Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Siasa za Kidemokrasia zina Faida Sana kwa Wanasiasa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mwaka mmoja baada ya kashfa ya mbunge wa Uingereza Owen Paterson kupelekea ahadi za udhibiti mkali, wanasiasa wamevuna £5m kutokana na kazi ya pembeni, gazeti la ‘The Observer’ limeripoti.

Kwa ujumla, wabunge walipata zaidi ya £5.3m kutokana na kazi za nje kuanzia Oktoba 2021 na Septemba 2022, huku wengi, wakiwemo mawaziri wa zamani, wakichukua majukumu mapya kama washauri na wasio watendaji katika mwaka uliopita kwa makampuni ambayo katika kesi kadhaa yaliendeshwa na wafadhili wakuu wa vyama.

Wengi wameajiriwa katika maeneo waliyokuwa wakisimamia serikalini.

Waziri wa zamani wa elimu Gavin Williamson alichukua jukumu mnamo Juni kama mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya RTC Education Ltd, kampuni ya elimu ya kibinafsi ambayo mwenyekiti wake Maurizio Bragagni na mtendaji mkuu Selva Pankaj ni wafadhili wakuu wa chama cha Conservative. Williamson alitazamiwa kupata pauni £50,000 kwa mwaka kwa jumla ya kazi ya masaa 80.

Waziri wa zamani wa uchukuzi Chris Grayling alipata pauni £100,840 kutokana na kazi ya nje, hasa kutokana na kusalia katika jukumu lake la pauni £100,000 kwa mwaka kama mshauri wa kampuni ya usafirishaji wa meli ya Hutchison Ports, ambayo yeye hufanya kazi masaa saba kwa wiki.

Mwanasheria mkuu wa zamani Cox alipata ada ya zaidi ya £1m kama wakili, na alikabiliwa na mashtaka mwaka jana ya mgongano wa kimaslahi, baada ya kufichuliwa alikuwa ameshawishi dhidi ya udhibiti mkali wa kifedha katika Visiwa vya Cayman huku akipata makumi ya maelfu ya pauni kutoka kwa makampuni ya sheria yaliyo katika eneo la kodi.

Ajira za pili za wabunge zilikuwa sehemu ya mzozo mkubwa mwaka mmoja uliopita, baada ya kamishna wa viwango wa bunge kupatikana wakati huo akiwa Mbunge wa Conservative Owen Paterson akiwa amekiuka kanuni za maadili ya mawaziri kwa kutumia vibaya rasilimali, kujihusisha na ushawishi wa kulipwa na kukosa kufichua maslahi. Alipatikana kuwashawishi mawaziri kwa niaba ya Randox na kampuni nyingine zilizomlipa.

Maoni:

Katika wiki ambayo mkuu wa jeshi anayeondoka wa Pakistan Qamar Javed Bajwa na familia yake walifichuliwa kuwa wamejikusanyia zaidi ya dolari milioni 50 katika kipindi cha miaka sita madarakani, wengi katika nchi za Magharibi wanaweza kujaribiwa kunyoshea kidole cha lawama ufisadi huo kwa kulaani. Hata hivyo, je ni sawa kwa buli kukituhumu chungu kuwa cheusi?

Ufisadi katika siasa za Uingereza ni mkongwe kama vile bunge lenyewe. Licha ya mageuzi mengi yaliyopigiwa debe hadharani kwa serikali kuzisafisha siasa, bado ingali ni sehemu kubwa ya mfumo mbovu wa demokrasia. Kwani wabunge hao wenyewe ni miongoni mwa wanufaikaji wa rushwa, nafasi ya wao kihakika kutunga sheria na kutekeleza kihakika na kukomesha rushwa ni ndogo sana.

Uislamu hauruhusu viongozi waliochaguliwa kutunga sheria ambazo kwazo watahisabiwa. Mwenyezi Mungu alikiteremsha kitabu kilicho wazi kuwa ni uongofu na kigezo ambacho kwacho wanadamu wote wanapaswa kuhisabiwa.

Al-Bukhari na Muslim wamepokea kutoka kwa Abu Humaid Al-Sa’idi ambaye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alimteua Ibn al-Utbiyya kuwa ‘amil msimamizi wa zaka (Sadaqa) ya Banu Salim. Aliporudi kwa Mtume (saw) alisema: “Hii ni yako na (hii ni zawadi) niliyopewa.” Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema:

«فَهَلَّا جَلَسْتَ فِي بَيْتِ أَبِيكَ وَأُمِّكَ حَتَّى تَأْتِيَكَ هَدِيَّتُكَ إِنْ كُنْتَ صَادِقًا»

“Ungekuwa umekaa nyumbani kwa babako na mamaku mpaka ikakujia zawadi yako kama wewe ni mkweli.”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.