwaka 2022, wakati wa ufuatiliaji wa visa vya maambukizi, kati ya Januari na Julai 2022, huku maambukizi yakifikia takriban watoto 1,400, kati yao 15 walikufa kwa sababu ya ugonjwa huo katika majimbo 7, ikiwa ni pamoja na Aden. Kuhusu idadi ya watu walioambukizwa ukambi nchini Yemen katika mwaka wa 2022, Wizara ya Afya ya serikali ya Sana'a ilitangaza Disemba mwaka jana kwamba kesi 18,597 zimerekodiwa, ambapo 131 walikufa. Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, ilitoa wito kwa mashirika ya kimataifa yanayofanya kazi nchini Yemen kuusaidia mfumo wa afya na kuzingatia kuimarisha hali ya kuwa tayari kwa magonjwa ya milipuko kama kipaumbele.

Yemen inakuja katika nafasi ya pili katika takwimu zilizotajwa na UNICEF, mwezi Aprili 2022, ambazo zilijumuisha zaidi ya nchi 5 zinazokumbwa na ongezeko la wagonjwa wa ukambi, huku visa nchini Yemen vikifikia 9,068.

Ukambi ni ugonjwa unaoambukiza sana ambao huathiri watoto. Karibu kila mtu anayeupata ana upele wenye uchungu, macho yanayouma, homa, misuli migumu na kikohozi kibaya. Wengi wa watoto walio katika hatari ya kuambukizwa ukambi ni wale wanaokabiliwa na utapiamlo.

Hali nchini Yemen na nchi nyengine imefikia jinsi ilivyo chini ya mfumo wa kibepari ambao hauwapi watu thamani yoyote kwa badali ya kufikia maslahi ya wale wanaowatawala watu kwayo. Watawala nchini Yemen na nchi nyengine za Kiislamu, na kupuuza kwao mambo ya Ummah, si chochote ila ni matokeo ya mfumo huo mbovu wa matumizi. Haya yote si chochote bali ni matokeo ya kimaumbile ya mtazamo wa kibepari wa maisha. Kupenda mali na manufaa ndio vigezo vyake, na muamala wa milki ya kifikra na sheria ndio matokeo yake. Mtazamo huu sio tu unatoa kipaumbele kwa thamani ya kimada, lakini pia huunganisha thamani zengine ili kuifanikisha. Yote haya ni kwa sababu ya msingi mbovu ambao kwao miamala hii ya kifisadi inachipuza ambayo imewatumbukiza wamiliki wake na dunia nzima katika uovu na dhulma.

Ama Uislamu, uliilazimisha dola kukidhi mahitaji ya kimsingi ya raia, yakiwemo matibabu, ambapo serikali inatoa huduma ya matibabu kwa kila mtu bila ya kutofautisha baina ya tajiri na masikini, au kati ya mfanyikazi na mtu asiye na kazi, na gharama zote zinazotumika hulipwa kutoka hazina ya dola. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«الْإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Mtawala ni mchungaji wa raia wake na ataulizwa kuwahusu.” Dawa ni mojawapo ya maslahi na huduma ambazo watu hawawezi kuishi bila, kwani ni moja ya mahitaji. Yeye (saw) amesema:

«‏مَنْ أَصْبَحَ مِنْكُمْ مُعَافًى فِي جَسَدِهِ، آمِناً فِي سِرْبِهِ، عِنْدَهُ قُوتُ يَوْمِهِ، فَكَأَنَّمَا حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا»

Yeyote miongoni mwenu atakayepambaukiwa akiwa na afya njema, akijisikia salama na amani ndani ya nyumba yake, akiwa na chakula cha siku yake, ni kana kwamba amemiliki ulimwengu nzima.” Mtume (saw) aliifanya afya kuwa ni hitaji la lazima, kwa hoja kwamba kutotoa dawa kwa kundi la watu kunaleta madhara, na kuondoa madhara ni wajibu kwa serikali. Yeye (saw) amesema:

«لَا ضَرَرَ وَلَا ضِرَارَ»

“Hakuna kudhuru wala kudhuriwa.”

Kwa mtazamo huu, matibabu pia yalikuwa ni jukumu la serikali. Juu ya hayo, Mtume (saw) alipewa daktari, hivyo akamfanya kuwa wa Waislamu. Ukweli kwamba Mtume alipewa zawadi na hakuitupa wala hakuichukua, bali aliifanya kuwa ya Waislamu, ni dalili kwamba zawadi hii ni kwa jumla ya Waislamu na si kwa ajili yake.

Mzizi uliooza, unaozaa matawi yanayomomonyoka na matunda mabovu, lazima ung'olewe na badala yake mti upandwe mwema wa Uislamu, na mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu uregeshwe tena kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa Njia ya Utume ambayo Hizb ut Tahrir inaifanyia kazi, ambayo ilitoa kitabu kiitwacho “Sera ya Huduma ya Afya katika Dola ya Khilafah”; ili itabikishwe mara tu itakaposimamishwa, Mwenyezi Mungu akipenda,

[وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَرِيباً]  

“na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!” [Al-Israa: 51].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.