Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  2 Rajab 1444 Na: BN/S 1444 / 07
M.  Jumanne, 24 Januari 2023

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi kutoka Kizazi cha Kwanza katika Hizb ut Tahrir

[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab:23]
(Imetafsiriwa)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina inamuomboleza mmoja wa wanaume wa Hizb ut Tahrir, mbebaji da’wah kutoka kizazi cha kwanza katika safu zake, aliyesamehewa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu:

Hajj Muhammad Khalil Qasim (Abu Khalil)

Ambaye amefariki dunia kwenda kwa rehema za Mwenyezi Mungu leo Jumanne, 24 Januari 2023, akiwa na umri wa miaka 92, ambaye alitumia muda mwingi wa maisha yake kubeba da’wah. Hajj Abu Khalil, Mwenyezi Mungu amrehemu, alijiunga na dawah katika miaka ya 1950 katika safu za kwanza za Hizb ut Tahrir ambaye ametumia maisha yake kubeba ulinganizi wa Uislamu na kufanya kazi ya kusimamisha tena Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, katika matendo yake yote (ya ndani ya nchi na akiwa safarini). Yeye, Mwenyezi Mungu amrehemu, alikuwa ni mshale kati ya mishale ya kazi ya kuregesha tena mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu, mtiifu, mwaminifu na mstahimilivu kwa ajili ya dawah hiyo, kifungo na matatizo, kutwikwa kazi nyingi za idara katika hizb, kutoa na kutumia kwa ajili ya ulinganizi huu maisha na mali yake.

Hata pamoja na uzee wake, aliendelea kuwa na bidii, mvumilivu, akishiriki katika amali, kusoma taarifa kwa vyombo vya habari na machapisho, akiwapenda Mashababu na kuwa mwandani kwao, akiwaombea dua nao wakimuombea kila kheri, upendo na uadilifu. Mwenyezi Mungu amrehemu Abu Khalil, kwani aliishi kwa kudumisha ahadi yake na Mwenyezi Mungu hadi dakika za mwisho za uhai wake, na akafa katika hali hiyo, akiwaacha nyuma watoto wema ambao wanabeba ulinganizi, wanaupenda Uislamu, na kufanya kazi kuuinua ili kuwa sifa kwake na katika mizani ya mema yake, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu amrehemu maiti wetu, amjaalie rehema pana zaidi, na akae katika mabustani yake (swt) mapana. Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake tutaregea. Mwenyezi Mungu (swt) awalipe mema familia yake na jamaa zake na awatie moyo wa subira na faraja.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

- Risala za Wanachama wa Hizb ut Tahrir katika Mazishi ya Hajj Muhammad Khalil Qasim (Abu Khalil) -

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.