Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  25 Safar 1444 Na: HTY- 1444 / 03
M.  Jumatano, 21 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Chama cha Ushirika wa Kilimo cha Saada nchini Yemen

Ukiukaji wa Hukmu za Uislamu na Uhuishaji wa Wazo la Vyama vya Ushirika
(Imetafsiriwa)

Ijapokuwa takriban miezi miwili imepita tangu kuzinduliwa kwa natija nyingi za Chama cha Ushirika wa Kilimo cha Saada, Usajili bado ungali wazi hadi leo kwa kiwango cha elfu kumi kwa kila hisa. Hivyo basi, ni lazima tufafanue uhalisia wa vyama hivyo ambavyo vinakiuka hukmu za Sharia tukufu, na ili kuhakikisha kwamba watu wa Yemen hawaanguki ndani makosa yao hatari.

Vyama vya Ushirika (co-ops) ni aina ya kampuni ya kirasilimali, hata kama inaitwa ushirika. Ni kampuni ya hisa kati ya kikundi cha watu, ambao wamekubaliana kati yao kutenda kwa pamoja kulingana na shughuli zao wenyewe. Ushirika hutokea katika muundo wa kawaida wa kibiashara kwa lengo la kusaidia wanachama wake, au kuhakikisha maslahi yao maalum ya kiuchumi, na ushirika hupata utu wa kisheria wa kampuni. Kwa hivyo, inatofautiana na vyama vyengine kwa kuwa vyama hivi kiasili ni dhahania kutoka kwa madhumuni ya kiuchumi. Ushirika hufanya kazi ya kukuuza faida ya wanachama wake, na sio maslahi ya wengine, ambayo inahitaji kuunda fungamano thabiti kati ya shughuli zake za kiuchumi na uchumi wa wanachama. Chama cha ushirika kinaundwa na zaidi au chini ya idadi ya wanachama, lakini hakiundwi na watu wawili pekee.

Viko aina mbili:

Aina ya kwanza: kampuni iliyo na hisa za msingi, ambapo mtu yeyote anaweza kuchukua wadhifa wa mshirika, kupitia kumiliki hisa hizi.

Aina ya pili: kampuni isiyo na hisa za msingi, ambayo ushiriki wake ni kupitia kulipa ada ya usajili ya kila mwaka, itakayoamuliwa na chama jumla kwa ajili yake katika kila kikao cha mwaka.

Ushirika lazima ukidhi masharti matano:

Moja: uhuru wa kushiriki katika ushirika; mlango wa ushiriki unabaki wazi kwa mtu yeyote chini ya masharti yale yale yanayotumika kwa wanachama waliotangulia, na kwamba kanuni, vikwazo na usajili wa ushirika vinatekelezeka kwa mwanachama, iwe vikwazo hivi ni vya asili, kama vile watu wa kijiji; au ni vya kitaaluma, kama vile maseremala, kwa mfano.

Pili: vyama vya ushirika vina haki sawa; muhimu zaidi ya haki hizi ni kupiga kura, ambapo kila mshirika anapewa kura moja.

Tatu: kuamua maslahi maalum kwa hisa; baadhi ya vyama vya ushirika huwalipa wenyehisa wa kudumu riba maalum, ikiwa faida yao itaruhusu.

Nne: mapato ya faida za ziada za uwekezaji; faida halisi itaregeshwa kwa wanachama, kulingana na kiwango cha shughuli walizofanya na ushirika, kuanzia kwenye ununuzi au matumizi ya huduma za ushirika na vifaa vyake.

Tano: ulazima wa kutengeneza utajiri wa ushirika kupitia kuhamisha hifadhi.

Huu ndio uhalisia wa vyama vya ushirika, ambavyo ni vyama batili vinavyogongana na hukmu za Uislamu kutokana na mambo yafuatayo:

1- Jumuiya ya ushirika ni kampuni, kwa hivyo lazima itimize masharti ya kampuni yaliyoainishwa na Sharia ili iweze kuwa halali. Na kampuni katika Uislamu ni mkataba kati ya wawili au zaidi, ambao wanakubali kufanya kitendo cha kifedha kwa nia ya kupata faida, na kwa hiyo kampuni lazima iwe na mwili, yaani chama au kampuni lazima isimamiwe na angalau mmoja wa washirika, mtu ambaye anamiliki na kutumia, na hivyo lazima kuwe na mwili ili hata iitwe kampuni kwa mujibu wa hukmu ya Sharia. Vyama vya ushirika sio makampuni halali, kwa sababu ni makampuni yanayotegemea fedha peke yake, na hayana mwili wa mshirika, na makubaliano yalifikiwa baina ya wanachama wao kuweka fedha fulani na kisha kutafuta usimamizi ya kufanya kazi hiyo. Kampuni ni mkataba juu ya utumiaji wa pesa na utumiaji unaweza tu kutoka kwa mwili, na ikiwa haina mwili, ni kampuni batili.

2- Kugawanya faida kwa kiwango cha ununuzi, au kulingana na uzalishaji, sio kwa kiwango cha mtaji au kazi, hairuhusiwi, kwani ni sharti fisidifu.

Kurudi kwa vyama hivi leo nchini Yemen ni kufufuliwa kwa vyama vya ushirika ambavyo wazo lake lililetwa na Magharibi nchini Yemen wakati wa siku za Rais Al-Hamdi katika miaka ya sabiini, na kuendelea hadi miaka ya themanini, na ambavyo asili yake vinagongana na Uislamu kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine vilifanya kazi ya kupotosha fikra za watu juu ya kufanya kazi ili kusimamisha dola inayosimamia mambo yao na yanayopaswa kushughulikiwa kwa ukamilifu na wajibu juu yao, badala ya kukimbizana na sarabi ya udanganyifu ambayo wanadhani ni maji yasiyo kata kiu wala kukidhi njaa kwani nyinyi, enyi watu wa Yemen, hamna lolote ila Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume inayosimamia mambo yenu, inayolinda damu yenu na kumridhisha Mola wenu Mlezi. Basi kunjeni mikono ya mashati yenu na mfanye kazi na Hizb ut-Tahrir kuisimamisha ili mpate ujira mkubwa, kwani nyinyi mnastahiki hayo.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.