Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ujumbe kwa Watu Wetu mjini Gaza
(Imetafsiriwa)

https://www.al-waie.org/archives/article/19996
Jarida la Al Waie Toleo Na. 470
Mwaka wa Thalathini na Tisa, Rabi’ al-Awwal 1447 H sawia na Septemba 2025 M

Enyi mlio imara na mliojiweka kwenye mpaka wa vita katika mipaka mitukufu zaidi ya Uislamu: jueni kwamba dhiki na mitihani mnayopitia ni njia ya heshima duniani na daraja za juu kesho Akhera. Mwenyezi Mungu (swt) anakujaribuni kwayo ili kukutakaseni na kukuinueni daraja. Amesema (swt):

[قُل لَّن يُصِيبَنَا إِلاَّ مَا كَتَبَ اللّهُ لَنَا هُوَ مَوْلاَنَا وَعَلَى اللّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ]

“Sema: Halitusibu ila alilo tuandikia Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mola wetu Mlinzi. Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu!” [Surah At-Tawbah: 51].

Mwenyezi Mungu (swt) amekuandikieni Aliyokuandikieni, sio dhidi yenu, ili mzidi malipo na uthabiti, na inyanyuliwe bendera yenu miongoni mwa mataifa.

Jueni kwamba hakuna msiba unaoipata ardhi wala nyinyi wenyewe ila kwa kuwa ulikwisha andikwa na Mwenyezi Mungu (swt) kabla haujawa kama alivyosema Yeye Aliyetukuka,

[مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي أَنفُسِكُمْ إِلَّا فِي كِتَابٍ مِّن قَبْلِ أَن نَّبْرَأَهَا إِنَّ ذَلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسِيرٌ]

“Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika Kitabu kabla hatujauumba. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.” [Surah Al-Hadid: 22].

Hebu yakini yenu na iwe kwamba kile kilichokukoseni, hakikukusudiwa kukupateni, na kilichokusibuni, hakikusudiwa kukukoseni.

Hii ni Sunnah (Njia) ya Mwenyezi Mungu (swt) inayojirudia katika historia ya waumini. Hakuna watu waliojaribiwa na wakabaki na subira isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt) amewaruzuku ardhi. Jambo hili haliko mbali na yale yaliyowapata watu wa Musa (as) pale Firauni alipotishia,

[سَنُقَتِّلُ أَبْنَاءهُمْ وَنَسْتَحْيِـي نِسَاءهُمْ وَإِنَّا فَوْقَهُمْ قَاهِرُونَ]

“Tutawauwa wavulana wao, na tutawaacha hai wanawake wao. Na bila ya shaka sisi ni wenye nguvu juu yao.” [Surah Al-Araf: 127].

Je, maelezo haya leo sio hali ya adui yenu anayelenga watoto na wanawake na kudhani kwamba kwa nguvu zake ana uwezo dhidi yako?!

Watu wa Musa (as) ambao walikuwa wamechoka kutokana na dhiki, kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyosema:

[قَالُواْ أُوذِينَا مِن قَبْلِ أَن تَأْتِينَا وَمِن بَعْدِ مَا جِئْتَنَا]

“Wakasema: Tumeudhiwa kabla hujatufikia, na baada ya wewe kutujia!” [Surah Al-Araf: 129].

Haya ni maneno yanayoonyesha udhaifu na maumivu ya muda mrefu. Kisha likaja jibu la hakika la Musa, lililobeba ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya ushindi. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[قَالَ عَسَى رَبُّكُمْ أَن يُهْلِكَ عَدُوَّكُمْ وَيَسْتَخْلِفَكُمْ فِي الأَرْضِ فَيَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ]

“Musa akasema: Huenda Mola wenu Mlezi akamhiliki adui wenu, na akakufanyeni nyinyi ndio wa kufuatia kushika nchi, ili atazame mtavyo kuja tenda nyinyi.” [Surah Al-Araf: 129].

Hivyo basi Musa (as) aliwafundisha kwamba njia ya ukhalifa na uwezeshaji (tamkini) haifunguki isipokuwa kwa subira chini ya dhiki, na kwamba dhulma ijapokuwa ni kali, mwisho wake ni kupungua, na mwisho ni kwa watu wema.

Nyinyi leo munazungumza kwa sauti sawa na wao, na jibu ni hilo hilo kwenu. Mola wenu (swt) atawaangamiza maadui zenu na atakupeni ardhi baada yao kwa uthabiti wenu, ikhlasi yenu, na misimamo thabiti. Basi subirini na vumilieni na musimame katika misimamo thabiti, kwani ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitufundisha kuichukulia dhiki kwa yakini, akimwambia Ibn Abbas (ra), «...وَلَوْ اجْتَمَعُوا عَلَى أَنْ يَضُرُّوكَ بِشَيْءٍ لَمْ يَضُرُّوكَ إِلَّا بِشَيْءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللَّهُ عَلَيْكَ»“...na lau wakikusanyika ili kukudhuru, basi wasingeweza kukudhuru ila kwa alicho kuandikia Mwenyezi Mungu.”

Mnayostahamili yako mikononi mwa Mwenyezi Mungu (swt), si kwa adui; riziki yenu, muda wenu wa uhai (ajal), na vyeo vyenu viko kwa Mwenyezi Mungu (swt) na hakuna mwengine.

Enyi watu wa Gaza: nyinyi leo mmesimama katika msimamo wa Mitume (as) na watu wema, mkisimama kidete kwa ajili ya haki dhidi ya dhulma. Kila dhiki, kila jeraha, kila Shahidi ni riziki katika mizani yenu ya mema, na kunyanyua daraja yenu. Ukuruba wa Mwenyezi Mungu uko pamoja nanyi, na ushindi wake uko karibu, basi subirini na muwe thabiti, na furahieni kwa yale aliyoyaahidi Mwenyezi Mungu (swt) ya bustani na daraja, na heshima ya dunia ambayo hupatikana kwa uthabiti na kujitolea mhanga.

Mwenyezi Mungu (swt) akuwekeni imara, na akukunjulieni nusra yake (nasr), azifunge nyoyo zenu, na afanyie wepesi katika nyayo zenu, na akupeni afueni ya haraka na ushindi ulio wazi.

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.