- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Al-Waqiyah TV: Kwa Nini Kuwahisabu Watawala ni Faradhi ya Kisheria
[Al-Waqiyah TV]
“Kwa Nini Kuwahisabu Watawala ni Faradhi ya Kisheria?”
Unapomteua mtu wa kutekeleza jukumu ambalo asili yake ulikabidhiwa, hii ina maana kwamba ni wajibu wako wa Shariah kumfuatilia na kumhisabu ikiwa ameghafilika, anafanya makosa, au anadhulumu, na kadhalika. Ni jambo la kawaida kwa Ummah kuendelea kuwa macho juu ya mtawala. Haya ni faradhi yake ya Shariah na Shariah yake kwa wakati mmoja. Maana ya faradhi yake ya Shariah ni kuwa Ummah utakuwa ni wenye dhambi ukilipuuza hili. Haki yake Shariah ni kwamba mtawala atatenda dhambi ikiwa atauzuia kutekeleza wajibu wa kuhisabu, ufuatiliaji, na ushauri, na kadhalika. Kama vile Ummah unavyomchagua mtawala wa kuuwakilisha katika kutekeleza Shari’ah, wajibu wake wa Shariah ni kubakia katika hali ya kumuangalia, kumfuatilia, katika njia ya ushauri na mapendekezo, na katika njia ya uwajibikaji, ikiwa amefanya kosa, akapungukiwa, au alikuwa dhalimu, na kadhalika. Inaweza kufikia hatua kwamba uhalali wa Shariah wa mtawala huyu umepotea na lazima aondolewe. Bila shaka, uondoaji huu pia una utaratibu wa Shariah, ambao tunaweza kuujadili katika ibara za kikatiba zijazo, Mwenyezi Mungu ﷻ akipenda. Ama kuhusiana na uwajibikaji na ufuatiliaji, ushahidi wa jambo hili ni mwingi, kama vile Hadith ya Mtume (saw) isemayo: “Lazima muwaamrishe watawala juu ya haki, na muwafunge watawala kwenye haki.” Kwa jumla, Hadith zinazoamrisha kuamrisha mema na kukataza maovu kimaumbile zinajumuisha, na kutoka kwa mtazamo wa kipaumbele (baab ul-awlah) watawala, kwa sababu watawala wakifanya mema, wema wao huakisi wema juu ya mambo yote, na wakifanya maovu, uovu wao huakisi uovu kwa wahusika wote, na hata juu ya uadilifu wa Uislamu, kwa kuwa Umma wa Kiislamu umepewa amana ya kuutekeleza Uislamu, kuuwasilisha kwa watu, na kuwalingania watu kwa Uislamu. Hivyo watawala lazima wawe juu ya vipaumbele katika kuamrisha mema na kukataza maovu. Nadhani msemo mashuhuri ulipokewa kutoka kwa Imam Malik au mmoja wa Maimamu wengine wakubwa, ili nisikosee, akasema, “Lau ningejua kwamba Dua fulani itajibiwa, ningeifunga kwa watawala,” kwa sababu anajua jinsi ilivyo hatari kwa mtawala kukengeuka, na kwa matendo yake au mazoea yake kuwa mabaya. Kosa hapa si juu ya nafsi yake tu, bali ni dhidi ya Ummah wote, hakika ni dhidi ya mataifa, kwani inahusika na kuuwasilisha Uislamu kwao ukiwa mtakatifu, safi, na wenye kung'aa, kama vile Mwenyezi Mungu ﷻ alivyoupenda na akauridhia kwetu sisi.
Imewasilishwa na: Ustadh Ahmad Al-Qasas
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Ijumaa, 07 Safar 1447 H - 01 Agosti 2025 M