Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Australia

H.  22 Rabi' I 1447 Na: 02 / 1447 H
M.  Jumapili, 14 Septemba 2025

Tanzia na Rambirambi kwa Kifo cha Khaled Ahmed Ibrahim Trad (Abu Muhammad)
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir nchini Australia inaomboleza kifo cha mmoja wa watu ambaye mapenzi yake kwa Quran, Waumini na Dawah yaliwagusa watu wengi katika jamii (Mwenyezi (swt) amrehemu):

Ndugu Khaled Ahmed Ibrahim Trad (Abu Muhammad)

ambaye alifariki dunia kwenda kwenye rehema za Mwenyezi Mungu (swt) leo, Jumapili tarehe 22 Rabi' al-Awwal 1447 H, sawia na tarehe 14 Septemba 2025 M.

Tunatoa rambirambi zetu kwa familia ya marehemu na wabebaji da’wah wote. Tuwamuomba Mwenyezi Mungu (swt) amfinike kwa rehema yake kubwa, ammiminie radhi na msamaha Wake (swt) na amruzuku mabustani yake makubwa pamoja na mitume, wakweli, mashahidi na watu wema. Hatimaye twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awalipe mema familia yake na jamaa zake na awape subira na faraja.

Hakika macho yanabubujika machozi na moyo unahuzunika, lakini hatutasema isipokuwa yanayomridhisha Mola wetu Mlezi.

[إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah: 156].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 0438 000 465
www.hizb-australia.org
E-Mail:  media@hizb-australia.org

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.