Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kukabiliana na Mayahudi ni jambo la Aqidah. Kujitayarisha kwa ajili yake Ni Faradhi ya Shariah, na Kuliepuka ni Maangamivu
(Imetafsiriwa)

Gazeti la Al-Rayah - Toleo 565 - 17/09/2025 M
Na: Ustadh Nasser Sheikh Abdul Hai*

Baadhi ya wanasiasa wa Syria hivi majuzi wamekuwa wakiendeleza wazo kwamba “hatutauza udanganyifu kwa watu wetu, na kwamba lazima tuchukue hatua ya kweli ili kujenga upya serikali.” Hili linafanywa kwa kisingizio kwamba “tunafahamu uwezo wetu wa kweli, na lugha ya vitisho haitakuwa na manufaa yoyote katika kukabiliana na uvamizi wa Kizayuni,” na kwamba “mazungumzo nao yanaendelea ili kuregea kwenye makubaliano ya 1974!”

Mbele ya madai haya ya kudhalilisha, ni lazima tukumbuke baadhi ya ukweli ulio wazi na dhahiri:

Sio udanganyifu kuwakumbusha watu juu ya ukweli wa kiitikadi, kisiasa, na msingi wa kiimani kwamba umbile la Kiyahudi ni umbile linalokalia kimabavu ambalo lazima likabiliwe, lishindwe, na matukufu ya Waislamu kusafishwa na uchafu wake. Hili linawezekana ikiwa tuna utashi, kwa sababu uwezo wote unapatikana kufanya hivyo, hasa baada ya mujahidina wa Gaza kufichua udanganyifu na uwongo wa ngano ya “jeshi lisiloshindwa” na kuthibitisha kwa idadi yao ndogo na vifaa vidogo, kwamba mmiliki wa haki ni sultan, kwamba Iman inafanya maajabu, kwamba haki ni yenye kushinda, na batili ni yenye kushindwa na itaangamia.

Ni udanganyifu kutumia uhalisia wa kisiasa kama kisingizio cha kueneza uoga, kuvunja moyo, udhaifu, na udhalilifu ili tubaki chini ya uvamizi wa umbile la Kiyahudi na maagizo ya muungaji mkono wake mkuu, mkuu wa ukafiri, Amerika. Hii ni sera iliyofeli ambayo itaongeza tu hasara yetu na itaongeza tu uvamizi wake, kiburi na majivuno yake.

Udanganyifu ni kujihami kwa kisingizio cha uhalisia chini ya kisingizio cha kujenga dola! Ni nini thamani ya amali yoyote ya kisiasa au ustawi wa kiuchumi – endapo itatokea – ikiwa ardhi yenu na anga zinakiukwa, ubwana wenu haujakamilika, na adui yenu ameenea katika ardhi na anga yenu, akivamia nyumba zenu asubuhi na jioni wakati wowote anapotaka, kuteka nyara, kuhoji, kutesa, kuua, na “kukufundisheni” kuweka sheria zake za udhalilifu juu yenu, huku parachuti zikiwa karibu na mji mkuu wenu. Haya yote ni huku mukiwa mumesimama na musitembeze misuli, mukitosheka na kulaani, kukashifu, na kupeleka udhalilifu wenu kwa Umoja wa Mataifa na mfumo wa kimataifa, ambao ni washirika na Mayahudi katika vita dhidi yetu na wizi wa kile kilichosalia cha adhama ya mapinduzi ambayo yamezalisha karibu mashahidi milioni mbili. Haya yote ni licha ya kuwa Mayahudi ndio viumbe waoga zaidi katika kupigana, na watu wa ash-Sham wana utashi, uamuzi, na azma ya kuing'oa milima?!

Makabiliano na Mayahudi hayaepukiki, na ucheleweshaji wowote una gharama zake. Daima tumekuwa tukisema kwamba umbile hili lemavu la Kizayuni ni umbile ovu na la khiyana, ambalo hakuna mikataba wala makubaliano yatakayofanya kazi, wala sera ya kutuliza au maridhiano haitafanya kazi.

Hii ni hasa baada ya kuona athari zao chungu na matokeo uwanjani. Ni uhamasishaji wa dhati pekee wenye kutikisa misingi yake na kutikisa kiti cha enzi cha umbile lake ndiyo utafanya kazi, ukivunja pembe yake dhaifu inayojitokeza inayozungumzia juu ya kiburi cha simba. Haya yote ni badali ya kuhangaika mbele ya umbile la Kiyahudi na kufungua njia za kuhalalisha mahusiano nalo kwa kisingizio cha kutafuta amani, usalama, na kujenga nchi na uchumi wake! Inafahamika vyema kwamba Marekani inaunga mkono, kwa uungaji mkono usio na kikomo, umbile la Kiyahudi na matarajio yake ya kujitanua kwa gharama ya ardhi na utajiri wa Waislamu. Inafahamika vyema pia kwamba Marekani inasukuma kuelekea katika kudhoofisha na kuzigawanya ardhi za Waislamu ili wasiinuke isipokuwa kwa mujibu wa yale yanayotumikia dira na maslahi ya Marekani, ya kwanza kabisa ambayo ni usalama wa umbile la Kiyahudi na kupiga vita kuregea kwa utawala wa Kiislamu kupitia dola kwa kisingizio cha “kupambana na ugaidi”!

Ndio, lau tungekubali uhalisia na uwongo na ngano za yasiyowezekana, tusingekuwa tumemuasi dhalimu hapo mwanzo ambaye aliungwa mkono na makafiri na wahalifu wa dunia. Tusingekuwa na subira, kusimama kidete, na imara kama milima imara, licha ya mihanga mikubwa iliyotolewa katika miaka yote ya mapinduzi.

Kwa miaka 14, hatukuwa na ndege, lakini tuliwalipua, na tulizuiwa kumiliki silaha hata moja ya kudingua ndege, kwa makubaliano ya kimataifa ya chuki na maovu.

Kwa miaka 14, tumepigana na utawala mkatili zaidi, licha ya uhalifu wake na nguvu ya jeshi lake la anga, na jeshi la anga la Urusi na muungano wa kimataifa unaouunga mkono, na licha ya kumiminika kwa wanamgambo wa Iran na Hizb yake nchini Lebanon, na wengineo. Wote kwa hakika wameujua ushujaa wa kweli wa watu wa ash-Sham na kushuhudia nguvu ya Imani yao, ushujaa wa ujasiri wao, na azma ya watu wao mashujaa.

Kwa miaka 14, Umma umekuwa ukiimba, عالجنة رايحين شهداء بالملايين “Tunakwenda peponi, kama mashahidi kwa mamilioni,” na kufichua rekodi iliyovunjika ya wasaliti kwamba hatuna nguvu leo ​​dhidi ya serikali, askari wake, washirika, na waungaji mkono wake.

Simba wa vita na askari wa uwanja wa vita walioonja utamu wa Iman, wakajihami nao na wakafanya jambo lisilowezekana kuwezekana. Waliyashinda matatizo, shingo zikainama mbele yao, na wakavunja minyororo na pingu za mantiki zilizofunga mikono ya wenye ikhlasi, na kuchelewesha kusonga mbele kwa wanamapinduzi kwa miaka mingi.

Wanaume wakweli walioamini Neno la Mwenyezi Mungu (swt), ambalo wale wenye mikono inayotetemeka walilisahau au walijifanya kulisahau. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ]

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini” [Surah At-Tawbah: 14].

Ndiyo, kama tungetenda kwa uhalisia, tusingepindua utawala wa zamani. Badala yake, vuguvugu letu likawa na silaha ya Iman na nyenzo muhimu. Ilikuwa ni harakati yenye lengo iliyoongozwa na Maneno ya Mwenyezi Mungu (swt), ambaye alisema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ] “Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Surah Muhammad: 47]. Na Yeye Aliyetukuka akasema,

[وَأَعِدُّوا لَهُمْ مَا اسْتَطَعْتُمْ مِنْ قُوَّةٍ وَمِنْ رِبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ]

“Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu” [Surah Al-Anfaal: 60].

Kwa kumalizia, tunakumbusha na kusisitiza kwamba sisi sio kiunganishi dhaifu zaidi katika mlingano kama vile watu wanaovunja moyo na wanaotishia wanavyokuuza. Sisi ni anga yenye nguvu, sio jicho lenye kuogopa. Sisi ni Umma wa Uislamu, Umma wa utambuzi na uthabiti, Umma wa kutoa na muhanga, Umma wa jihad na mauaji ya kishahidi, Umma bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu. Kinachokosekana ni Imam mwenye ikhlasi wa kuuongoza kwenye izza na utukufu chini ya utawala wa Uislamu na dola yake, Khilafah, dola ya utukufu, nguvu na kinga. Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara njema ya Mtume wake (saw). Kusimamisha Khilafah ni faradhi ya Shariah; hakika ni taji la faradhi zote. Kwa ajili ya kheri kubwa kama hii, basi wale wanaofanya matendo mema na wafanye matendo mema.

* Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Syria

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.