Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari: 06/04/2022

Vichwa vya Habari:

• Mauaji ya Halaiki Nchini Ukraine?

• ‘Israel’, UAE Zakamilisha 'Malengo' ya Mkataba wa Biashara Huru

• Mfumko wa Bei wa Uturuki

Maelezo

Mauaji ya Halaiki Nchini Ukraine?

Mamlaka za Ukraine zilitoa picha na video zinazoonyesha maiti zikiwa zimelala kwenye barabara za mji wa Bucha karibu na Kyiv baada ya vikosi vya Urusi kuondoka eneo hilo. Kyiv alikiita kile kilichotokea huko kuwa mauaji ya halaiki na kuzitaka nchi za Magharibi kuweka vikwazo zaidi dhidi ya Moscow. Wizara ya Ulinzi ya Urusi, hata hivyo, iliziita picha hizo "uchochezi wa wazi" na kutaka mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Picha za maiti waliofungwa pingu wakiwa wamelala kifudifudi barabarani au makaburi yaliyochimbwa kwa haraka mjini Bucha ziliibua wimbi la hasira, viongozi wa Ulaya waliungana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy katika kuyaita mauaji ya halaiki. Vita vya propaganda vimepamba moto sasa na kwa miezi kadhaa Urusi imekuwa ikijitahidi kutawala mawimbi ya anga. Ikiwa Urusi yahitaji kuhukumiwa kwa uhalifu wa kivita, basi kwa sababu kubwa zaidi nchi za Magharibi zahitaji kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kampeni za mauaji nchini Iraq, Afghanistan, na Syria.

‘Israel’, UAE Zakamilisha 'Malengo' ya Mkataba wa Biashara Huru

'Israel' na Umoja wa Milki za Kiarabu zimehitimisha mazungumzo ya makubaliano ya biashara huria, 'Wizara ya Uchumi ya Israel na Waziri wa Biashara ya Nje wa UAE walisema mnamo Ijumaa baada ya kuanzisha rasmi uhusiano mwaka 2020. Makubaliano ya hivi karibuni yalijumuisha 95% ya bidhaa zinazouzwa, ambazo zitakuwa bila malipo ya forodha, mara moja au polepole, ikiwa ni pamoja na chakula, kilimo na bidhaa za vipodozi, pamoja na vifaa vya matibabu na dawa, Wizara ya Uchumi ya 'Israel' ilisema katika taarifa. Mkataba huo ulijumuisha udhibiti, forodha, huduma, ununuzi wa serikali na biashara ya kielektroniki na utaanza kutekelezwa utakapotiwa saini na mawaziri wa uchumi wa nchi na kuidhinishwa, ilisema taarifa hiyo, ingawa hakuna ratiba iliyotolewa. "Mkataba huu muhimu utajengwa juu ya Makubaliano ya kihistoria ya Abraham na kuimarisha moja ya uhusiano muhimu zaidi na wa mafanikio wa kibiashara unaoibukia," Waziri wa Biashara ya Nje wa Umoja wa Milki za Kiarabu Thani Al Zeyoudi alisema kwenye Twitter.

Mfumko wa Bei wa Uturuki

Mnamo Machi, bei ya watumiaji nchini Uturuki iliongezeka kwa 61% kila mwaka, ikikaribia kupanda kwa miaka 20. Ongezeko la juu zaidi la kila mwaka mwezi uliopita lilikuwa katika usafiri (99%), vyakula na vinywaji visivyo na kileo (70%), na samani na vifaa vya nyumbani (69%). Kundi la Utafiti wa Mfumko wa Bei la Uturuki, au ENAG, mjumuiko wa wataalam wanaokokotoa viwango mbadala vya mfumko wa bei, walikadiria mfumko wa bei wa kila mwaka wa Uturuki wa mwezi Machi ulikuwa 143%. Mfumko wa bei wa kasi wa Uturuki unafuatia mfululizo wa kupunguzwa kwa kiwango cha riba mwishoni mwa mwaka jana, sambamba na upinzani wa Rais Recep Tayyip Erdogan dhidi ya gharama kubwa za kukopa katika jitihada za kukuza ukuaji, uwekezaji na mauzo ya nje. Tofauti na fikra ya kiuchumi iliyoanzishwa, rais anasisitiza kuwa viwango vya juu vinasababisha mfumko wa bei. Katika jitihada za kupunguza pigo kwa familia, serikali imetabikisha kupunguzo la ushuru kwa bidhaa za kimsingi na imerekebisha ushuru wa umeme. Erdogan alijilimbikizia sifa yake juu ya usimamizi wake wa uchumi, lakini hivi karibuni sehemu kubwa ya nyumba yake ya kadi imefichuka kwani ukuaji wa kiuchumi unaotokana na deni wa miongo miwili iliyopita sasa unamrudia tena kumuogofya.

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.